Unawezaje kumwambia rafiki yako ajirekebishe jambo fulani pasipo kuikwaza nafsi yake? Mfano kinywa chake hakipo katika hali nzuri siku hiyo

Unachukua ulichokiandika hapa, unakiweka kama status kwenye Whatsapp una post...





Cc: mahondaw
Unamaanisha niandike hivi "Unawezaje kumwambia swahiba/rafiki yako ajirekebishe jambo fulani pasipo kuikwaza nafsi yake? Mfano kinywa chake hakipo katika hali nzuri siku hiyo" katika status yangu ili nimfikishie ujumbe indirectly. Au sio mkuu?
 
Kama mimi juzi kati hapa naitwa na mzee fulani Kanisani ananiambia Bwana mdogo nakupenda sana lakini utanisamehe kama nitakukwazwa, Akaanza kwa kuniambia kuna Padri mmoja alipandishwa cheo SAUT Mwanza, Hivyo kwa hadhi ya cheo kile ilibidi hata life style nayo ibadilike kulingana na cheo chake hivyo aliambiwa mavazi,gari na vitu vingine lazima vibadilike atake-asitake na ikawa hivyo.

Sasa kesi yangu inaelekea huko nimechaguliwa kanisani kuwa nakaribisha watu na huwa sipigi machomeko, tai n.k, kwahiyo aliniona kama kibaka fulani hivi(hahahaha), akaniambia unakaribisha watu wakubwa hivyo jitahidi kufanyia ushauri wangu kazi huku akirudia utanisamehe kama nimekukwaza.

Though naamini kila mtu ana definition yake ya smartness, yangu imejikita zaidi katika utulivu wa akili haijalishi machomeko wala tai lakini mind yako inakuwa huru kulingana na dressing code yako, kikubwa hauvunji sheria.
Maeneo ya kanisani watu huamini sana kuwa kuchomekea ndio ishara njema ya mtu aliyestaarabika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom