Unayakumbuka mabasi na daladala za kwenu siku za nyuma? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unayakumbuka mabasi na daladala za kwenu siku za nyuma?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Kiranja Mkuu, Oct 25, 2011.

 1. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwetu Mbeya kulikuwa na daladala (Mzunguko) mmoja unaitwa Mafegi, huo ulikuwa ni noma. Rangi nzuri, mziki mnene, kitu kipyaaaaa, haukudumu, ulichomwa moto na washindani wake.
  Kulikuwa na Mwailubi, Mgangaluma, Green Belt la kina Bisso Ntepa, Black Belt, Linolino la kina Makorija, Usafiri Milimani la kina Mwaigomole, Slow but sure la kina Billey Massawe. Hili lilikuwa ni bedford, likisukumwa Mlima wa Ghana linaenda kuwakia mteremko wa Mbeya Hotel.
  Hebu na wewe tujulishe ya kwenu
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwa njia ndefu kulikuwa na
  Nyota likipiga safari za Mbeya Dar,
  Okoa, Mbeya Dar,
  Tunyande- Mbeya,Lusaka Dar,
  Movement Star- Mbeya Dar, dereva alikuwa Henry Mwantobe.
  Amina (Aluta Continua)- Dar Mbeya
  Safina- Dar Mbeya
  Matema Beach- Dar Mbeya
  Tawaqal Dar Mbeya, kuna moja lilikuwa linaendeshwa na Giriki, jamaa alikuwa noma sana.
   
 3. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Pia kulikuwa na Tahfif, wali moto mchuzi moto, hii ilikuwa inapiga Mbeya Mombasa.
  Zainabs na Scandnavia zilikuwa ni Dar Mby.
  Victoria ilikuwa inaondoka Mby kwenda Iringa kila siku saa saba mchana.
   
 4. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwacha, Kamata na Relwe yalikuwa lazima yalale njiani kutoka Mby kwenda Dar
   
 5. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Mwenzetu hujaenda kwenu una muda gani?
   
 6. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,088
  Trophy Points: 280
  Pale Bk yalikuwepo Byonabusha,Zafanana,Salima na nduguze,Bujugo trans n.k
   
 7. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Pale iringa kulukuwa na daladala inaitwa vitu laini ilikuwa inapiga root ya Mwangata kihesa kilolo, pia kulikuwa na na mabasi ya Kwacha ilula iringa, Mwafrika Njombe iringa na idodi iringa, kulikuwa na basi la tarafa ya kalenga lilikuwa linaitwa UTAKA (usafiri tarafa ya kalenga) nakumbuka mbali sana.
   
 8. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kwetu kulikuwa na baiskeli nyingi zote aina moja SWALA nauli 200 kijiji to kijiji
   
 9. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nasikia mwenye mabasi ya Zafanana alikuwa na wanawake wengi sana wa aina tofautitofauti akiitafuta k tamu kuliko zote. Mwisho wa siku akagundua kuwa zote Zafanana
   
 10. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,120
  Likes Received: 6,603
  Trophy Points: 280
  Kweli wewe ni kiranjamkuu, heshima mbele mkuu.
   
 11. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kule MOSHI yalikua black nyau, blach mamba, sirori hethina horomire, dadadala zilikua hazima majina zenyewe zilikua zinashikiliwa gia na manati usipoweka manati gia inafyetuka.
   
 12. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu kuna moja pale mbeya lilikuwa linaitwa kichaa kapewa rungu,mwenye hilo daladala alikuwa anaitwa mfikemo,nililipenda sana enzi hizo
   
 13. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Atown kulikuwa na kiford kinaitwa take-uch.moshi arusha coster inaitwa TOP STORY,injili iende mbele,mwaka mpya,wacha waseme na machame safari
   
 14. sunshine1

  sunshine1 JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2011
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 523
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  kwetu kulikuwa na TTBS, Harambee, kindo kya Kombe n.k   
 15. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,641
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  kwenye red...hili basi lilipata ajali mbaya sana miaka hiyo likauwa wat wengi....lilikuwa gumzo sana, ngoja nivute kumbukumbu ajali ilitokea mto gani na barabara gani
   
 16. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,641
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Sio Leyland DAF na Bedford mkuu...zilikuwa na shepu ya mkate
   
 17. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  lol! JF!!
   
Loading...