Mwita Matteo
JF-Expert Member
- May 16, 2010
- 216
- 55
Kwa siku hizo 30, ningekua bado nawaza niongozeje?
Kabla hujaapishwa utakuwa umejipanga tayari.
Tunataka kujua ndani ya mwezi mmoja utakuwa umefanya nini? mwezi ukiisha unaachia ngazi tunaanza kukufanyia evaluation.
Haiwezekani ikawa mwezi mzima hujafanya lolote. Hata yule polisi muuwaji atakushinda?
Tupe mikakati yako, utakapoishia ni hapohapo.
Ningemweka SLAA Ndani... JELA. Kifungo cha maisha.
Kwenye red, waislamu watakuambia wanataka utumie sharia kutawala. Kama kiongozi wa nchi huwezi kuuliza swali la hivyo. Ni bora:Dah utakuwa rais wa aina yake ,hatuhitaji rais km wewe maana hata ukimnyonga huyo bwana bado matatizo ya watanzania yataongezeka, ningekuwa mimi ningefumua jeshi la polisi na hao ntakaowqchagua nitawapeleka shule wajue nini maana ya democrasia,nitasimamia uchumi kwa kuondoa misamaa ya kodi kwa wawekezaji,nitaagiza waliotunza fedha uswis wakamatwe mara moja, nitavunja baraza la mawaziri la wakereketwa na kuunda baraza la uwajibikaji ikiwa ni pamoja na kulipunguza ukubwa wake , pia nitafungua mjadala wa namna watanzania wanavyotaka kuongozwa
Nimekupa 100% Maana yake hapo unamaanisha ni kuheshimu utawala wa sheria! Kitu ambacho naamini ndicho kinachomsumbua JK na utawala wake na ndicho kitakacho mfanya siku moja aje asimame mbele ya mahakama kujibu tuhuma (Hili wana CCM kama akina William Malecela waelewe kuwa ipo siku JK atakuja kusimama mahakamani kujibu shutuma za mauaji).Swali gumu sana mkuu hata hivyo ngoja nijaribu kujibu. Ningeteua watu wenye matazamo chanya wa kuleta maendeleo ya dhati kwa nchi watakaofuatilia mienendo ya wabunge jinsi walivyoingia kwenye uongozi kama ni halali au sivyo hasa kuangalia la rushwa na ghiliba nyingine. Ningewaita viongozi wote wa CCM, wabunge na baadhi ya wanachama kadhaa toka kila mkoa kwa uwiano kulingana na wingi wa wanachama kwenye mkutano wa dharura utakaochukua wiki moja. Kuwe na moderator anayefahamika kwa weledi bila upendeleo. Katika mkutano huo agenda kuu zitakuwa kama zifuatazo:
- Kupitia katiba ya chama cha Mapinduzi na kuonyesha mambo yaliyokiukwa au kwa kujua au kwa kutokujua
- Kujadili yale yote yalijitokeza kwenye mapitio ili yawe msingi wa kuchukua hatua za kukinusuru chama. (Maoni haya ni shirikishi kwa kuwa wanachama wote wamewakilishwa). Pia wanachama ambao hawakuweza kuhudhuria japo wamewakilishwa, watume maoni yao kwa njia mbalimbali za mawasiliano ya hapo kwa papo
- Wanachama wasio viongozi watapiga kura ya siri kuonyesha wabunge na viongozi wengine waliokiuka katiba kwa kushiriki rushwa na mambo mengine.
- Kujumuisha kwa pamoja yaliyojiri kutokana na michango yao na wachangie hatua za kuchukua ili ziwe ni kutokana na wao wenyewe kwa njia shirikishi bila kutaja majina. Hii itasaidia kupunguza manung'uniko.
- Kuchagua kamati maalum (watu waadilifu na wenye weledi wa taaluma za elimu ya kisiasa na jamii) ya kusaidia kuainisha hatua za kuchukua kulingana na kvifungu vya katiba vilivovunjwa
- Kuandaa hadidu rejea kwa ajili ya kamati maalum itakayoundwa
Wakati wote wa mkutano kuwe na ulinzi makali kuzuia rushwa na ghiliba za aina zote na ikiwezekana zitumike njia za kielektroniki kama kamera na mengine kama hayo
Mkutano huu ufanyike katika wiki moja mpaka ya pili ya mwezi Septemba 2012
HADIDU REJEA KWA KAMATI MAALUM YA KUAINISHA HATUA ZA KUCHUKUA DHIDI YA WANACHAMA WA CCM WANAOKIUKA KATIBA YA CHAMA (Muda siku saba)
- Kuainisha hatua za kuchuka kulingana na kifungu cha katiba kilichovunjwa na wahusika
- Kuorodhesha hatua na wahusika zikijumuisha onyo, onyo kali, kufukuzwa uanachama na kufunguliwa mashtaka bila kujali wadhifa wa mwanachama na wataarifiwe kwa barua kura zilivyoamua juu yao
Wiki ya mwisho ya Septemba, baada ya kusafisha nyumba ya CCM uchaguzi mkuu uitishwe kwa kuzingatia uhuru wa mawazo na itikadi za vyama halali vya kisiasa ilihali hakuna uvunjifu wa sheria za nchi.
Note: Wakati wote huu dhamira na mtazamo viwe ni kukinusuru chama tawala na kuleta utawala wa haki kwa nchi kwa njia ya uchaguzi huru hata kama CCM au chama kingine kitakuwa chaguo la wananchi.
I would try to be the best president ever.
Ningesimamisha shughuli za vyama kwa muda ili watu wakafanye kazi za kuzalisha mali kwanza katika kilimo, ufugaji, viwandani. Wananchi wote masikini sana vijijini na walio katika mazingira magumu watafutiwe shughuli za kujiingizia kipato na kujikimu, shughuli za vyama vyote ningezielekeza huko kuhakikisha watu hawa kwanza wanatoka katika umaskini kwa shughulki zao wenyewe.
Ningebadili jukwaa la siasa hapa JF kuwa jukwaa la kilimo na uzalishaji, kwa kuwa wanasiasa nitakuwa nimeshawapa ban hapo juu then hakutakuwa na cha kuandika na kuchangia. Kuongeza capacity ya magereza na kusimamia sheria kama zilivyo andikwa ili mkizingua tu unajikuta ndani ya bar mpaka mnatakapo nyooka ndio tutayabadili kuwa shule baadae. Wabunifu, wagunduzi na kuenziwa kwanza wataendelezwa na kupewa priveledge zote kama viongozi wa juu, yaani wanapita VIP lounge na gamba jeusi tax exemption na ulinzi wa dola. watu magumashi woote watashika adabu ndani ya huo huo mwezi.
Ningesimamisha shughuli za vyama kwa muda ili watu wakafanye kazi za kuzalisha mali kwanza katika kilimo, ufugaji, viwandani. Wananchi wote masikini sana vijijini na walio katika mazingira magumu watafutiwe shughuli za kujiingizia kipato na kujikimu, shughuli za vyama vyote ningezielekeza huko kuhakikisha watu hawa kwanza wanatoka katika umaskini kwa shughulki zao wenyewe.
Ningebadili jukwaa la siasa hapa JF kuwa jukwaa la kilimo na uzalishaji, kwa kuwa wanasiasa nitakuwa nimeshawapa ban hapo juu then hakutakuwa na cha kuandika na kuchangia. Kuongeza capacity ya magereza na kusimamia sheria kama zilivyo andikwa ili mkizingua tu unajikuta ndani ya bar mpaka mnatakapo nyooka ndio tutayabadili kuwa shule baadae. Wabunifu, wagunduzi na kuenziwa kwanza wataendelezwa na kupewa priveledge zote kama viongozi wa juu, yaani wanapita VIP lounge na gamba jeusi tax exemption na ulinzi wa dola. watu magumashi woote watashika adabu ndani ya huo huo mwezi.
Kila mmoja wetu nadhani kwa njia moja ama nyingine ameguswa na matukio ya kila aina yanayotokea hapa nchini. Watu wengi wamekuwa wakirusha lawama za kila aina kwa mh. JK.
Sasa inawezekana kabisa hapo alipo amezidiwa na hajui afanye nini kwani aidha washauri wake wakuu wanamuangusha ama hawasikilizi au inawezekana pia, wote hawana mikakati yoyote. Inawezekana kabisa wanaona nchi inavyokwenda ni sahihi kabisa.
Sasa je mwana JF, ungefanya nini katika kipindi cha mwezi mmoja tu ambacho ungejaliwa kuwa RAIS wa nchi hii?
Only constructive suggestions and opinions are needed na wala si utani na matusi kwani tunakusanya maoni tuyafanyie
kazi.
KARIBUNI KUCHANGIA.:welcome: