Unazikumbuka hizi hadithi?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,204
12,695
Utii wa Roda


Mama yumo nyumbani, anapika chakula chetu.
Roda yuko nje, anacheza na wenzi wake. Sasa
mama anamwita Roda aje kumsaidia.
— Roda, njoo hapa.
— Ndiyo mama.
Lakini haji. Anacheza na wenzi wake. Mama ana-
mwita tena :
— Roda, njoo ; ukapasue kuni.
— Ndiyo mama, nakuja sasa hivi.
Lakini haji.
— Roda, nakuita, je husikii
— Ndiyo mama, nakuja.
Lakini hata sasa haji. Anaendelea kucheza mchezo
wake.
— Je, Roda, utakuja ama huji ?
— Naja mama, sasa hivi.
Lakini bado anakawia. Anasema ndiyo, utii hakuna. Mama anaona vibaya, anakasirika.
— Basi, sasa nitakupiga, Roda.
— Usinipge mama !
Nimekwisha kuja sasa.
— Sasa umechelewa.
Si mtoto mwema we.

Huna utii.

1628320519064.png
 
Habari ya sungura

Siku moja sungura alikwenda kula majani matamu
katika shamba la watu. Shamba lile lilikuwa lime-
jaa mimea ya kila namna, hasa michipukizi ya
miharagwe, minyanya, na ya mdewere. Baba yake
mzee akamwambia: Usiende kula mdewere leo.
Nimemwona mwenyewe anatembeatembea sha-
mbani. Ukila chochote atakuua.
Sungura akajibu : Hii si kitu. Hataweza kuniua
mimi. Nikimwona nitakwenda zangu mbio, nitaJi-
ficha. Najua mirm.
Baba yake akasema : Mimi mzee, wewe mtoto.
Akili ya nani? Kabla hujamwona umekwisha kufa.
Lakini sungura hakutaka kusikiliza. Alipenda
mno kula mdewere. Akaenda shambani, akala yote
aliyoweza. Matamu kabisa ! Mara akamwona mtu
mmoja bunduki mkononi. Sungura akajisemea :
Sasa mbio ! Sitaki kufa mimi : mbio nyumbani !
Lakini mtu yule akalenga, akapiga bunduki, risasi
ikampata sungura. Akafa.
Kosa lake mwenyewe. Sungura yule alikuwa
mjinga. Hasikii maneno ya baba.

1628320901410.png
 
Hadithi ya ngamia aliyekuwa mvivu



Hapo zamani za kale dunia ilikuwa bado mpya
kabisa. Iliwapasa wanyama wote kufanya kazi nyingi
ili waitengeneze sawa sawa, iwe mahali pazuri pa
kukaa. Farasi akafanya kazi nyingi kabisa ; na
ng’ombe pia, na mbwa, na punda, na ndovu
kadhalika. lla ngamia peke yake hakufanya kazi
yo yote. Alikuwa akipiga uvivu kutwa kucha,
akijitenga mbali na wanyama wengine, na kula
majani jangwani katika upweke.
Wanyama wengine hawakupenda uvivu wake
hata kidogo, kwa maana kazi yao ikazidi, wakanuna.
Mwisho wakamwendea ngamia yule kumwuliza
sababu ya kupiga uvivu yeye peke yake, asifanye
kazi yoyote, dunia ikiwa bado mpya kabisa. Lakini
yeye mkorofi ; kila anapoulizwa hujibu : Nunduuu!
Wala hajibu kitu kingine, wasijue tena la kusema:
Kila mara wao wakimwuliza, yeye hujibu : Nunduuu ! Halafu huwacheka.
Hata mwisho wakachoka. Wakaenda kwa mchawi mkuu wa jangwani, wakamwuliza :
Je, ni haki ngamia yule kupiga uvivu siku zote, Sisi tukifanya
kazi kwa kuwa dunia ni bado mpya kabisa

Akajibu : Si haki kata kidogo.
Wakasema : Basi, umwambie wewe afanye kazi,
kwa sababu Sisi tukimwambia anatucheka tu ; anajibu : nundu, nundu. Hasemi neno jingine. Mchawi akafikiri kidogo, halafu akachukua
mumunye na uvumbi wa dunia mpya, akaenda
zake kumtafuta ngamia yule aliyekuwa mvivu.
Akamkuta jangwani peke yake, akila manyasi ya
nyikani, akiangalia uso wake katika kidimbwi. Kwakuwa ngamia si mvivu tu, lakini ana majivuno vilevile.
Mchawi akamwuliza : Je, bwana ngamia, nasikia nini juu yako, kwamba hutaki kufanya kazi yoyote, hata siku hizi kama dunia ni mpya kabisa
bado

Ngamia akajibu : Nunduuuu !
Mchawi akasema : Nadhani ni afadhali usiseme nundu kila mara. Neno hili litakudhuru. Sasa nataka kujua kama utakwenda kazini sasa hivi, au
kama unakataa

Ngamia akasema : Nunduuu !
Hapo mchawi mkuu wa jangwani akachukuamumunye lake pamoja na uvumbi wa dunia mpya akaanza kucheza na uchawi wake. Na bwana
ngamia akazidi kujiangalia katika kidimbwi, akijifurahisha moyo kwa ajili ya uzuri wake. Ndivyo alivyofanya ukorofi wa kumchokoza mchawi yule.

Lakini alipokuwa akijitazama hivi katika maji ya kidimbwi, akaona kwamba mgongo wake ulianza kuvimba kwa ajili ya uchawi ule. Mgongo wake ukavimba, ukavimba, hata mwisho ukawa nundu kweli kweli. Akajaribu kuiondoa asiweze.

Akanung'unika kwa mchawi, akasema : Sasa umeniharibu kabisa. Sitaweza kufanya kazi yoyote namna hii. Lakini mchawi akajibu : Utaweza
tu. Itakufaa kwa chakula cha akiba, utumie wakati wa kufanya kazi jangwani. Na usipofanya haraka ya kwenda kazini sasa hivi, nitaharibu kichwa chako vile vile.

Ndiyo maana ngamia ana nundu siku hizi, na
kazi anaifanya kwa shida tu, bila kupenda. Na
iwapo anafanya, hana haraka.

1628321462769.png
 
Hadithi ya Mjane mwenye mali

Hapo zamani za kale palikuwa na mwanamke
mmoja, mjane mwenye mali nyingi sana. Alikuwa
tajiri mno. Mavazi yake alikuwa akivaa hariri siku
zote. Vyombo vyake vilikuwa vya fedha, kama
vijiko, uma, vijaluba, mabuli, midila, vyote vya
fdha; na hata bawaba za milango zilikuwa za
fedha vile vile. Na marembo ambayo huzoea kujipamba nayo, hata siwezi kuyataja. 'Mikufu, mafurungu, bangili, vikuku, vipini, vipuli, pete, yote ya
dhahabu tupu ; tena yametiwa malulu na almasi.
Mwanamke yule ukikutana naye njiani utafikiri
umekutana na Jua, Jinsi anavyong'ara na kumetameta kwa aiili ya marembo. Na asili ya utajiri
wake biashara. Ana merikebu nyingi zenye kusafiri nchi za mbali.
Basi, Siku moja aliona merikebu yake moja imerudi katika bandari ya mji. Mara akaenda kuonana
na nahodha wake, apate kujua ameletewa faida gani.
Akamwuliza . je, umeleta nini toka nchi za
kigeni
Nahodha akajibu : Sikuona bidhaa nzuri za kuleta kuliko ngano. Merikebu yote nimeijaza nafaka.
Hapo mwanamke yule alikasirika sana. Akapiga
Kelele, akasema: Nafaka? Una wazimu we? Nafaka
itanifaa nini? Umeingiza shehena upande gani
Akajibu : Upande wa kushoto.
Akasema : Basi, kaitupilie baharini upande wa
kuume. Watu wote waliokuwapo wakaona uchungu kwa
ajili ya amri hii. Wakasikitika juu ya ratili nyingi
za chakula kutupwa baharini. Hata mzee mmoja
wa mji akajaribu kumwonya mjane yule, akamwa-
mbia : Ama huwezi kufikiri kwamba Bwana Mungu
atakasirika labda kwa jambo baya kama hili la
kutupa vyakula baharini? Huogopi kwamba atakunyanganya mali yako yote, ukawa fukara na
maskini
Lakini mwanamke yule akazidi ukorofi wake,
akavua pete ya almasi aliyokuwa amevaa kidoleni,
akaitupa baharini pia, akasema : Ikiwezekana pete
hii ya almasi kurudi nyumbani kwangu ikiisha
zama katika mawimbi, basi, hapo nitajua kwamba
naweza kuwa maskini mimi !
Watu wote wakashtuka walipoona majivuno
makubwa hayo, wakanyamaa. Nafaka yote ika-
tupwa baharini ikatoswa.

Lakini siku ya pili yake mtumishi wa mjane
yule tajiri akaenda sokoni kununua samaki. Akarudi nyumbani amenunua samaki mkubwa na
mzuri. Alipoanza kumtumbulia, mara akaona kitu
tumboni kinametameta. Akakitwaa, kumbe, ndiyo
pete ile ile ya almasi, mali ya memsahib yake.
Ndivyo ile pete ilivyomrudia mwenyewe, tena
ikawa adhabu yake. Maana tangu siku ile biashara
yake ikaharibika, akapata hasara na hasara tena.
Baada ya mwaka mmoja mali yote ikampotea,
mwisho akawa maskini kabisa. Na katika umaskini
huo akafariki dunia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom