UNESCO yakubali Uranium kuchimbwa Selou Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UNESCO yakubali Uranium kuchimbwa Selou Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bornvilla, Jul 4, 2012.

 1. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 921
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  UNESCO imeridhia uranium kuchimbwa Tanzania.

  Balozi Kagasheki amesema kulikuwa na upinzani lakini sasa tumeridhiwa kuchimba uranium.

  Source: TBC1
   
 2. M

  Mr. Chi Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ni jambo jema endapo tu! tutafanya shughuli hizo za uchimbaji kwa namna ambayo hatutaathiri mazingira yanayolizunguka eneo la uchimbaji,na ukizingatia mgodi huo utakuwa karibu sana (with sharp boundary) na hifadhi hiyo ya selou ni rahisi sana kuathiri bayonuai/biodiversity katika hifadhi hiyo. imekuwa ni kawaida yetu kuji-commit kama tulivyofanya safari hii kwa UNESCO kwamba tutaendesha shughulu za uchimbaji bila ya kuathiri mazingira, sehemu ya mapato itaendeleza hifadhi ya selou na pia jamii zinazozunguka eneo lile kupatiwa huduma za jamii na kampuni itakayokuwa inaendesha machimbo hayo,lakini uzoefu katika nchi yetu unaonyesha kuwa hayo yote huwa hayafanyiki/ama yakifanyika ni kwa kiasi ambacho ni tofauti na makubaliano. kwa mfano yaliyokwisha tokea katika mgodi wa nyamongo/north mara na kwingineko sisi wote ni mashuhuda. Tusiruhusu mazingira yetu kuharibika kwa jina la uwekezaji, mwisho wa siku mwekezaji ataondoka na tutabikia na madhara katika mfumo wa ikolojia ya nchi yetu, na kwa bahati mbaya sana uharibifu mwingine katika mazingira ni irreversible...hauwezi kurudisha katika hali yake ya awali hata kama unge-invest pesa kiasi gani.

  Tuyalinde mazingira yetu na raslimali za nchi yetu, na iwe na kwa faida ya watanzania wote na sio wachache wala wageni!
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 201
  Trophy Points: 160
  Aloo hayo madini ya Uranium hayana bei kubwa katika soko la kimataifa,ni moja ya madini yenye bei ya chini kabisa ,usiwekeze kwenye tamaa kuwa yatasaidia nchi kwa kupata hela ya kigeni.labda kwenye black market.na ni kosa kuuza huko tena kosa la jinai.

  Umuhimu ni kutuwezesha sisi kuyatumia kwa kutuzalishia umeme ,jambo ambalo si rahisi kupata leseni yake.
   
 4. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2016
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,111
  Likes Received: 1,483
  Trophy Points: 280
  Kagasheki anaweza kutuambia pamoja na kuwa yeye si Waziri tena hapa hawajatuingiza chaka kwa kushirikiana na UNESCO?
   
Loading...