Underground Politics Zimeleta Umeme? Wananchi Million 43 Hawausishwi Wala Kuulizwa Wana-Solutions | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Underground Politics Zimeleta Umeme? Wananchi Million 43 Hawausishwi Wala Kuulizwa Wana-Solutions

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by niweze, Mar 29, 2011.

 1. n

  niweze JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Utafikiri Watanzania wote hatuna majibu ya matatizo tulionayo. Hii serikali siku zote ina-assume sisi sote watanzania tunataka umaskini wakati nafasi ya kujadili policies zetu na future ya Taifa letu hatupewi. Hili swala la umeme limekuwa kimya kwa sasa (kama matatizo mengine ya maji, elimu na uchumi) na ukiangalia hii serikali inachokifanya kama kawaida yao, wanakaa vikao vya nyuma ya nyumba ya Rostam, Ngereja na January kujadili wampe nani hii deal ili awe tajiri kama wao. Hii ni policy ya watanzania? Watanzania wangapi wanapenda solutions za matatizo zizungumziwe nyuma nyuma bila transparency? Kinachotakiwa katika democracy yoyote ile ni public hearings (citizens involvements) ambazo kila mtanzania apate kuchangia hoja na hasa wale walio na professionals katika haya maswala.

  Siku zote njia za kuzuaia rushwa na wizi ni kuweka system ya transparency. Hii njia imetumika nchi nyingi na ndio chanzo cha maendeleo sehemu nyingi. Mfano ni ukusanyaji wa kodi kunatakiwa system ya wazi na clear documentations za kuzuia kufichwa au kukwepa kwa walipa kodi, utaratibu wa kupata vibali vya biashara (viwanda na biashara ndogo ndogo). Siwezi kuamini kwamba hizi taratibu zinashindikana kuanzishwa nchini. Swali ni kwamba kitu gani kinawazuia ccm miaka 50 kuanzisha hii mifumo kama sio kulindana na kuwaibia Watanzania? Haya yote yanadhibitisha mipango ya ccm kuzuia democratic reforms (including Katiba), waweze kupata fedha ku-fund hiki chama cha ccm. Leo wanauliza Chadema wanapata wapi funds wakati wao wazi wanawaibia watanzania.

  Nchi kama Marekani na Uingereza, wananchi wamejifunza na kuona hizi njia za demokrasia na mpaka sasa tunaona nchi zao na hizi nyingine kama South Korea zinazidi kutuacha mbali. Tukizungumiza the fall of financial institutions na the collapse of housing industry in US, kuna mengi ya kuijifunza na wenzetu wananchi wa hizi nchi wanapambana na haya majanga yao. Mikakati ipo wapi Tanzania? Tunacho kiona ni ccm kujifanya wao wanamajibu ya kila kitu na kuwanyamazisha wananchi kila wakati (Chadema wanawapa majina na kusingizia wanataka kuchafua amani). Hii kama sio dharau na discrimination ni nini? Tuangalie hii healthcare debate in US, tutaona jinsi gani wananchi wanahusishwa kuleta solutions
  Energy & Environment | The White House  Kama hizi nchi zinaweza kufanya hizi discussions na ku-dialog kupata policies kwa nini havifanyiki Tanzania? Kitu gani Kikwete na viongozi wa serikali yake wanatafuta nje ya nchi kama hawajifunzi wanavyoviona?

  Siasa ni platform ya Wananchi kujadili na kutatua matatizo ya nchi​
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...