Unawezaje kumwambia swahiba/rafiki yako ajirekebishe jambo fulani pasipo kuikwaza nafsi yake? Mfano kinywa chake hakipo katika hali nzuri siku hiyo

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari za wakati huu ndugu zangu wote wa humu jamiiforums.

Unawezaje kumwambia swahiba/rafiki yako ajirekebishe jambo fulani pasipo kuikwaza nafsi yake? Mfano kinywa chake hakipo katika hali nzuri siku hiyo.

Sote tunajua ya kwamba watu wakishakuwa marafiki wa karibu walioshibana inakuwaga ngumu sana kumwambia mtu ule ukweli mchungu wa kiingereza wanaita "a bitter truth". Kuna urafiki kama urafiki na pia kuna urafiki ule uliokomaa sana na unakaribia kuwa undugu sasa.

Achilia mbali urafiki wa kukutana tu barabarani, unakuta mtu ni rafiki yako tangia darasa la kwanza mpaka unafika miaka 30 bado mmeshibana. Kwa mfano chukulia siku moja unakutana na mwana kama mimi Soldier maeneo ya posta huko Dar.

Baada ya kukutana alafu katika kupiga piga story mbili tatu ukagundua kuwa mzee baba Soja leo kinywa chake hakipo katika hali nzuri kabisa labda kwa sababu alikuwa anawahi misele alfajiri akaamua kupiga mswaki bila dawa au kutokupiga kabisa. Je, utamwambiaje ili asikwazike nafsini mwake?

Lengo ni kuwa asikwazike nafsini mwake na ajirekebishe kwa maana huko mbeleni anapoelekea (labda ndani ya daladala) ataenda kukutana na watu baki asiowafahamu kisha akaaibika.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Marafiki wengi ni wanafki, japo umetoa mfano hafifu kwenye suala nyeti. Chukulia wanajua mkeo analiwa na hawakwambii eti wanaepusha shari!
Sio wanafiki inategemea na asilimia za urafiki wenu.

Unakuta mtu mmekutana kazini since day one,huo ni mwaka wa 10 mko pamoja,hata shemeji yako akijua umemuona sehemu lazimaa aanze kujieleza kwako.

Ila huu urafiki wa kukutana bar na mabanda ya mpira, haiwezekani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom