Unawezaje kutenganisha uozo wa chama na mwenyekiti wake kama siyo usanii mtupu!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unawezaje kutenganisha uozo wa chama na mwenyekiti wake kama siyo usanii mtupu!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dumelambegu, Apr 24, 2011.

 1. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Dear JF members,

  Watanzania kwa mara nyingine tena, tumeendelea kupumbazwa na usanii wa hali ya juu unaosanifiwa na kutekelezwa na Chama Cha Magamba maarufu kwa kifupi kama ccm. Baadhi ya wananchi wameanza kuamini kuwa sasa ccm imezaliwa upya. Hayo ni mafanikio makubwa ya usanii uliofanywa na jopo la wataalam koko mmojawapo akiwa Prof. Mkandala wa UDSM. Walichotaka 'wataalam' hao siyo kukinusuru chama directly bali ni kumnusuru M/Kiti wa Chama kwani hali ilikuwa inaendelea kuwa mbaya siku hadi siku. Walijua kuwa ukimnusuru M'kiti automatically utakuwa umenusuru chama.

  Leo hii akina Nnape wanazunguka huko na huko wakidai kuwa magamba (mafisadi) walikuwa wanamchafua M'kiti wao na chama kwa ujumla. Sasa imefika wakati wanatakiwa wakae pembeni. Hivi ni nani katika nchi hii asiyejua kuwa fedha za mafisadi ndizo zilizowezesha rais wa sasa kufika ikulu?! Ni nani asiyejua katika nchi hii kuwa ndani ya kipindi alichoongoza kikwete chama chake kimekuwa na minyukano ya ndani isiyoisha tena hadharani kabisa. Ni nani asiyejua katika nchi hii kuwa ndani ya uongozi wa kikwete lugha ya taarabu ya watu kama akina makamba na tambwe hiza imeshamiri kuliko wakati wowote mwingine!!?

  Kama hivyo ndivyo, tunawezaje kumtenganisha kikwete na magamba yanayodaiwa kuvuliwa ndani ya chama kama huo siyo usanii wa waziwazi?
   
Loading...