Unawezaje kuamrisha watendaji wa kivuko cha MV Nyerere wachukuliwe hatua kali wakati walitoa tahadhari kuwa kivuko hicho kibovu hawakusikilizwa?

Acha miemko ya kuchochea usichokifahamu. Kivuko kinapaswa kubeba watu *101* na Mpaka sasa Miili iliyoopolewa *209* Watu waliookolewa Hai *41* Jumla *250* lakini siyo hakika kama wameisha Ama lah!!
Mungu ibariki Tanzania Mungu Awafariji Ndugu, Jamaa na Marafiki Waliyowapoteza Wapendwa wao_
Sasa ryana fan unaongea nini mbona sikuelewi ?, unaunga hoja au unapinga ?, kuwa muungwana, kipi hapo kinahusisha kuchochea ?, nyie wafia Lumumba huwa mnapenda kujitoa akili, naamini una ufahamu mzuri ila inapofika serikali yenu kusemwa akili zenu zinaondoka, namshukuru Nape kwani aliwahi kukiri hadaharani kwamba Hali ilikuwa tete mwaka 2015 wakati wa kampeni za uchagu na iliwalazimu wawe kama wehu
 
Umenena vema Smilling Killer, na awamu hii tutasikia mengi ya ajabu ajabu sana, najiuliza tu, hivi kwa nini hajaenda huko Ukara kwenye tatizo, au kwa sababu jimbohilo liko chini ya mbunge wa Upinzani, na bora asiende, kwani najua angeenda angeishia kutoa matamshi ya kejeli na kashfa kwa wahanga kama alivyofanya Bukoba.
Huyo Jiwe hawezi kwenda kwenye msiba unaohusisha maafa ya watu wengi.....

Hebu jiulize ni kwanini hakwenda kwenye msiba wa tetemeko la ardhi Bukoba??

Jiulize pia ni kwanini hajaenda kwenye msiba wa wale mabinti wa Lucky Vincent's??

Hayo ndiyo miongoni ya masharti ya mganga wake!
 
Huyo Jiwe hawezi kwenda kwenye msiba unaohusisha maafa ya watu wengi.....

Hebu jiulize ni kwanini hakwenda kwenye msiba wa tetemeko la ardhi Bukoba??

Jiulize pia ni kwanini hajaenda kwenye msiba wa wale mabinti wa Lucky Vincent's??

Hayo ndiyo miongoni ya masharti ya mganga wake!
Kinachonifurahisha mimi ni baada ya kusikia kwamba ameambiwa maafa haya ya |Mv Nyerere na mengine ya aina hiyo yana connection na yeye binafsi, na hii ni nzuri kwani itamfanyaa ajihoji kila anapotaka kufanya jambo au kwenda mahali popote, ana spirit ya mauaji kwenye nafsi yake.
 
Chadema bhana wanaweza kukuambia hata kivuko cha waenda kwa miguu kilikuwa ni kibovu.
 
Ujinga mwingine ni kudhani kivuko kingekuwa kipya kisingepinduka kwa kuzidisha abria na mizigo
 
Mbunge alilalamika na malalamiko yake yakasikilizwa injini mbili zilinunuliwa, na ushahidi upo, ipo video inayotembea mitandaoni.

Tatizo pia ni uzembe wa hao wafanyakazi wa hiyo meli, waliambiwa na abiria mbona magari ni mengi na mizigo ni mingi, wakawaambia abiria msitupangie kazi!!, Upuuzi ule ule wa kitanzania, ujuaji usio na kichwa wala miguu.
 
Mkuu unapoamua kumtumia Mungu inabidi uwe mkweli wa nafsi maana Mungu hadanganyiki.

Watu 50,000 walitajwa bungeni na mbunge wa eneo husika. Sijui nani mkweli kati ya wewe na mh. Mkundi.

Pili kuhusu hotuba ya mwl. Nyerere alikuwa anaongelea suala la ukabila kwenye chaguzi na si suala la idadi na wala hakutaja idadi yao. Pia zingatia ni lini aliyasema hayo. Hata kama walikuwa wachache wakati huo unadhani bado ni ileile?

Je, umesikia idadi ya wakazi wa vijiji viwili vya Bwisya ilosemwa na msemaji wa serikali leo? Amesema watu 16,000. Ukara ina vijiji vingapi ili ubishi vizuri?

Pia kivuko kilikuwa kinafanya safari kati ya Ukara na Bugolola, je umejaribu kujiuliza idadi ya watu upande wa pili?

Swali dogo la ufahamu, unadhani Kituo cha Ubungo kinahudumia wakazi wa ubungo tu ama Kinondoni tu ama Dar es Salaam tu?

Wewe msukuma acha dhihaka, hata kama hujaguswa kwa namna yoyote acha kuwaliza waliofkkwa na msiba. Hata wewe yaweza kukukuta ya maji. Au umesahau ajali ya Manonga? Watu waliokuwa kwenye basi walifia majini.

Tumuogope Mungu
Tuseme ukweli kijiji hakina gari hata moja, majeneza yanabebwa kwa bodaboda, tizama clip hakuna barabara, imebidi wapeleke bulldozer kwenye uokozi badala ya crane, hata hilo dozer imebidi lianze kukwangua miti lipate pa kuegeshwa. Mie naona hiki kisiwa sasa kipewe uangalizi wa pekee ikiwezekana kiwe wilaya na kipate mbunge wake.
 
Back
Top Bottom