Ungana na sisi uwe mwenye nguvu

naan ngik-kundie

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
1,766
2,423
Poleni na pilika pilika za kuukaribisha mwaka mpya 2017.

Kwa kipindi kirefu sana nimeitafuta Amani ya moyo lakini kwa kipindi chote sijawahi kuiona, Amani yenyewe ni Pesa. Moyo wangu umekua na shauku ya mafanikio makubwa na kuona malengo yangu yanatimia kwa wakati, lkn siku zote za maisha yangu hii ndoto haijawai kutimia wala ata kuona nakaribia ndoto hii. Nimefanya yote ambayo nilihisi wenda inaweza kuwa njia ya kunifikisha kwenye mafanikio makubwa lakini nimekua naambulia patupu. nimekuwa mtetezi wa wanyonge, mtenda haki na mwenye kutoa kwa wasiokua nacho lkn yote haya bado yameonekana wenda ndiyo kikwazo cha safari yangu.

Nikafikili sana kwanini wengine wanafanikiwa? Nikaona bado Nina mengi ya kujifunza kwa waliofanikiwa. Lakini wengi wao wenye mafanikio wamekua ndiyo watu wenye maovu mengi kupindukia, wamekuwa wapinga haki, wamekukua watetezi wa wanyonge lakini nyuma yake wana maslahi yao binafsi. Ni ngumu sana kumpata mtu aliyefanikiwa kwa halali, lazima nyuma yake kutakuwa na kashfa nzito sana za mafanikio yake, aidha dhuruma, wizi, unyonyaji au njia nyingine yoyote mbaya.

Nimeamua kwa moyo wangu wa dhati bila kushinikizwa na mtu kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM. Kwa sababu naamini siku zote mwenye nguvu anashindana na mwenye nguvu. Siwezi kushindana na aliyeshiba wakati mimi Nina njaa, ukitaka shibe, ukitaka kunywa mpaka pomoni basi simama upande wa mwenye nacho, na pia ukitaka pesa kaa karibu na wenye pesa.

Nimechoka kuongozana na wanafiki ( mtu anakwambia tusonge mbele tuko pamoja wakati yeye nyuma ya pazia anatii upande wa hadui yenu) wacha sote tuwe watumwa wa hadui siku tukishiba na tukapata nguvu basi tutatafuta haki ya ardhi yetu.

Familia kwanza Chama baadae.

Samahani kwa uandishi mbaya maana natumia simu.

Karibuni.
 
Back
Top Bottom