Unga, Bangi, pembe za ndovu zilifanyika kwenye vibanda vya machinga

kipindi cha jakaya kulikuwa na maduka ya nguo full AC na muuzaji hapo dukani kapendeza anatumia iphone,viwanja vikali una mkuta.
lakini duka wiki nzima hata mteja wa kununua nguo hayupo
 
kipindi cha jakaya kulikuwa na maduka ya nguo full AC na muuzaji hapo dukani kapendeza anatumia iphone,viwanja vikali una mkuta.
lakini duka wiki nzima hata mteja wa kununua nguo hayupo

Ndio tunarudi huko sasa subiri uone, nampinga Rais Samia lakini anafanya vizuri mambo yatabadilika sio muda
 
Hilo Nenp mmachinga mnalitumia vibaya.
Kwa hyo unaona NI sahihi wengine wateseke kwa ajili ya huyo rafiki yako?
 
Naanza na kisa cha rafiki yangu anaitwa B .

B anazaliwa machame ni muhitimu wa chuo kikuu alisomea mitambo pale MUST.

B baada ya chuo alianza biashara ya kuuza bangi mjini mbeya baadae akanieleza amehamia DAR ameamua kujiongeza kutokana na ruhusa ya machinga kuruhusiwa popote.

Ndio mwamba aliendelea na biashara yake alichofanya alinunua friji tano na madeli matano ya kuzugia na aliajiri vijana watano wote akawakatia vitambulisho vya machinga wao wale vijana na B hukutana usiku kwenye center fulani kupanga mpango wa kesho.

Kwa ufupi ilikua sio machinga wala nini zilikua sehemu za kupokelea mizigo ya madawa ya kulevya na kuanza kusambaza maeneo mbalimbali, vibanda vilikua maeneo yafuatayo Kigamboni, Makumbusho, Manzese, Kimara Mwisho, Segerea sasa vijana wake wote walifahamiana na walifanya kwa weledi mkubwa iwe kupokea vipodozi sawa maana mzigo ukifika kwenye basi unapelekwa point nyingine chap huku akiufuatilia na boksa kwa nyuma.

Iwe kupokea pembe ilikuwa chap mzigo unafika unapokelewa chap unaenda alikojua yeye.
Iwe kupokea bangi ya musoma, Bukoba au tabora ndio mapigo yake hayo,

Iwe kupokea unga na kupeleka sehemu ya kufungia kipimo cha buku tatu tatu sawa tu kazi inafanyika.

Yes B ndani ya miaka 4 kapata pesa nyingi sana kwa kutumia kivuli cha machinga.

Kwa hiyo sio kila kibanda ilikuwa cha machinga, vingine ilikuwa kuzugia tu kupokelea mizigo ya pesa nyingi kwa hili naipongeza Serikali

Nitawaletea kisa kingine cha viabanda vya machinga siku nyingine.
Novel
 
Back
Top Bottom