David Mataka wa ATCL, ahukumiwa kulipa faini Tsh milioni 8 kwa kulisababishia hasara ya Tsh Bilioni 71 shirika

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,220
12,937
Bosi wa zamani wa ATCL, David Mataka amehukumiwa kwenda jela miaka minne ama kulipa faini ya Sh milioni 8 baada ya kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi na kusababishia shirika hasara ya Sh bilioni 100.

====

Mataka wa ATCL Ahukumiwa Jela Miaka 4​

August 20, 2021
mataka.jpg


Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka amehukumiwa kwenda jela miaka minne ama kulipa faini ya Tsh milioni 8 baada ya kukutwa na hatia katika mashtaka waliokuwa wakikabiliwa nayo.

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa, Agosti 20, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega katika Mahakama ya Kisutu ambapo pia Mahakama hiyo imewahukumu watuhumiwa wenzake ambao ni Ramadhani Mlinga Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), na aliyekuwa mwanasheria wa mamlaka hiyo, Bertha Soka kifungo cha mwaka mmoja ama kulipa faini ya Tsh milioni 2 kila mmoja.
mataka-1.jpg

Mattaka na wenzake walikuwa akikabiliwa na mashitaka sita likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 71. Wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi zaidi ya 20 na vielelezo.

Ilidaiwa mahakamani kuwa, Oktoba 9 mwaka 2007 wakati Mattaka akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, alitumia madaraka vibaya kwa kusaini mkataba wa kukodisha ndege aina ya Airbus na kwamba mkataba huo unadaiwa kuisababishia serikali hasara ya zaidi.

Katika shitaka lingine Dk Mlinga na Soka walidaiwa kuwa Machi 19, 2008 katika ofisi za PPRA Ilala, Dar es Salaam walighushi muhtasari wa kikao wa tarehe hiyo, wakionesha kwamba mamlaka hiyo ilikaa kikao na kujadili maombi ya kuidhinisha ATCL ikodishe ndege hiyo.

Pia soma: Mahakama imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa ATCL, David Mataka kifungo cha miaka 6 au faini ya milioni 35
 
Kama walishamfanyia confiscation ya baadhi mali zilizotokana na hasara aliyotia hiyo inaweza kuwa adhabu

Vinginevyo hayo ni masihara
 
Back
Top Bottom