Unawezaje kuhimili lawama mbalimbali kutoka kwa ndugu?

Nina mke na watoto wawili wote wanasoma.. Asante mungu suala la kodi ya nyumba nimeliepuka...

Baba mzazi na ndugu zangu (kaka wakubwa wawili, mdogo wangu wa kike mmoja) wote choka mbaya....

Baba mgonjwa wa moyo, mwaka jana nilimtibu kwa 8mil pale JK bila msaada mwingine wowote kwa ndugu....

Nalisha familia yangu binafsi, nalisha familia ya baba maana ni mgonjwa tu na hafanyi tena biashara zake, kaka zangu wote watu wa vijiweni, huyu wa kike ndo kama vile beki 3(mungu aepushe asipatie mimba na ngoma akiwa palepale home)

Kila mwezi, mzee lazima ahudhulie clinic yake pale JK (apo 350k ya dawa ni pie)

Lazima nitume ela ya matumizi ya mwezi mzima pale nyumbani, namlipa mfanyakazi wa pale kwa mzee,

KITUKO SASA!!
January hii pamoja na msalaba wote hu nlionao, kuna shangazi mmoja eti ananiomba nimuongezee laki 2 atoe mchango wa harusi na ashone sare... Tusi nililompa naamini mpaka sasa bado analitafakari!!! mxiiiiuuu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu lawama mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna maisha ya ndugu zako,kuna maisha yako,na kuna maisha ya watoto wako;unatakiwa ujue kuyatofautisha.
 
Back
Top Bottom