Unawezaje kupata wazo la biashara lenye faida?

Lazaro Samwel

Member
Apr 27, 2019
33
26
Hili ni moja ya swali kubwa mbalo limekuwa likiulizwa na watu wengi kwamba watawezaje kupata wazo la biashara lenye faida katika maisha yao?

Haswa kwa wengi huliuliza kwakuwa wanataka mafanikio ya haraka katika maisha yao ndio maana wanakazania “KUPATA WAZO LENYE FAIDA.”

Sio hivyo tuu lakini pia kwasababu wengi tumelelewa katika mazingira ya kuangalia lenye faida basi wazo lenye hasara tumekuwa hatuoni umuhimu wake kwasababu tunadhani ndiyo mwisho wake.

Nisikupeleke mbali sana lengo ni kuweza kukufundisha namna ya kupata wazo bora la biashara.

Kwanza kabisaa hakikisha katika akili yako unaondoa mafunzo yote ambayo umeshawahi kuyapata juu ya wazo la biashara na kuwa makini na hiki nikufundishacho.

Unapoambiwa Wazo Bora kwanza kabisa nini ambacho kinakuja katika akili yako?

Wengi wataishia kusema kwamba ni wazo ambalo linakuingizia hela nyingi basi au wazo ambalo litafanya upate faida kubwa utakapolifanyia kazi,hakuna kosa lolote katika kuwaza hili japo umeruka hatua muhimu sana kabla ya kuanza kuona hizi faida na mauzo makubwa.

Nikwambie tu kwa kifupi kwamba WAZO BORA LA BIASHARA hupimwa kwa utatuzi uliopo ndani yake na walengwa wa utatuzi ndani ya wazo lenyewe tofauti na hapo wazo lako haliwezi kuwa bora.

Sasa wazo lako unawezaje kujua ni BORA? Let us put it in a simple way, ukitaka kujua ubora wa jembe na kisu unaangalia nini?

Najua wewe utasema ni makali, sawa unaweza kuwa sahihi kwa asilimia flani lakini ubora wake hupimwa kwa utatuzi ndani ya jukumu la jembe na kisu kwa makali yake.

Wazo Bora La Biashara Haliji Kwa Kufanya Kitu Kipya Kabisa Katika Maisha Yako, Ila Linakuja Kwa Kufanya Vitu Hivi;

Wazo lako bora linaweza kuja kwa kuongeza kitu ambacho hukuwa nacho katika wazo ambalo tayari ulishaanza kulifanyia kazi.

Wazo bora la biashara linaweza kuja kwa kuangalia makosa ya washindani katika soko ambalo unaona unapaswa kuingia na bidhaa au huduma yako.

Wazo bora la biashara linaweza kuja kwa kuamisha wazo la biashara katika eneo lako ukizingatia wazo hilo halikuwepo.

Hapa usilete wazo lako sawa na ulipolitoa, hakikisha kwamba wazo lako unaliwekea chochote kile kipya au cha ubunifu kutengeneza picha yako katika biashara yako.

Wazo lako bora la biashara linaweza kuja kwa kujifunza ujuzi flani ambao unaona kuna nafasi katika soko mfano kwa upande wangu nimejikita kwenye kusaidia wafanyabiashara na wajasiriamali kuwapa elimu ya mauzo na utafuta wa masoko.

Wazo bora la biashara unaweza lipata kwa kuangalia kitu ambacho wengi wanachukia kukifanya lakini kina umuhimu kwao mfano sio kila mmoja anapenda kuwa mzoa takataka lakini kuna umuhimu wa kila mmoja kuzoa takataka.

Ni Muhimu Sana Kuweza Kuhakikisha Kwamba Katika Wazo Lolote Linalokuja Katika Akili Yako Kwanza Kabisa Unajiuliza Maswali Haya;

Wazo hili linautatuzi gani?

Kwasababu gani nilichague lenyewe kulifanyia kazi kati ya mawazo mengi niliyonayo?

Wazo hili linawalenga watu gani?

Kwasababu gani watu hawa wanalengwa na wazo hili?

Ni gharama gani ambazo zitahitajika katika kuhakikisha wazo hili linafanyiwa kazi?

Kuna ushindani wowote katika wazo ambalo ninalo katika soko husika?

Wazo hili litahitaji utofauti gani katika soko tofauti na washindani kusudi liweze kuwa bora zaidi?

Haya ni maswali ambayo yatakusaidia sana kuweza kuwa na wazo lenye faida tofauti na ukiamua kuanza kufanyia kazi wazo ulilokuwa nalo kibiashara.

Nataka nikusaidia kitu kingine ambacho kitakusaidia sana wazo lako liweze kuwa na faida,haswa kwa wale ambao unakuta kwamba wameshachagua wazo flani katika mawazo mengi waliyokuwa nayo lakini bado hawajua wataanzaje kufanyia kazi wazo lao.

Unapochagua Wazo Moja Kulifanyia Kazi Na Ukawa Hujua Unatakiwa Ufanye Nini;

Fanya uchunguzi zaidi juu ya wazo lako.Hakikisha unalielewa wazo lako vizuri kwa ndani na nje bila kusita,hapa itakujenga ujasiri wa kuweza kuwasilisha wazo lako kwa watu tofauti bila uwoga.

Tafuta mentor au mshauri ambaye unaona atajitosheleza kutokana na wazo ulilonalo. Mtu ambaye anaweza kukupa mwongozo kwa mawazo ambayo unayo.

Jitolee kuomba kufanya kazi katika kampuni au taasisi ambazo unaona kuna kitu utajifunza kwa maslahi ya wazo lako.

Anza kuangalia ni aina gani ya marafiki ambao utawahitaji katika wazo lako kwasababu kila kitu mwenyewe hutaweza.

Chunguza washindani wako sokoni, angalia utendaji wao wa kazi angalia bidhaa au huduma zao na jiulize unaona kitu gani ambacho kimepungua katika huduma au bidhaa zao kusudi wewe uweze kukiongeza katika huduma au bidhaa yako.

Kwa ujumla nikusitize kitu kimoja ambacho ni wachache sana huwa wanaambiwa na bado hawatilii maanani kitu ambacho kinawafanya washindwe kunufaika na wazo la biashara ambalo unakuta wanalo.

Kwapamoja Kuweza Kukusaidia Zaidi, Kuna Maswali 6 Ambayo Ni Muhimu Sana Kuhakikisha Kwamba Kwa Kila Wazo La Biashara Unalopata Unahakikisha Kwamba Unayajibu Bila Shaka;

Unawazo gani la biashara?

Kwanini umeamua kuchagua wazo hilo? Yaani umeona gap/mwanya gani au tatizo gani kiasi kwamba ukaona wazo lako litafaa?

Hapo hapo Unatakiwa kueleza umewalenga wakina nani na kwasababu gani kwa wazo lako?

Wazo lako litakugharimu shilingi ngapi mpaka kuhakikisha linaanza kufanya kazi?

Utauzaje bidhaa zako? Utatumia mbinu gani za mauzo na usambazaji wa huduma zako?

Utategemea kuingiza shilingi ngapi katika biashara yako kila siku,kwa wiki,mwezi na mwaka?

Mfumo wako wa malipo utakuwaje pia kusudi uweze kujua utabakiwa na sh ngapi kama utaajiri watu?

Nikukumbushe tuu kitu kimoja,kwa sasa kuanzisha biashara sio shida tena,shida ipo kwenye upande wa kuendeleza biashara yako,na ukweli ni kwamba maendeleo ya biashara yako yanategemea sana MAUZO.

Ikiwa sasa utapenda kupata mafunzo ambayo yatakusaidia kujua namna ya kuongeza mauzo ya biashara yako kuanzia kwenye mitandao ya kijamii na nje ya mitandao ya kijamii basi hakikisha unawasiliana nami kwa namba hizi 0753616584 / 0678010334

Lazaro Samwel
Author-10 Books | Sales And Marketing Expert | Professional Copywriter
#akiliyaushindiView attachment UNAWEZAJE KUPATA WAZO LA BIASHARA LENYE FAIDA.pdf
 
Back
Top Bottom