Unawezaje kumfanya mpenzi wako awe na Exposure?

chugaa

Member
Nov 6, 2020
80
99
Wasalaam JF,

Kuna binti nimetokea kuwa naye kwenye uhusiano miaka miwili sasa. Nampenda jinsi alivyotulia mpole , mstaarabu ,mcha Mungu na asivyo na tamaa hana makuu. Tatizo Academic exposure yake ipo chini sana , sizungumzii ile exposure ya Kidimbwi na Juliana.

Kifupi huyu binti amesoma na kukulia kijijini kwao huko mkoani. Ni mwanamke mchapa kazi sana , Yeye jembe twende kila kitu twende . Ukimkuta kapendeza na kazi anazopiga huwezi kuamini. Sio mwanamke anayependa U'slay queen hata kidogo. Elimu yake ni form four ila kuna short courses flani alisomea. Na mimi Elimu yangu ni Degree.

Nimevutiwa na baadhi ya tabia zake mpaka sasa natamani nimuoe. Ni mtu anayenifanya nijihisi na amani hana yale mapicha picha.
Kwa sasa nimekaa naye kwangu kama mwaka hivi. Hana dalili zote za kunitia mashaka.

Tatizo alilonalo ni mtu mvivu wa kujifunza vitu na exposure ya masuala tu ya kawaida ya kijamii na Shuleni. Yaani mpaka sa nyingine napata tabu! Vitu vingi vya shule vya Academic vingi amesahau mpaka inshanagaza . Imefika hatua nawaza kumuacha nitafute mtu mwingine!!! Ila roho nyingine inaniambia kazana naye.

Je, naweza kumbadilisha vp awe na exposure maana alisoma huko kijijini kwenye shule za kata labda ndo maana ufahamu wake ni mdogo hivi? Naweza vp nikamnoa akili yake?
 
Akishakuwa hivi 👇baadaye utakuja kulia lia amebadilika🐒
IMG_20211024_103120.png
 
Jamaa niliyezaa nae mtoto wa kwanza ambaye nishawahi simulia alinibana sana nitoe mimba ya huyu my firstborn...alinikuta nina kaz tayari,nafuga kuku kienyeji nalima sana...kuna siku nakumbuka akamuuliza mshkaji wake aliyekuja nae kwangu sikuhiyo,"sijui nioe huyu" sikujua maana yake lakin kumbe tupo wengi.

Akaniacha na maumivu na mimba kususiwa juu.....mpaka sasa mwanangu ana wadogo watatu waliyeshea baba....alioa wa degree mwenzie wakazaa wakashindwana,akazalisha mwingine wakashindwana,ndo nasikia Kaka saloonist ambaye nae sana mtoto mmoja.mwanangu ana 5 years ana wadogo 4 pamoja na huyu wangu.Hivyo kupanga ni kuchagua...utavuna ukitakacho.
 
Jamaa niliyezaa nae mtoto wa kwanza ambaye nishawahi simulia alinibana sana nitoe mimba ya huyu my firstborn...alinikuta nina kaz tayari,nafuga kuku kienyeji nalima sana...kuna siku nakumbuka akamuuliza mshkaji wake aliyekuja nae kwangu sikuhiyo,"sijui nioe huyu" sikujua maana yake lakin kumbe tupo wengi.Akaniacha na maumivu na mimba kususiwa juu.....mpaka sasa mwanangu ana wadogo watatu waliyeshea baba....alioa wa degree mwenzie wakazaa wakashindwana,akazalisha mwingine wakashindwana,ndo nasikia Kaka saloonist ambaye nae sana mtoto mmoja.mwanangu ana 5 years ana wadogo 4 pamoja na huyu wangu.Hivyo kupanga ni kuchagua...utavuna ukitakacho.
Poleee sana dada yangu, Huyu mwenzako nampenda ila ni mvivu wa kujifunza vitu. Hata vipindi vya TV yeye ni muziki na movie tu, Hataki hata kuangalia vipindi akajifunza kitu.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom