KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 18,894
- 36,211
Habari za wakati huu...poleni na mfungo...
Rafiki yangu wa karibu amepatwa na mkasa huu au niseme mtihani huu kwenye maisha yake.....Rafiki yangu huyu aliangukia katika penzi la mwanadada mmoja mrembo.....waliyekutana huko maeneo ya Posta ambapo huyo rafiki yangu anajishughulisha na kusafisha magari maeneo ya karibu na ofisi anayofanyia kazi mwanadada huyo......katika miaka miwili ya mahusiano yao wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume........lakini kilio chao kikubwa kipindi chote cha mahusiano yao ilikuwa ni ndoa.....jamaa yangu kutokana na maisha yake ya kubangaiza akaona hatoweza kumudu gharama za kumtunza mke ambaye kwa muonekano tu anaonekana ni mtu wa gharama....
Vile vile hakuwa tayari kuishi na mwanamke ambaye amemdhidi kipato kwani kwake yeye maisha hayo huambatana na masimango ambayo yeye asingeyamudu.......lakini maisha ya kimahusiano baina yao yaliendelea chini ya ahadi za kuwa nitakuoa mwaka ujao huku siku izikikatika......
Sasa siku za hivi karibuni huyo shemeji yangu huyo amesema amepata mchumba ambaye yupo tayari kumuoa siku za hivi karibuni......lakini shemeji huyo anamuambia hataki waishie kwenye uadui kwa kuwa wameshazaa na mtoto anahitaji uangalizi wa wazazi.....na ili kulidhihirisha hilo ameombwa asikose kuhudhuria sherehe hizo za harusi.....
Mpaka dakika hii amechanganywa na masuala yote mawili lakini la kutomuoa alimuumizi sana kwa kuwa anakiri kuwa bado hana uwezo huo hata akipewa miaka kumi zaidi ya maandalizi.....lakini la kumtaka ahudhurie harusi na kushuhudia mwanamke wake kipenzi akijikabidhi kwa mwanamume mwingine hawezi kuvumilia kulitazama mbele ya macho yake.....
Je wewe ungeweza?