Uchaguzi 2020 Unaweza usiaminiI CHADEMA kusumbua sana uchaguzi mkuu 2020 kuibuka kidedea

daza steven

JF-Expert Member
Aug 30, 2016
359
357
Pamoja kuwa chama kikuu cha upanzani kiko katika hari mbaya sana kwa sasa ni kama mtu anapumulia mashine ya ugonjwa wa Korona katika chumba cha wagonjwa mauti uti lakini kinahistoria za ajabu kuibuka kidedea au kukimbiza dakika za majerui.
Chadema kimepita katika misukosuko mikubwa huko nyuma na kuonyesha historia ya kuvuka bila mtu kuelewa au kuamini. Ukianzia kipindi cha Marehemu Chacha Wangwe yule aliyekuwa anautaka uwenyekiti wa chadema alileta mtikisiko mzito wakati ule lakini chama kilivuka salama salmini.

Zito Kabwe na Kitila mkumbo pia nao walileta hekaheka sana ndani ya chama wakati ule Kitila mkumbo alimdanganya Zito kuwa agombee uenyekiti wa Chadema hari ilikuwa tete walifukuzwa wote lakini chama kilivuka salama Act wazalendo ikazaliwa.

Kuondoka kwa Dr. Slaa ambae alikuwa kama injini ya chama na mbeba maono na kuonyesha njia zakupita ambaye aliaminika sana, alileta sintofaamu tena ilikuwa kuelekea katika uchaguzi mkuu ambapo katika short run hakuonekana kuleta madhara makubwa na Chadema ilipita salama na kuwa cha kikuu cha upinzani Tanzania.

Hakuna mtu aliyetegemea kuwa uchaguzi wa 2015 Chadema ingepata wabunge wengi na madiwani kwani uchaguzi wa 2015 Chadema ilimvuta Mwanasiasa nguli Tanzania Edward Lowasa na wenzake na heka heka ilikuwa ya kufa mtu wakitembea mwendo wa mabadiliko na kuzungusha mikono na chama kikuu cha upinzani tunacho hadi sasa.

Wengi tunategemea Chadema kuonyesha maajabu mengine katika uchaguzi mkuu 2020 labda itamvuta Tundu Lisu, au Benald Membe au Freemani mwenyewe kuwa mgombea urais au chochote kile kwani ndiyo kawaida ya Chadema kufanya maajabu.

Lakini kuanzia 2015 hadi leo naandika Chadema ni kama imekutana na kisiki cha Mpingo ambacho kimeng'oa kucha zote katika mguu ambapo kimeleta maumivu makali sana lakini aliyeumia anafukutia ndani kwa ndani haya maumivu na akiulizwa kama ameumia au apatiwe msaada anasema hajaumia kabisa sasa hili pia ni jambo la ajabu sana.

Kinachoonyesha kwa sasa JPM amewapiga pini kali sana yaani kama uwanjani kipindi cha pili dakika ya 85 bao ni 9 bila, na nusu ya wachezaji wa Chadema wamekula kadi nyekundu yaani wanacheza nusu na bado ni wabishi wanaingia hadi katika box kupitia winga ya Korona na kulokudouni.

Wadadisi wa mambo ya siasa wasema kuwa Chadema inapita katika kipindi kigumu sana ambacho haijawai tokea tangia kuaziswa kwa chama hicho na wameenda mbali zaidi na kusema kama hawakuchua hatua za makusudi wanaweza kuanguka na kupotea vibaya kuliko hata CUF na NCCR Mageuzi ambapo vilifulia taratibu.

Zile ngome za Chadema kwa sasa si ngome tena labda kwingine kwani kusema unazitegemea kwa sasa hazipo kama Kilimanjaro, Mara, Mbeya na Mwanza kwani si ngome kwa sasa zimebomoka pakubwa na ujenzi wake unaitaji gharama kubwa si kwakusema zimenunuliwa.

Na JPM inasemekana ni Rais ambaye anauruma sana hata kama ujaomba msamaa uwa anasamehe lakini kwa upande wa Chadema ndiyo anazidi kupigilia misumali hadi misumali ya nchi 6 kichwani sasa atapona mtu kweli sijui?

Wadadavuaji wa mambo ya michezo ya siasa wanasema Mchezaji huyu wa CCM DKT John Pombe ambaye anajua michezo mingi hata ile ya bungasiliga yaani ukiweka ugoko anatupia jiwe la kilo 50 mguuni.

Tusubiri maajabu.
 
SIIPENDI CCM ILA KWA HALI NINAYOIONA KWA UPINZANI ITAWACHUKUA MIAKA 20 AU 30 IJAYO KUKAMATA NCHI
 
Chadema hoi inapumulia mashine!
CA0D7C19-7533-432A-AE0B-F0C204028469.jpeg
 
Kwa chadema ya mbowe labda, ngoja tuone mda utaongea tuu.

Kwani mgombea ni nani CDM?
 
Haiwez kutokea ...! CCM inajielewa sn kuliko kawaida..! Ni taasisi inayojua inachokifanya unlike vyama vingine...! Angalia Raisi wetu anayoyafanya unadhan tuna muda na vyama pinzani no way!!! CCM tutaendelea kutawala mpk mwisho wa tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo CCM haipo vizuri kihivyo lakini Ni Bora kuliko upinzani uliopo sasa vyama vya upinzani vya Tanzania havina vision sasa sijui ikulu wanataka kwenda kufanya Nini? Vyama vyao tu havina demokrasia sasa hiyo demokrasia wanayotaka ya Nini?
 
Kusema ukweli chadema iko kwenye hali mbaya sana,kilichowaponza ni tabia yao ya kupinga kila kitu hata kwenye mambo yenye tija kwa taifa.Ambacho hawakielewi unapompinga Rais Magufuli unawapinga Watanzania mil 50+ kitu ambacho hutakuwa salama kisiasa.Kazi aliyoifanya Rais Magufuli ni kubwa sana kwa watanzania hasa wanyonge.Nani asiyejua dhuluma zilizokuwa zinafanyika kipindi cha nyuma?Mtu unanunua kiwanja leo baada ya mwezi unakuta mwenye pesa zake kajenga ghorofa ukifuatilia huambulii kitu zaidi ya kutishiwa kuuawa,haya mambo awamu hii hayapo ndugu.Huo ni mfano mdogo tu ukiacha mambo mengi ambayo Rais ameyafanya ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu,SGR, ununuzi wa ndege,barabara,mwl Nyerere stiegler's-HEP,elimu bure na mengine mengi.Hayo yote ukiyapinga watanzania watakuona chizi tu hata wasipokwambia,adhabu yake utaiona baadaye.Kwenye uchaguzi wa mwaka huu chadema isitegemee kitu hata kama wasimamishe wagombea kumi kwa ngazi ya urais,wakipata wabunge watatu wakatambikie.
 
Cha muhimu ccm watuoneshe zile Mil 50 kila kijiji pia watuoneshe na viwanda elfu 4 wakivyojenga hapo ccm watashinda kwa 100%
 
Hii nchi ina mambo mengi sn kuliko hata hyo mil 50 Rais wetu anajua anachokifanya na kiukwel sisi kama wananchi lazma tujifunze kumuamini na lazma tujue kua yy kama Raisi yuko pale kuchukua maamuzi kwa niaba yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusema ukweli chadema iko kwenye hali mbaya sana,kilichowaponza ni tabia yao ya kupinga kila kitu hata kwenye mambo yenye tija kwa taifa.Ambacho hawakielewi unapompinga Rais Magufuli unawapinga Watanzania mil 50+ kitu ambacho hutakuwa salama kisiasa.Kazi aliyoifanya Rais Magufuli ni kubwa sana kwa watanzania hasa wanyonge.Nani asiyejua dhuluma zilizokuwa zinafanyika kipindi cha nyuma?Mtu unanunua kiwanja leo baada ya mwezi unakuta mwenye pesa zake kajenga ghorofa ukifuatilia huambulii kitu zaidi ya kutishiwa kuuawa,haya mambo awamu hii hayapo ndugu.Huo ni mfano mdogo tu ukiacha mambo mengi ambayo Rais ameyafanya ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu,SGR, ununuzi wa ndege,barabara,mwl Nyerere stiegler's-HEP,elimu bure na mengine mengi.Hayo yote ukiyapinga watanzania watakuona chizi tu hata wasipokwambia,adhabu yake utaiona baadaye.Kwenye uchaguzi wa mwaka huu chadema isitegemee kitu hata kama wasimamishe wagombea kumi kwa ngazi ya urais,wakipata wabunge watatu wakatambikie.
Ajabu ni kwamba wewe unayo Kura moja tu Sasa sijuwi kama itatosha kumpa ushindi huyo kiongozi wako maana mtazamo wako na wa mwengine hauwezi kuwa sawa hata siku moja
 
Yawezekana kilichoongelewa hapa kikawa na ukweli kwa asilimia kadhaa kwa jinsi hali ilivyo

Ni kweli kabisa CHADEMA haiko vizuri kwa sasa hasa baada ya hili saga la Corona.

Corona (japo haitakiwi kuangaliwa kisiasa) imemuinua sana Magufuri na wote waliomsapoti "kiwoga woga" na "kimkumbo mkumbo" na imewadidimiza zaidi waliopingana naye hasa waliopinga kwa kejeli na hadi sasa bado hawajashituka

Inasemekana Mbatia ameshahama kutoka upinzani/chama mbadala na ameshapewa task ya kufanya ndiomaana katika wakati wote hajawahi kutoa mtazamo wake juu ya saga la corona. Yuko kimya hivyo ukimya wake utamfanya siku akiongea asihukumiwe kwa kuunga mkono upande wowote ambao ungeonekana kuwa sahihi

Katika hili CHADEMA na ACT wale over react na ku under rate taarifa za serikali. Corona imetuaminisha wengine kwamba CHADEMA na ACT hawana wapenyeza taarifa kama waliokuwa nao zamani. Taarifa zilizokuwa zinaipa kiburi serikali kwa kutokubali wote walioshauri lockdown au partial lockdown hawakutakiwa kuzi under rate kwa kiasi kile

Si jambo la kawaida kupingana na karibu nchi zote zilizokuzunguka kama huna hoja unayosimamia. Ilitakiwa wachange karata hapa wafukunyue serikalini wanajiamini na nini kuweka rehani Maisha ya watu kiasi hiki!?

Pamoja na yote hayo na yote yaliyosemwa hapa na yote yanayoendelea huko mjengoni na Ndugai na namna wabunge wanavyoitisha press kila kukicha wakati huo huo Mbowe akinyimwa wasaa wa press,

WATU WA TUME WAKISHUKIWA NA ROHO MTAKATIFU WAKAAMUA KWA PAMOJA NA KWA KAULI MOJA KWAMBA WATANGAZE KWA UHALALI YEYETO ATAKAYE SHINDA KWENYE UCHAGUZI, CHADEMA WANAWEZA KUKOSA URAIS ILA WABUNGE NA MADIWANI WATAKUWA WENGI KULIKO WALIOPO SASA.

Kama mnabisha, waombeeni watu wa tume na polisi kwa MUNGU hiyo roho iwashukie watangaze kura kwa kuzingatia aliyeshinda na wathibiti mianya yote ya kuiba au kuongeza kura kwenye maboksi halafu muone maajabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaweza vile vile tusiamini wana Chadema mda si mda wakaanza kusema Freemani kanunuliwa yupo kimkakati kuuza chama
 
Pamoja kuwa chama kikuu cha upanzani kiko katika hari mbaya sana kwa sasa ni kama mtu anapumulia mashine ya ugonjwa wa Korona katika chumba cha wagonjwa mauti uti lakini kinahistoria za ajabu kuibuka kidedea au kukimbiza dakika za majerui.
Chadema kimepita katika misukosuko mikubwa huko nyuma na kuonyesha historia ya kuvuka bila mtu kuelewa au kuamini. Ukianzia kipindi cha Marehemu Chacha Wangwe yule aliyekuwa anautaka uwenyekiti wa chadema alileta mtikisiko mzito wakati ule lakini chama kilivuka salama salmini.

Zito Kabwe na Kitila mkumbo pia nao walileta hekaheka sana ndani ya chama wakati ule Kitila mkumbo alimdanganya Zito kuwa agombee uenyekiti wa Chadema hari ilikuwa tete walifukuzwa wote lakini chama kilivuka salama Act wazalendo ikazaliwa.

Kuondoka kwa Dr. Slaa ambae alikuwa kama injini ya chama na mbeba maono na kuonyesha njia zakupita ambaye aliaminika sana, alileta sintofaamu tena ilikuwa kuelekea katika uchaguzi mkuu ambapo katika short run hakuonekana kuleta madhara makubwa na Chadema ilipita salama na kuwa cha kikuu cha upinzani Tanzania.

Hakuna mtu aliyetegemea kuwa uchaguzi wa 2015 Chadema ingepata wabunge wengi na madiwani kwani uchaguzi wa 2015 Chadema ilimvuta Mwanasiasa nguli Tanzania Edward Lowasa na wenzake na heka heka ilikuwa ya kufa mtu wakitembea mwendo wa mabadiliko na kuzungusha mikono na chama kikuu cha upinzani tunacho hadi sasa.

Wengi tunategemea Chadema kuonyesha maajabu mengine katika uchaguzi mkuu 2020 labda itamvuta Tundu Lisu, au Benald Membe au Freemani mwenyewe kuwa mgombea urais au chochote kile kwani ndiyo kawaida ya Chadema kufanya maajabu.

Lakini kuanzia 2015 hadi leo naandika Chadema ni kama imekutana na kisiki cha Mpingo ambacho kimeng'oa kucha zote katika mguu ambapo kimeleta maumivu makali sana lakini aliyeumia anafukutia ndani kwa ndani haya maumivu na akiulizwa kama ameumia au apatiwe msaada anasema hajaumia kabisa sasa hili pia ni jambo la ajabu sana.

Kinachoonyesha kwa sasa JPM amewapiga pini kali sana yaani kama uwanjani kipindi cha pili dakika ya 85 bao ni 9 bila, na nusu ya wachezaji wa Chadema wamekula kadi nyekundu yaani wanacheza nusu na bado ni wabishi wanaingia hadi katika box kupitia winga ya Korona na kulokudouni.

Wadadisi wa mambo ya siasa wasema kuwa Chadema inapita katika kipindi kigumu sana ambacho haijawai tokea tangia kuaziswa kwa chama hicho na wameenda mbali zaidi na kusema kama hawakuchua hatua za makusudi wanaweza kuanguka na kupotea vibaya kuliko hata CUF na NCCR Mageuzi ambapo vilifulia taratibu.

Zile ngome za Chadema kwa sasa si ngome tena labda kwingine kwani kusema unazitegemea kwa sasa hazipo kama Kilimanjaro, Mara, Mbeya na Mwanza kwani si ngome kwa sasa zimebomoka pakubwa na ujenzi wake unaitaji gharama kubwa si kwakusema zimenunuliwa.

Na JPM inasemekana ni Rais ambaye anauruma sana hata kama ujaomba msamaa uwa anasamehe lakini kwa upande wa Chadema ndiyo anazidi kupigilia misumali hadi misumali ya nchi 6 kichwani sasa atapona mtu kweli sijui?

Wadadavuaji wa mambo ya michezo ya siasa wanasema Mchezaji huyu wa CCM DKT John Pombe ambaye anajua michezo mingi hata ile ya bungasiliga yaani ukiweka ugoko anatupia jiwe la kilo 50 mguuni.

Tusubiri maajabu.
Kabisa, CDM imepitia moto ambao hautawaua bali utawaimarisha zaidi. Natumaini CDM watafanya vizuri zaidi 2020 chama kina mizizi ya uhakika.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom