Undugunization (Nepotism) ndani ya PPF: Ajira zenye mashaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Undugunization (Nepotism) ndani ya PPF: Ajira zenye mashaka

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by mchukiaufisadi, Jan 12, 2011.

 1. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  PPF IMEAJIRI WATOTO WA VIGOGO MBONA WA BOT WALISHTAKIWA?

  Miaka michache iliyopita BOT ilichunguzwa jinsi ilivyojaza watoto wa vigogo.

  PPF kama shirika la umma, ajira inatakiwa iwe kwa watanzania wenye sifa na waajiliwe kwa utaratibu wa wazi. Lakini sio hivyo kwa PPF wengi wameajiliwa kwa maagizo ya wakubwa au kujipendekeza.

  Mifano michache:
  1. DG ERIO: Mjomba wa Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa. Aliajiliwa kwa shinikizo kama mwanasheria. Mwezi mmoja kabla Mkapa hajaachia uraisi akamtoa aliyekuwa DG na kumweka mpwawe ERIO.
  2. Modigard Lumbanga: Mtoto wa aliyekuwa Katibu mkuu Kiongozi, Martin Lumbanga. Aliajiriwa kwa shinikizo wakati baba yake akiwa katibu mkuu kiongozi.
  3. Musiba: Mtoto wa Marehemu Elvis Musiba. Aliajiliwa wakati baba yake akiwa Makamu wa mwenyekiti wa Bodi. Huyu alikuwa ulaya, PPF walighalimia gharama za kumsafirisha kuja kufanya interview. Hakuna mfanyakazi yeyote aliyefanyiwa hivyo hata kama anatokea Kibaha.
  4. Dozite Musofe: Shemeji wa Mr. Ngumbulu. Alimleta PPF wakati Ngumbulu ni mwenyekiti wa Bodi ya PPF pia Katibu mkuu Hazina
  5. Hawa Mwema: Huyu ni mtoto wa IGP Mwema. Hivi sasa mikakati inasukwa apewe Umeneja wa utawala baada kumtoa aliyekuwepo kwa mizengwe.
  6. Idara ya uwekezaji DG ERIO kamweka ndugu yake mtoto wa Mzee Magani, ambaye ni ndugu Rais mstaafu Mkapa. Huku ndiko anakotumia erio kuiba pesa ya wanachama.


  Wengine wamejaa watoto wa majaji (eg Assumpta Maina na Nicander Kileo) angalia surnames zao

  Wengine ni watoto wa Bodi Members eg wa Monica Mbega. Aliajiliwa akiwa bidi member.

  Naomba wenzangu mnaochukia ufisadi mniongezee orodha.


  Kama BOT serikari ilichunguza EPA, Majengo pacha na ajira za watoto wa vigogo basi na hapa PPF ichunguze GROUP ENDOWMENT (EPA ya PPF), Tenda za Majengo ya DODOMA, viwanja waligawana mkurugenzi wa fedha na mkaguzi wa ndani na ajira za watoto wa vigogo.

  NISAIDIENI MWENZENU NAUMIA MADARAKA YANAPOTUMIKA OVYO.
   
 2. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 689
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mchukiaufisadi Hongera sana!

  Kwa kweli hili shirika la PPF ni kuzunzungu kabisa na hayo yote uliyoyatoa ni sahihi kabisa na tena utashangaa huyu dada Hawa Mwema alifanya kazi PPF kwa muda mfupi ndipo na sijui kama hata probation yake ilikuwa ime-mature akaenda UK kusomea Masters degree katika Public Administration aliporudi alerejeshewa ajira yake.

  Wakati kuna mabinti na vijana ambao hufanya kazi kama matempo kwa muda zaidi ya miaka mitatu na huwa hawapati hiyo ajira na mchezo huu upo sana pale Kurugenzi ya Komputa, Operesheni hata Rasilimali Watu na bila kusahau na idara na kurugenzi zingine nazo pia zina huo mchezo mchafu wa kuwasotesha wasoma kwa kutowapa ajira za kudumu.

  Staff wa tempo PPF ambao ni mabinti wasio na support toka kwa vigogo bali ni watoto wa wavimba macho wao walie tu kwani wanaweza kupata ajira pale tu Erio akipewa uloda. Mmari, Kashimba, Mganga na Carina huwa wananguvu sana katika kupandisha vyeo na kumshusha mtu cheo na hata kumwamisha idara moja kwenda nyingine iwapo waowahitaji kufanya hivyo.

  Mengi yanakuja wana JF.
   
 3. m

  msitaki Member

  #3
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Hii ni hatari sana...afu jamaa wanavyoonekana wastaarabu wakina nje ya huo mjengo....kumbe uozo mtupu!!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 5,944
  Likes Received: 536
  Trophy Points: 280
  Mimi sihujui huuu utaratibu wa undugunization utatufikisha Mahala gani, ninachojua kwa vyvyote mwisho wa siku kunakuwa hakuna perfomance.

  Haya Mashirika yameachiwa Uhuru sana kana kwamba wao ndio wenye uamuzi wa chochoye kuhusu mashirika hayo wamesahau kuwa hayo ni mashirika ya umma na kuwa mwisho wa siku watanzania ndio wenye maamuzi.

  Viongozi waliopo ni dhamana tu ila mwisho wa siku ni shirika la watanzania kwa manufaa ya watanazani iweje watu wachache wachafue mashirika ya watanzania zaidi ya mil 40!

  Hivi watanzania tumerogwa au ni nini jamani, mbona kila mtu anafanya kila kitu bila waliopewa dhamana kushtuka? Mi nachoka kabisa kwa kweli!
   
 5. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,465
  Likes Received: 4,090
  Trophy Points: 280
  Ohh kumbe zile kazi walizo tangaza ni viini macho.
   
 6. TATIANA

  TATIANA JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 4,016
  Likes Received: 399
  Trophy Points: 180
  sasa kwann wanatufanya ss mazoba kwa kutoa nafasi hewa?
   
 7. M

  Matarese JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 514
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwa bongo, mambo kama haya sio PPF tu, ila mashirika karibu yote ya umma yapo hivyo! Tatizo kubwa linalosababisha haya ni kulindana, mfumo ambao umekuwepo Tanzania kwa miaka mingi. Labda katiba ikibadilishwa au CCM ikitolewa madarakani ndio mambo haya yanaweza kupungua.
   
 8. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2011
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 689
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nondo zingine upendeleo wa ajira PPF:

  1. Ms. Hawa Mwema ni mtoto wa IGP Mwema na huyu binti ni mjomba wa Jakaya Mrisho Kikwete, sister wa JK kazaa Hawa, kwa mtindo hapa hakuna jipya ni yale yale ya kule kwetu mzenga.

  2. Ms. Maimuna Masebu ni dada yake Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mr. Masebu yuko idara ya PMU,

  3. Mr. Sabuni yenye akuajiriwa kama Principal officer ktk PMU na sasa ni meneja wa procurement na yeye inasemekana ameletwa na Mgonja Mwenyekiti wa Bodi ya PPF mstaafu ambaye yuko mahakamani kwa kesi ya ubadhilifu wa pesa za Hazina kwa kutoa misamaha ya kodi. Huyu jamaa bado ana undugu na mzee vijisenti Chenge kama shemeji yake.

  Sasa je mtoto wa sakala atapata kazi atafumania kazi hapa nchini kama hataishi kwenye ujambazi wa kutumia silaha na kuwa tapeli wa kimataifa. Hicho kwa siku za baadaye Tanzania tutegemee kwani tutengeneza sumu mbaya sana kwa siku za usoni.
   
 9. s

  sexon2000 JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 305
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wana PPF wekeni humu madudu yote yanisaidie ninapowasiliana na TUME YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA.

  Erio kesha anza kuongea na baadhi ya watu wake kule kwenye tume ila wamesema hawatababaika na watasimama kwenye ukweli mtupu.

  Tajeni wafanyakazi wote tunaoamini eidha wallingia kwa title za wakubwa au za waliingia kwa NGONO na wakurugenzi wa PPF.

  Msimsahau aliyeingia kwa mkono wa Waziri wa Fedha Mkuro na kupewa UMENEJA WA KANDA na kuacha walioshinda INTERVIEW
   
 10. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,099
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Erio aliingizwaa na mkapa, anza nae
   
 11. C

  Campana JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Du. Mimi nasikitikia michango yangu ya kila mwezi. Kwa hali hii iko salama kweli?
   
 12. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,821
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hili la undugunaizesheni litauwa haya mashirika muda si mrefu,waingizwe kwa vigezo na siyo mtoto wa anti au anko..
   
 13. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,397
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Kaka tuwekee na CV au Qualifications za hao uliowataja hapa ili tuangalie na upande wa pili. Tusilaumu tu kuwa wameingia kwa njia za vimemo, tujiulize pia are they Qualified for those Posts???
   
 14. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,190
  Likes Received: 3,122
  Trophy Points: 280
  mi nafikiri tupate cv zao maana nasema hivi kwa kuwasaidia watanzania makelele tutapiga lakini watu wanendelea kula shushu tunabaki mabwege we kama una ushahidi shule aliyonayo aikidhi mahitaji tumwagie hadharani wala usi PM mtu tuwake nazo...tatizo hata wa BOT akuna aliepata ushahdi na ndio maana nikasema umesikia BOT kama wametoka na kama sio pole sana
   
 15. WA MAMNDENII

  WA MAMNDENII JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2011
  Joined: Jun 5, 2010
  Messages: 287
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  taratibu za ajira ppf zinasemaje sijui , cv ddo inajalisha kupata ajira au kujuana zaidi?
   
 16. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,711
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Pheww!!
   
 17. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,919
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Huyu ni nani nimempata kwenye contact us.
   

  Attached Files:

 18. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 742
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Someni kitabu kinachoitwa " Who moved my Cheese" , kelele zote zitaisha. Inatakiwa uendane na mabadiliko yanayotokea kwa haraka sana, na bila hivyo mtaishia kulalamika kila kukicha.
   
 19. T

  Tunsume Member

  #19
  Jan 13, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Ajira bila upendeleo ni haki ya kila Mtanzania hivyo basi hata watoto wa vigogo wanahaki kuajiriwa kama walivyo-wa Tanzania wengine pale ambapo wanavigezo vyote vinavyokidhi mahitaji ya kazi husika.

  Hata hivyo, ni ukweli usiopingika kwamba kwasasa Tanzania kama huna jina kupata ajira ni ngumu kwasababu nafasi katika ajira za umma zinatolewa kwa upendeleo na kujuana kwa kwasababu nyingi ukijumlisha ukabila/undugu/urafiki/uhusiano wa kimapenzi etc. Hili tatizo si la kulichekea na ndiyo maana Katiba Mpya itatusaidia sana kutoa haki katika ajira Tanzania.

  Ajira ni moja ya fursa ambayo ni haki ya kila Mtanzania kama anavyo vigezo. Haki hii inakwenda inategemea zaidi haki ya kila Mtanzania kupewa fursa ya kujenga uwezo wa kuwa na vigezo muhimu vya kutumia/kupata haki ya ajira, kama vile elimu na afya. Mara nyingi, watu wamekuwa wanasema fulani kapewa ama kateuliwa kwa kazi ile kwa vile anauwezo .

  Kuwa na uwezo ni swala la kisiasa na linatokana na maamuzi ya ugawaji wa rasilimali za taifa ikijumlisha kodi/bajeti ya elimu etc. Kwa vyovyote vile itakuwa vigumu kwa mtoto wa mkulima aliyesoma shule ya msingi yenye mwalimu mmoja kwa wanafunzi 60, ama wanafunzi 80 darasa moja la ukubwa wa mita 9 kwa tisa; wanafunzi 6 kuchangia dawati (kama wanabahat) ama kukaa chini, shule ya sekondari yenye mwalimu mmoja kwa wanfunzi 60 kushindina na mtoto wa 'imposed, fake or legal' kigogo aliyesomea shule ya msingi ya academy, sekondari ya academy au nje ya Tanzania na Chuo nje ya Tanzania.

  Jinsi gani Katiba mpya inaweza kupunguza dhana ya kutokuwa na haki katika ajira ama dhana ya upendeleo katika ajira na kutoa fursa kwa kwa watoto wa vigogo na wa-Tanzania wengine. Hapa Kenya, Katiba imeweka wazi kuwa mtu hatabaguliwa katika ajira kwa misingi ya kabila/kundi;umri;hali ya afya;hali ya kiuchumi/kisiasa/kijamii.

  Pia mtu mmoja hata bambikiwa vyeo kwasababu tuu anaonekana yeye tuu ndiyo anauwezo. Katika hili, kufuatia Katiba Mpya Kenya, kama umeteuliwa kwenye commission za kikatiba na unashika wadhifa mwingine serikalini unapaswa kuachia ngazi.Pia kamati za bunge zimepewa mamlaka kuchunguza ajira zenye utata na zinazokiuka sheria.

  Hapa Juzi Waziri wa Mbao ya Nje pamoja na kuachia ngazi kwa tuhuma za rishwa ya jengo la Ubalozi Japan, kama Prof, Costa Mahalu, ameletewa kashfa mpya iliyochunguzwa na bunge na kukutwa kuwa uteuzi na upewaji wa ajira za mabalozi na watendaji zilishawishiwa na undugu, kujuana, mahusiano ya kimapenzi na mengineyo.

  Pia wafanyakazi karibu 2,500 wa sekta ya elimu watafukuzwa kazi kutokana na kuajiriwa kwa misingi ya ukabila/undugu/urafiki/upendeleo/mahusiano ya mapenzi etc. Hata Tanzania, misingi mikubwa ya ajira katika utumishi wa umma ni undugu/ukabili/uhusiano wa kimapenzi/urafiki/kujuana. Hii ni misingi mibovu na inajenga matabaka; uhasama na chuki katika jamii na mwisho wa yote ni vita ya wenyewe kwa wenyewe. Kwasasa Tanzania kuna waTanzania wako katika kila uteuzi na ajira zenye kulipa vizuri ikijumlisha commission na miradi yenye kufadhiliwa na ama Benki za Dunia etc.

  Ni utawala mbovu kwa PPF kuajiri watoto wa bodi membas, kama hii ni kweli hata wangekuwa na vigezo wanatakiwa wachunguzwe kama kweli uwepo wa ndugu/wapenzi/wazazi wao kwenye bodi haukushinikiza wao kupewa kazi.

  Mfano mzuri ni kwenye nafasi pia za upendeleo kwa wanawake haswa wasomi. Kuna majina maalumu utayakuta yako kila kona na katika kila teuzi. Ukiuliza ama utaambiwa unawivu au mtu mbaya hupendi maendeleo ya wengine.

  Vinginevyo utaambiwa eti tuu wao ni wanawake na wamesoma. Ukija kuchunguza wako wanawake wengine wamesoma na wanauwezo na uzoefu lakini hawana vigogo wa kupendekeza majina yao. Jamani kiongozi kutumia nafasi yake katika utumishi wa umma, kujinufaisha yeye na jamii yake ni ufisadi na umetokana na Katiba ya sasa inayomnyima mwananchi uhuru wa kuuliza na kuwawajibisha viongozi kwa kukiuka maadili. Hivi mbona Mwl Nyerere hakutumia na hakukubali watoto wake kupendelewa? Mbona hata hao watoto wa Nyerere wengi walikuwa na wanauwezo sana tuu lakini haya tunayoyaona sasa hayakuwepo wakati wa Mwal.? Tuache kuhalalisha uhuni kwasababu tuu unatufaidisha sisi na familia zetu.

  Kwasasa Kenya uteuzi wa cheo chochote kinachohusu taasisi ya umma, unachangiwa na kupitia mikono ya wananchi, bunge na rais. Hivyo wale wanaopendekezwa wanachujwa kila kona na kuna wengi walijitokeza ama kwa kupenda wenyewe ama kupendekezwa na wanaowaamini na kuchujwa vibaya ama vizuri.

  Sasa hivi wimbi la watu kujiuzuru kwa kushindwa vigezo ni kubwa mno. Sisemi hakuna uwezekano wa upendeleo katika mfumo ulioletwa na katiba mpya Kenya, upo ila ni vigumu sana na tumeona jinsi gani Wa-Kenya wamepata kiongozi mzuri kwenye taasisi yao ya kupambana na Rushwa. Uteuzi wa Dr PLO Lumumba ulikuja kabla ya kupitishwa Katiba Mpya Kenya.

  Hata hivyo tayari Kenya ilisha mnyang'anya rais mamlaka ya kuteua wakuu wa taasisi nyeti za uwajibikaji kama vile taasisi ya kupamba na rushwa. Hivyo ilichukua bunge la Kenya malumbano ya miezi kadhaa kukubaliana kumuajiri Dr Lumumba.

  Huyu Bwana ameanza kupambana na mafisadi papa na nyangumi kuanzia misamaha ya kodi; ajira za upendeleo; uwizi wa fedha za mifuko ya majimbo; ikiwagusa mawaziri; makatibu wa kuu; wakuu wa taasisi za umma. Lumumba ameweza kwasababu ajiri yake haifungani na upande wowote na hawajibiki kujikomba na kujipendekeza kwa wateule maana si mmoja mwenye mamlaka hayo tena.

  Naomba kuwasilisha
   
 20. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #20
  Jan 13, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,275
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Ndo mtindo wa mashirika mengi kwa sasa wanaajili on the basis of who knows who!
   
Loading...