Undugu wa kiafrica...naona bora marafiki tu!

idaz

JF-Expert Member
Sep 1, 2013
1,054
2,000
Ndugu wamekuwa ni sehem ya kuanzisha mifarakano isiyo na tija,kusemana na kusengenyana,inasikitisha saaana,naandika kwa majonzi sababu nimepitia hii situation this year:

Kuna ndugu wanaamini kwasababu wewe una ka ajira,ni haki yao kutimiziwa haja zao zote pasipo hata kujua unapata salary kiasi gani,ni kweli kama mwanafamilia,michango yenye tija,kama vile ada,matibabu na the likes,siko nyuma,frankly; per year ada tu nilizolipia madogo kama mchango wangu weka pembeni ya mwanangu ni around 1.5m, nimejitoa kwa kadri ya uwezo wangu sababu pia nina familia inayohitaji huduma na mimi ndiye baba;its so sad baadhi ya ndugu wanaungana tena ukiangalia kiuwezo,kuna wengine wao wako well off zaidi,wanakusema vibaya,kwamba mbahili,unaroho mbaya,mara hatumkubali jamaa,mara hivi mara vile but nimekuwa nikivumilia koz ndio ushakuwa kaka mkubwa,

Ukubwa jalala,kikubwa na kilichoniumiza zaidi,ni dogo ambaye tumepambana naye hadi kamaliza chuo ths yr pale UDSM,dogo kaja kukaa home,bila kinyongo,ni mdogo wangu,nikampokea huku anatafuta ajira,inaeleweka ajira sio rahisi,so kubebana ni kawaida,sasa ndugu zangu wengine,haswa wale wakike ndio wakawa wanamtumia dogo kupata kila info ya kinachoendelea home kwangu,walikuwa wakitaka kuongea na mwanangu kumsalimu,wanampigia wife then wife anawapa mtoto anaongea nao kwenye sim,lkn tangu dogo aje, wanampigia sim dogo wanamwambia tupe dogo tumsalimie,its ok, but not proper!

We ignored tht, maisha yakaendelea, next time..wife anakutana ma wifi msibani katika story,wanamwambia mbona bro hampi dogo nauli za mishe mishe zake?..wife akashangaa sana..akawauliza,dogo ameshawahi kumuomba bro wake pesa akamnyima? wife akawaambia,hata kama ndio hivyo,mbona hakuniambia mimi?..

Wife na mimi tumetoka kijiji kimoja anatufahamu wote na sisi tunawafahamu wote,nilishangaa,huyu namwita dogo lkn ni mtu mzima,graduate,kweeeli anashindwa kuni konfront kama bro na kuniomba pesa?,nikaja kujua sister huyo mwenye maneno,ndiye anayempa dogo pesa,ni sawa ni sister yake,ni haki yake,lkn mbona ananinaga?mbona dogo anaishi kwangu?mbona sijawahi kuuliza chochote?...sasa dogo kapata kazi mahali, anzia mwezi wa nane,frankly,sijui mshahara wake na hata sijawahi kumuuliza,hainihusu,sister kampa kitanda na vitu,kahamishia kwangu nadhan anajipanga ahame,nimempa nafasi aweke vitu vyake hata sijawahi kumuuliza anahama lini?...

Infact narud home late nakuta wamelala,dogo akawa anaachiwa msosi hali,wife akamwambia kama haji kula atoe taarifa mapema,sawa, ikawa hivo,sasa jana ndio kanichefua ile yenyewe,amekaa na wife na mtoto wangu na shemeji,dogo anawaambia,mi bro simpendi kabisa,yaani simkubali anzia tupo kijiji,ana roho mbaya sana,..wife akamuuliza kwanini unasema humpendi bro wako?kuna kitu amekukosea?...

Anajibu, damu zetu tu haziendani,anasema anamkubali sista na shemeji aliyemuoa sista..ilihali huyo sista ana uwezo na nyumba kubwa tu,aiseee,hii kitu imeniumiza sana,kwa namna nilivyo hustle nae na hawa madogo wengine walio chuo,amenikatisha tamaa ya undugu kabisa,na elimu yake yote!.....kweli ndugu sio lazima uzaliwe nae,hata rafik anaweza kuwa ndugu,nimempigia sim,kapokea ananiambia hawaruhusiwi kuongea na sim mda wa kazi,nikamwambia hana haja ya kuongea,anisikilize tu,jion akirudi,abebe kila kilicho chake,

Aende anapopajua,...hadi nimeandika huu uzi,nimeumizwa,na kuutoa moyoni,

Nimeshusha mzigo!
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
14,951
2,000
pole...anaweza akawa member wa JF..UJUMBE UTAKUWA UMEMFIKIA..Ila ungepunguza maamuzi ya hasira...Ungetumia ustaarabu katika uamuzi uliofikia ili dhamira imsute hata huko mbeleni..
jamaa yupo sahihi kabisa, fukuza kabisa huyo akajionee maisha yalivyo huko mbeleni
 

Patience123

JF-Expert Member
Mar 10, 2013
5,046
2,000
Ndugu wamekuwa ni sehem ya kuanzisha mifarakano isiyo na tija,kusemana na kusengenyana,inasikitisha saaana,naandika kwa majonzi sababu nimepitia hii situation this year:
Kuna ndugu wanaamini kwasababu wewe una ka ajira,ni haki yao kutimiziwa haja zao zote pasipo hata kujua unapata salary kiasi gani,ni kweli kama mwanafamilia,michango yenye tija,kama vile ada,matibabu na the likes,siko nyuma,frankly; per year ada tu nilizolipia madogo kama mchango wangu weka pembeni ya mwanangu ni around 1.5m,nimejitoa kwa kadri ya uwezo wangu sababu pia nina familia inayohitaji huduma na mimi ndiye baba;its so sad baadhi ya ndugu wanaungana tena ukiangalia kiuwezo,kuna wengine wao wako well off zaidi,wanakusema vibaya,kwamba mbahili,unaroho mbaya,mara hatumkubali jamaa,mara hivi mara vile but nimekuwa nikivumilia koz ndio ushakuwa kaka mkubwa,ukubwa jalala,kikubwa na kilichoniumiza zaidi,ni dogo ambaye tumepambana naye hadi kamaliza chuo ths yr pale UDSM,dogo kaja kukaa home,bila kinyongo,ni mdogo wangu,nikampokea huku anatafuta ajira,inaeleweka ajira sio rahisi,so kubebana ni kawaida,sasa ndugu zangu wengine,haswa wale wakike ndio wakawa wanamtumia dogo kupata kila info ya kinachoendelea home kwangu,walikuwa wakitaka kuongea na mwanangu kumsalimu,wanampigia wife then wife anawapa mtoto anaongea nao kwenye sim,lkn tangu dogo aje,wanampigia sim dogo wanamwambia tupe dogo tumsalimie,its ok, but not proper!
We ignored tht,maisha yakaendelea, next time..wife anakutana ma wifi msibani katika story,wanamwambia mbona bro hampi dogo nauli za mishe mishe zake?..wife akashangaa sana..akawauliza,dogo ameshawahi kumuomba bro wake pesa akamnyima?wife akawaambia,hata kama ndio hivyo,mbona hakuniambia mimi?..wife na mimi tumetoka kijiji kimoja anatufahamu wote na sisi tunawafahamu wote,nilishangaa,huyu namwita dogo lkn ni mtu mzima,graduate,kweeeli anashindwa kuni konfront kama bro na kuniomba pesa?,nikaja kujua sister huyo mwenye maneno,ndiye anayempa dogo pesa,ni sawa ni sister yake,ni haki yake,lkn mbona ananinaga?mbona dogo anaishi kwangu?mbona sijawahi kuuliza chochote?...sasa dogo kapata kazi mahali, anzia mwezi wa nane,frankly,sijui mshahara wake na hata sijawahi kumuuliza,hainihusu,sister kampa kitanda na vitu,kahamishia kwangu nadhan anajipanga ahame,nimempa nafasi aweke vitu vyake hata sijawahi kumuuliza anahama lini?...infact narud home late nakuta wamelala,dogo akawa anaachiwa msosi hali,wife akamwambia kama haji kula atoe taarifa mapema,sawa, ikawa hivo,sasa jana ndio kanichefua ile yenyewe,amekaa na wife na mtoto wangu na shemeji,dogo anawaambia,mi bro simpendi kabisa,yaani simkubali anzia tupo kijiji,ana roho mbaya sana,..wife akamuuliza kwanini unasema humpendi bro wako?kuna kitu amekukosea?...anajibu,damu zetu tu haziendani,anasema anamkubali sista na shemeji aliyemuoa sista..ilihali huyo sista ana uwezo na nyumba kubwa tu,aiseee,hii kitu imeniumiza sana,kwa namna nilivyo hustle nae na hawa madogo wengine walio chuo,amenikatisha tamaa ya undugu kabisa,na elimu yake yote!.....kweli ndugu sio lazima uzaliwe nae,hata rafik anaweza kuwa ndugu,nimempigia sim,kapokea ananiambia hawaruhusiwi kuongea na sim mda wa kazi,nikamwambia hana haja ya kuongea,anisikilize tu,jion akirudi,abebe kila kilicho chake,aende anapopajua,...hadi nimeandika huu uzi,nimeumizwa,na kuutoa moyoni,nimeshusha mzigo!
Pole sana,ndugu wanakatisha tamaa sana,

Mimi nimejifunza kuishi kama ninavyotaka mimi,na sio kama wanavyotaka wao,na ninajiskia amani.
 

Patience123

JF-Expert Member
Mar 10, 2013
5,046
2,000
pole...anaweza akawa member wa JF..UJUMBE UTAKUWA UMEMFIKIA..Ila ungepunguza maamuzi ya hasira...Ungetumia ustaarabu katika uamuzi uliofikia ili dhamira imsute hata huko mbeleni..
Amfukuze tu,siku hizi kum host ndugu imekuwa kama kubeba gunia la misumari,ni lawama tu kwa kweli.

Kila mmoja akae kwake mkutane kwa hamu ndio heshima itapatikana.
 

kijani11

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
7,027
2,000
Pole sana mkuu. Kikubwa hakutegemei tena umefanya sehemu yako kwa hilo pongezi.
 

Tyta

JF-Expert Member
May 21, 2011
12,774
2,000
jamaa yupo sahihi kabisa, fukuza kabisa huyo akajionee maisha yalivyo huko mbeleni
Zingatia story ni ya upande mmoja,pengine ukipata upande wa pili unaweza kuta zipo sababu ama chanzo cha msingi kinachoweza mfanya mleta mada naye kuwa sehemu ya tatizo.Approach yake katika kumfukuza mdogo wake haikuwa nzuri.
 

Stayfar

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
929
1,000
Du inaonekana jamaa umeumia sana.Pole ila jua kwamba huyo bado ni ndugu yako na huwezi kutengua jambo hilo,ikiwa mlitoka kwa Mama au Baba mmoja,

Na pia tambua kwamba haya mambo yapo kwenye familia nyingi tu!.Cha muhimu ni kuchukua hatua stahiki kama ulivyoamua,msaidie kupata mahali ajitegemee na ipo siku atakumbuka wema uliyomtendea,inawezekana ni utoto unaokolezwa na Dada yako.
 

Tyta

JF-Expert Member
May 21, 2011
12,774
2,000
Amfukuze tu,siku hizi kum host ndugu imekuwa kama kubeba gunia la misumari,ni lawama tu kwa kweli.
Kila mmoja akae kwake mkutane kwa hamu ndio heshima itapatikana.
Kumfukuza ni jambo moja(ambalo sina tatizo nalo)..appraoch aliyotumia ni jambo lingine (ambayo binafsi siiungi mkono)...
wakati mwingine maamuzi yanayoambatana na hasira hata kama una hoja ya msingi yanaweza yasiwe mazuri(during and aftermath)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom