Unayopaswa kuyafahamu kuhusu Filamu mpya ijayo ya James Bond.Mtz Lupita ndani!

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,824
9,521
Mambo muhimu unayofaa kuyafahamu kuhusu filamu pendwa mpya ni pamoja na haya:-

1. Lupita Nyong'o mtanzania kutoka pale jijini Mwanza ni miongoni mwa watakaokuwemo kwenye filamu ijayo ya James Bond.

2. Muongozaji wa filamu hiyo ijayo wa awali dingilai Danny Boyle alijitoa kuongoza filamu hiyo kutokana na kile alichoeleza kuwa ni tofauti za kitaalamu...hivyo akaingia muongozaji mpya kijana Cary Joji Fukunaga ambae ndie anaongoza filamu hiyo tunayoisubiri kwa hamu 'the Bond 25' .

3. Mbabe wa Filamu za Bond Daniel Craig anarudi tena baada ya mafanikio kwenye filamu yake ya aina hii ya hapo awali the Spectre au 'Mzimu' kwa kizaramo.

4. James Bond ya sasa itakuwa tofauti kidogo na zile zilizopita za akina 007...Safari hii movie itaanza kwa Bond kuishi huko Visiwa vya Caribbean,na hatakuwa tena yule Jasusi James Bond ambae anafanya kazi za usalama na kijasusi kwa niaba ya kasli la Malkia...atakuja na mission/kisa tofauti na ile ya kutetea maslahi ya London beibe!

5. Bond ijayo itasadifu mazingira ya Matera, Italia, jijni London na Norway...huko Caribean itakuwa by the way tu.

6. James Bond ijayo inatarajiwa itaitwa 'ECLIPSE' yaani 'Kupatwa' kama inavyokuwa kupatwa kwa Jua,Mwezi nk...

7. Inayumkinika kwamba filamu hii itakuwa ndio ya mwisho kwa mbabe Daniel Craig kucheza filamu za Bond baada ya hapo atasakwa Bond mpya kuendeleza kisasili cha Bond.

8. Aidha kumekuwa na 'fununu' kwamba huenda kwenye filamu hii ya ECLIPSE au Bond 25 kama inavyotambulishwa James Bond, the 007,Womaniser,Shaken not stirred ATAKUFA mwishoni mwa filamu huku wadadisi wakihoji akifaa? itakuwaje kwa filamu zijazo...kisa kitaishia hapoo?

9. Pamoja na wasiwasi kwamba kwenye Bond ya sasa Starring atauawa inadhaniwa kwamba kwenye James Bond ya 26 Bond atafufuliwa kwa kufanya 'Regeneration'.

10. Na mwisho; Yule demu maarufu ambae ilikuwa lazima atoke na Bond ilipangwa awe Lupita Nyong'o Mtanzania maarufu huko Hollywood kutoka jijini Mwanza, lakini nasikia mpango huko umepigwa kumbo na wanafigisu wa hapo Califonia "ni wivu tu; ni wivu tu!"

By N'yadikwa
 
Huyu jamaa ndie muongozaji mpya wa James Bond 25 ijayo baada ya mdingi kujitoa
GettyImages-1032852656-adfe546.jpg
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom