Unawezaje kuhimili lawama mbalimbali kutoka kwa ndugu?

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Kama mnavyojua maisha hayana formula kuna wengine kwa kiasi chake mwenyezi Mungu amewabariki na kuwapa maisha mazuri Kiasi cha kuweza kutoa msaada kidogo kwa ndugu pale shida inapojitokeza,

Vijana wenzangu ambao mko njiani kutafuta maisha je kile kidogo unachopata unawezaje kuhimili lawama kutoka kwa ndugu zako pale wanapoitaji na kukosa msaada kutoka kwako?

Kama mnavyojua wengi wetu sisi tunaotokea kwenye familia za kiafrica tumezaliwa kwenye familia tegemezi kwani Mungu akikujalia kuuona mwanga kidogo wa mafanikio ya maisha basi na ndugu nao wanakutazama.

Ni kweli kuna wakati wa lazima kutoa msaada lakini siyo kila wakati ni wakutoa msaada .

Cc Zero IQ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lawama katika Maisha haziepukiki hata ufanye nn,kuna watu Pamoja na kupewa uhai bado wanamlaumu Mungu kwann aliwaumba kwann aliruhusu wakazaliwa hivyo binadamu mm na ww Ngumu sana kuepuka lawama, kuhusu issue ya kusaidia saidia kadri ya uwezo wako na pale unapoona pana ulazima wa kufanya hivyo.. Sio jitu halitaki kufanya Kazi kwa makusudi kabisa hata Kama Kazi ya kufanya ipo ila linaamua tu kuwa omba omba.. My friend Live your life

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani kuna ndugu yangu mmoja hajui hata kama huna yeye anajua kila siku tu unaamipesaa kisa mfanyakazi

Kinachonishangaza ndugu wa damu hawasumbui kama wale ndugu wa mbalimbali sijui inakuwaje hiii?

Kiukweli ni shida sana inabidi ujikaushe tu hakuna namna.

Sent using Jamii Forums mobile app
Cha kufanya,
1. Epuka kutoa hela kwa anayekuomba mara tu baada ya kukuomba... Subiri kwa muda au piga piga kalenda...unless otherwise tatizo liwe linauwa
2. Epuka kutoa msaada kwa ndugu wa aina moja... Yaani siyo kwa vile ni wa kuzaliwa tumbo moja basi unadhani unatakiwa kuwapa msaada
3. Wakati mwingine, hata kama unazo usitoe, jenga mazingira ya kuwa huwa unakosa
4. Usihofie kutumia hela zako kwa matatizo yako kisa kuna mtu umemwambia huna hela...
5. Shirikisha ndugu wengine unapoombwa msaada na mtu.. Kujifanya unamsaidia kwa siri kutakuja kukupa shida siku za mbele
6. Siku nyingine WEWE walilie shida hata kama huna shida hiyo...nao wajue kuwa huwa unaishiwa... Watakaokupa ndo hapo nawe utawasaidie watakapokulilia shida
 
Lawama katika Maisha haziepukiki hata ufanye nn,kuna watu Pamoja na kupewa uhai bado wanamlaumu Mungu kwann aliwaumba kwann aliruhusu wakazaliwa hivyo binadamu mm na ww Ngumu sana kuepuka lawama, kuhusu issue ya kusaidia saidia kadri ya uwezo wako na pale unapoona pana ulazima wa kufanya hivyo.. Sio jitu halitaki kufanya Kazi kwa makusudi kabisa hata Kama Kazi ya kufanya ipo ila linaamua tu kuwa omba omba.. My friend Live your life

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hii ID yako kuna kijiji ukiwa unaenda gairo kiko upande wa kulia ni kweli?
 
Cha kufanya,
1. Epuka kutoa hela kwa anayekuomba mara tu baada ya kukuomba... Subiri kwa muda au piga piga kalenda...unless otherwise tatizo liwe linauwa
2. Epuka kutoa msaada kwa ndugu wa aina moja... Yaani siyo kwa vile ni wa kuzaliwa tumbo moja basi unadhani unatakiwa kuwapa msaada
3. Wakati mwingine, hata kama unazo usitoe, jenga mazingira ya kuwa huwa unakosa
4. Usihofie kutumia hela zako kwa matatizo yako kisa kuna mtu umemwambia huna hela...
5. Shirikisha ndugu wengine unapoombwa msaada na mtu.. Kujifanya unamsaidia kwa siri kutakuja kukupa shida siku za mbele
6. Siku nyingine WEWE walilie shida hata kama huna shida hiyo...nao wajue kuwa huwa unaishiwa... Watakaokupa ndo hapo nawe utawasaidie watakapokulilia shida
Bonge la kitu.
Salute mkuu n thanks for your brave advice

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Choyo choyo choyo choyo.ubinafsi na umimi watu kama hawa pengine wao walilelewa na ndugu kwa heshima zote.ukiwa na uwezo toa huna kaa kimya.
 
Kweli muda mwingine ina kera sana suala la kuombwa pesa. Kabla hujalaumu fanya jiulize kwa nn wanaokuomba wasimuombe mwingine isipo kuwa wewe ?? Tunafunzwa mali kuweka mikononi ili tuweze kutoa sana kwa ndugu na asie ndugu japo n binadamu mwenye uhitaji kuwa mkwel na muwazi tu... Ukiwa nacho toa na ukikwama basi weka wazi hakuna mtakae sumbuana
 
Maada kutoka Zero IQ na haihusu pochi mayoya ila pochi nyingine! Ni kweli ukiishi duniani utaona mengi! Vipi baada ya kupigwa buti asubuhi subuhi, uko salama, mkuu????
 
Back
Top Bottom