Uchaguzi 2020 Unaweza usiaminiI CHADEMA kusumbua sana uchaguzi mkuu 2020 kuibuka kidedea

Ni kwasababu hakutakuwa na uchaguzi bali uchafuzi na uhuni, vinginevyo CCM itaagukia pua ndio maana Magufuli aliagiza wakurugenzi ushindi wa lazima eti kisa wanalipwa na serikali ya CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja kuwa chama kikuu cha upanzani kiko katika hari mbaya sana kwa sasa ni kama mtu anapumulia mashine ya ugonjwa wa Korona katika chumba cha wagonjwa mauti uti lakini kinahistoria za ajabu kuibuka kidedea au kukimbiza dakika za majerui.
Chadema kimepita katika misukosuko mikubwa huko nyuma na kuonyesha historia ya kuvuka bila mtu kuelewa au kuamini. Ukianzia kipindi cha Marehemu Chacha Wangwe yule aliyekuwa anautaka uwenyekiti wa chadema alileta mtikisiko mzito wakati ule lakini chama kilivuka salama salmini.

Zito Kabwe na Kitila mkumbo pia nao walileta hekaheka sana ndani ya chama wakati ule Kitila mkumbo alimdanganya Zito kuwa agombee uenyekiti wa Chadema hari ilikuwa tete walifukuzwa wote lakini chama kilivuka salama Act wazalendo ikazaliwa.

Kuondoka kwa Dr. Slaa ambae alikuwa kama injini ya chama na mbeba maono na kuonyesha njia zakupita ambaye aliaminika sana, alileta sintofaamu tena ilikuwa kuelekea katika uchaguzi mkuu ambapo katika short run hakuonekana kuleta madhara makubwa na Chadema ilipita salama na kuwa cha kikuu cha upinzani Tanzania.

Hakuna mtu aliyetegemea kuwa uchaguzi wa 2015 Chadema ingepata wabunge wengi na madiwani kwani uchaguzi wa 2015 Chadema ilimvuta Mwanasiasa nguli Tanzania Edward Lowasa na wenzake na heka heka ilikuwa ya kufa mtu wakitembea mwendo wa mabadiliko na kuzungusha mikono na chama kikuu cha upinzani tunacho hadi sasa.

Wengi tunategemea Chadema kuonyesha maajabu mengine katika uchaguzi mkuu 2020 labda itamvuta Tundu Lisu, au Benald Membe au Freemani mwenyewe kuwa mgombea urais au chochote kile kwani ndiyo kawaida ya Chadema kufanya maajabu.

Lakini kuanzia 2015 hadi leo naandika Chadema ni kama imekutana na kisiki cha Mpingo ambacho kimeng'oa kucha zote katika mguu ambapo kimeleta maumivu makali sana lakini aliyeumia anafukutia ndani kwa ndani haya maumivu na akiulizwa kama ameumia au apatiwe msaada anasema hajaumia kabisa sasa hili pia ni jambo la ajabu sana.

Kinachoonyesha kwa sasa JPM amewapiga pini kali sana yaani kama uwanjani kipindi cha pili dakika ya 85 bao ni 9 bila, na nusu ya wachezaji wa Chadema wamekula kadi nyekundu yaani wanacheza nusu na bado ni wabishi wanaingia hadi katika box kupitia winga ya Korona na kulokudouni.

Wadadisi wa mambo ya siasa wasema kuwa Chadema inapita katika kipindi kigumu sana ambacho haijawai tokea tangia kuaziswa kwa chama hicho na wameenda mbali zaidi na kusema kama hawakuchua hatua za makusudi wanaweza kuanguka na kupotea vibaya kuliko hata CUF na NCCR Mageuzi ambapo vilifulia taratibu.

Zile ngome za Chadema kwa sasa si ngome tena labda kwingine kwani kusema unazitegemea kwa sasa hazipo kama Kilimanjaro, Mara, Mbeya na Mwanza kwani si ngome kwa sasa zimebomoka pakubwa na ujenzi wake unaitaji gharama kubwa si kwakusema zimenunuliwa.

Na JPM inasemekana ni Rais ambaye anauruma sana hata kama ujaomba msamaa uwa anasamehe lakini kwa upande wa Chadema ndiyo anazidi kupigilia misumali hadi misumali ya nchi 6 kichwani sasa atapona mtu kweli sijui?

Wadadavuaji wa mambo ya michezo ya siasa wanasema Mchezaji huyu wa CCM DKT John Pombe ambaye anajua michezo mingi hata ile ya bungasiliga yaani ukiweka ugoko anatupia jiwe la kilo 50 mguuni.

Tusubiri maajabu.
Wenzako wote wameuchuna!
 
Naamini mwaka huu watakuwa vizuri zaidi. Jiwe anavutiwa pumzi tu. Hata Waitara mwenyewe najua atarudi upinzani - subirini mtaona
 
Back
Top Bottom