Undumira kuwili kwa Anne Semamba Makinda kumeshusha hadhi ya bunge.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Bunge kama mwakilishi wa wananchi, linapashwa kuendesha mambo yake kwa uwazi kabisa na kwa kutanguliza maslahi ya nchi kuliko ya vyama vya siasa. Mtu pekee ambaye yuko katika nafasi nzuri ya kuhakikisha kuwa hayo yanatendeka ni spika wa bunge hilo. Kwa bahati mbaya spika aliyopo sasa, tangu aingie madarakani ameonyesha wazi wazi ya kwamba yuko pale kulinda maslahi ya chama chake na wala siyo ya wananchi wanao mlipa. Na hivyo amekuwa akitumia madaraka yake siyo tu kuwanyima fursa wabunge wa upinzani, hasa wa kutoka CDM, kutoa hoja zao kwa uhuru, lakini mara nyingi ameonekana kupindisha sheria ili kuwalinda wabunge kutoka kwenye chama chake kutokana na kusema uongo bugeni. Hali hiyo inaanza kuwafanya baadhi ya wabunge na wananchi kwa jumla kupoteza imani yao kwa mama huyo. Tafrani iliyoibuka jana humo bungeni, ni ushahidi tosha unadhihirisha ni kwa kiwango gani baadhi ya wabunge walivyoanza kutilia shaka uwezo wa mama huyo wa kuwatendea haki wabunge wote bila ya kujali vyama vyao. Pasipo kujirekebisha huko mbele ya safari uenda tukashuhudia visa vya kurushiana ngumi humo bungeni.
 
Mbona tangu mwanzo tulishayaona haya na tukayasema. Huyu mama ni kibaraka cha mafisadi.
Namshangaa sana kwa umri huu kukosa busara kwa kushindwa kuendesha bunge objectively instead amekuwa akionyesha wazi ukandamizaji na ubabe mkubwa usio kuwa na tija.
Mungu inusuru Tanzania katika mikono hii ya ajabu!
 
Hivi Sitta yuko wapi angekalia kiti Temp .kukiwa na issure kama hii? Sitta nae kwa kujificha!!
 
Wembe ni ule ule mama Makinda, Kazi moja hadi wakome, naona pumzi fupi route ndefu wameanza kulalama.
 
Nadhani busara na hekima zinatakiwa wakati wa maamuzi kama haya na jana tumeshuhudia jinsi wabunge walivyoonyesha kuwa si wamoja, lakini wacha wale wenye kuendelea na zomea zomea wakisahau kutoa michango 2015 wataadabishwa na wapiga kura wao. Mtz wa leo anaona live bunge jinsi linavyoendeshwa na kama kuna kuonewa inaonekana live sasa sijui utamdanganyia wapi. Jamani usimwamshe alielala......!!
 
Yote hayo yatokana na kukidhi matakwa ya waliomuingiza kwenye uspika. sioni sababu ya KUPINDISHA KANUNI. Hao wanaosema na kusifia kasi yake ni vipofu ambao wanatia aibu kwa kufikiriria maslahi yao binafsi bila kujali wananchi waliowachagua kutokana na umri wake sikutegemea kama anaweza kujidhalilisha kiasi hicho kwa kujionyesha ujinga alio nao. POLENI wana CCM waelewa tumeona umbumbumbu wa viongozi wenu mlio wapa dhamana ya kuwaongoza.
 
mwacheni aendelee na upumbavu wake lakini iko siku atalia machozi hapo kwenye hicho kiti
 
huyu mama anatakiwa atokee mbunge mmoja wa upinzani chizi amwache makofi yavimbe mashabu kama alivyopigwa gbagbo na wote watoke nje hana adabu kabisa tena za kuzaliwa....
 
huyu mama mie nahisi ana matatizo ya akili, anamzidi mwendawazimu kwa kuvaa nguo tu... andhihirizha kuwa wanawake wa kibongo bado hawana ability ya kushika post kubwa kama hiyo....shame one woman...!.
 
Hapana mkuu!! Wanawake wanaweza kuongoza. Ni aina ya waliyemuweka hapo si wanawake wote. Kwani wanaume wote wanaweza uongozi?
huyu mama mie nahisi ana matatizo ya akili, anamzidi mwendawazimu kwa kuvaa nguo tu... andhihirizha kuwa wanawake wa kibongo bado hawana ability ya kushika post kubwa kama hiyo....shame one woman...!.
 
Wameweka zigo(Makinda) na sasa naona hata TV zimezuiwa kuonyesha vipindi vya bunge,TBC yao naona inaonesha miziki,wasanii,warembo,kamati kuu ya CCM n.k badala ya bunge,kweli mda ndo huu wa kuondoa mirija hii ya wanyonyaji makupe wa nchi yetu na chama chao...siku yaja na iko karibu kama kesho
 
Back
Top Bottom