Unawezaje kuamrisha watendaji wa kivuko cha MV Nyerere wachukuliwe hatua kali wakati walitoa tahadhari kuwa kivuko hicho kibovu hawakusikilizwa?

Injini iliyofungwa ilitaarifiwa ingekiwezesha kivuko kusafiri kwa dakika 45. Lakini hilo halijawahi kufanikiwa, kwani kivuko kilikuwa kinaenda mwendo wa saa 1:30 kuendelea.

Naamini, ukarabati huo, ama haukukamilika, au injini ilikuwa mtumba kama kivuko cha bagamoyo, na pia waliopakia abiria hawakuzingatia uwezo wa kivuko.
 
Kwa utawala huu,
Usishangae kabisa yule mbunge kukamatwa na kuulizwa kwa nini pesa ya jimbo hajaipeleka kwenye Kivuko.
Wee tulia utaona movie lote
serikali ilishakarabati kivuko, shida ni kubeba mzigo mkubwa kuliko uwezo wa kivuko chenyewe! acheni kupotosha.
 
Kabla hamjaanzisha mada muwe mnafanya research. Kivuko kilishatengenezwa tayari baada ya huyo mbunge kufikisha hoja bungeni. Halafu kile kivuko kimeandikwa kabisa idadi ni watu 100, lakini angalia hadi sasa ni maiti ngapi zimeopolewa, ongeza na wale majeruhi je kilipakia idadi inayoruhusiwa? Hapo bado hujaangalia mizigo na magari yaliyokuwemo. Acheni siasa kwenye vitu vya msingi. Serikali unayoiponda ndiyo serikali iliyoona kuwa hoja ya mbunge wa Chadema ni ya msingi na ikaifanyia kazi kwa kufunga injini mbili mpya. Sasa watu wamefanya uzembe mnataka wasichukuliwe hatua kali, acheni upuuzi.
nyumbu ni wapumbavu wa kutupwa.
 
Habari kubwa inayotrend ndani ya nchi yetu hivi sasa na nje ya nchi ni kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere kilichokuwa kikifanya safari zake huko Ukerewe katika ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watanzania wasio na hatia zaidi ya 130

Tumemsikia Rais wetu Magufuli kama kawaida yake akiagiza kwa ukali kabisa, hatua Kali zichukuliwe kwa wote waliohusika na uzembe huo hadi kusababisha maafa hayo makubwa kwa nchi yetu

Lakini pia kuna clip moja inayotrend humu mtandaoni kwa hivi sasa ikimuonyesha Mbunge wa Ukerewe kwa tiketi ya Chadema, Joseph Makundi, akilalamika wakati huo Bungeni kuwa kivuko cha MV Nyerere ni kibovu na akaendelea kueleza kuwa aliwasiliana na Waziri wa uchukuzi kwa kipindi kirefu kumweleza tatizo hilo lakini hajasikilizwa, akaendelea kueleza kuwa au ndiyo inasubiriwa kizame kivuko hicho ndiyo waje hapo Bungeni kuchangishana pesa ya rambirambi? Mwisho wa kunukuu

Na kweli hivi sasa utabiri huo umetimia kwa kivuko hicho kuzama na kama alivyoeleza Mheshimiwa Mbunge huyo kuwa sasa ndiyo tuko "busy" kuchangishana pesa ya rambirambi!

Hebu tujiulize kama Taifa ni kweli tunatoa kipaumbele katika vitu vya muhimu kwa Taifa letu?

Au ndiyo tunatoa kipaumbele katika vitu anavyohitaji Mheshimiwa "Mfalme" vipewe kipaumbele?

Hapo ndipo tulipofika kama Taifa, wapo watu watakuwa "victimized" katika tukio hili wakati UKWELI unajulikana kuwa kama Taifa tumeachana na kutoa kipaumbele katika vitu ambavyo kama Taifa tunapaswa kuvipa kipaumbele

RIP wote waliokumbwa na mkasa wa kuzama kwa MV Nyerere huko ziwa Victoria
Rais alishasema kuwa hapeleki fedha "zake" kwenye majimbo ya upinzani
 
Siasa za kuwaona wapinzani hawana jema wanaloweza kulisema na kulitenda ndizo zilizochukua roho za watanzania wenzetu,mhe mbunge angesikilizwa tusingefika mahali tulipofikia,kwa kuwa aliyesema ni mpinzani pamoja na kwamba alikuwa na hoja nzuri lakini hoja yake ikafanyiwa kazi kipinzani.

Hata boss mwenyewe kwa kuwa nayeye anaendesha nchi kipinzanikipinzani katoa amri kwa wahusika wa ngazi ya chini washughulikiwe badala ya kutoa mfano kwa kumshughulikia wazri wake kwa kuwa alikuwa na taarifa ya ubovu kamuacha waziri salama kawashughulikia vidagaa wakati kunauwezekano mkubwa kuwa wao ndio waliotoa taarifa kwa mbunge wao ambaye naye alizipeleka bungeni zikapuuziwa na waziri wake kwa kuwa zimepelekwa na mbunge wa upinzani wakati taarifa ya mbunge ulikuwa ni ushahidi tosha wa kumuajibisha waziri wale.
 
hivi nyie chadema akili zenu zikoje? nimegundua ndio maana huwa mnakamatwa kwa uchochezi, mbona hamsemi kuwa watu walijaa kuzidi uwezo wa kivuko? serikali ilikarabati hicho kivuko kwa kuweka injini mpya halafu bado mnataka kumlaumu Mh rais.
 
Mystery, umenena vema, kama mbunge alisema hawakumsikiliza, iweje leo unataka watendaji wa kivuko wachukuliwe hatua za kinidhamu ?, Kuna Viongozi walioko juu ya wale watendaji wa kivuko, Kuna Sumatra, Kuna Jeshi la Majini, na sasa waziri mwenye dhamana na wizara hiyo, lakini pili waziri mkuu, wote hawa yapaswa wafukuzwe mara moja, sio kuwatoa kafara wasimamizi wa kivuko, Magufuli ameamuru zitumike Tshs Billion 41 kujenga uwanja wa ndege kule chato (nyumbani kwao),
Uwanja ambao kuna taarifa unaweza usije kufanya kazi yake effectively, pesa hizo zingeweza kuokoa maisha ya hawa watu.
Kweli Mkuu, hicho ndicho nilichomaanisha kuwa "agizo" la Mkuu wa nchi la kuwachukulia hatua watendaji litachukuliwa ndivyo sivyo.....

Wapo Sumatra, lipo Jeshi la majini waliopaswa kuchukua hatua za kuokoa maisha ya watanzania wenzetu, je kila chombo husika kilichukua hatua za dhati za kuokoa maisha ya wahanga??
 
Ni kweli kabisa Mheshimiwa Mbunge alitoa tahadhari kubwa, lakini wakubwa wakaamua "wakaziba" masikio!
Mbna naskia kimefanyiwa matengenezo July n kufungwa injin mpya mbili.ni uzembe wa Sumatra na watendaji sio kosa la mheshimiwa rais
 
Mpumbavu wewe na vichaa wenzio, mpaka sasa waziri wa uchukuzi alitakiwa awe ameisha achia ngazi ila kwakuwa ni mshikaji wa kichaa wenu atadunda tu
aachie kwa lipi? subiri majibu yatatoka, mbwembwe zenu za kutafuta huruma hazina nafasi.
 
Mbunge wenu wa chadema anajua fika kuwa swali lake lilijibiwa kwa vitendo...injini mpya mbili zilifungwa...kwa hiyo hoja yako haina connection
 
Wachukuliwe hatua kali sana chombo kilikua kizima na engine ni mpya zili fungwa juzi tu,
 
Mystery, umenena vema, kama mbunge alisema hawakumsikiliza, iweje leo unataka watendaji wa kivuko wachukuliwe hatua za kinidhamu ?, Kuna Viongozi walioko juu ya wale watendaji wa kivuko, Kuna Sumatra, Kuna Jeshi la Majini, na sasa waziri mwenye dhamana na wizara hiyo, lakini pili waziri mkuu, wote hawa yapaswa wafukuzwe mara moja, sio kuwatoa kafara wasimamizi wa kivuko, Magufuli ameamuru zitumike Tshs Billion 41 kujenga uwanja wa ndege kule chato (nyumbani kwao),
Uwanja ambao kuna taarifa unaweza usije kufanya kazi yake effectively, pesa hizo zingeweza kuokoa maisha ya hawa watu.
Siasa Mbaya sana
 
Habari kubwa inayotrend ndani ya nchi yetu hivi sasa na nje ya nchi ni kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere kilichokuwa kikifanya safari zake huko Ukerewe katika ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watanzania wasio na hatia zaidi ya 130

Tumemsikia Rais wetu Magufuli kama kawaida yake akiagiza kwa ukali kabisa, hatua Kali zichukuliwe kwa wote waliohusika na uzembe huo hadi kusababisha maafa hayo makubwa kwa nchi yetu

Lakini pia kuna clip moja inayotrend humu mtandaoni kwa hivi sasa ikimuonyesha Mbunge wa Ukerewe kwa tiketi ya Chadema, Joseph Makundi, akilalamika wakati huo Bungeni kuwa kivuko cha MV Nyerere ni kibovu na akaendelea kueleza kuwa aliwasiliana na Waziri wa uchukuzi kwa kipindi kirefu kumweleza tatizo hilo lakini hajasikilizwa, akaendelea kueleza kuwa au ndiyo inasubiriwa kizame kivuko hicho ndiyo waje hapo Bungeni kuchangishana pesa ya rambirambi? Mwisho wa kunukuu

Na kweli hivi sasa utabiri huo umetimia kwa kivuko hicho kuzama na kama alivyoeleza Mheshimiwa Mbunge huyo kuwa sasa ndiyo tuko "busy" kuchangishana pesa ya rambirambi!

Hebu tujiulize kama Taifa ni kweli tunatoa kipaumbele katika vitu vya muhimu kwa Taifa letu?

Au ndiyo tunatoa kipaumbele katika vitu anavyohitaji Mheshimiwa "Mfalme" vipewe kipaumbele?

Hapo ndipo tulipofika kama Taifa, wapo watu watakuwa "victimized" katika tukio hili wakati UKWELI unajulikana kuwa kama Taifa tumeachana na kutoa kipaumbele katika vitu ambavyo kama Taifa tunapaswa kuvipa kipaumbele

RIP wote waliokumbwa na mkasa wa kuzama kwa MV Nyerere huko ziwa Victoria
Dah.. acha uzwazwa..post ndefu umeijaza ujinga tu...ubovu si sababu ya kuzama kwa kivuko....tuliza macalio ujifunze labda utaacha kuandika ujinga ujinga
 
Back
Top Bottom