Unaweza ukachukiwa milele kwa kufanya hivi

Muuza simu used

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
4,393
7,039
Wahenga walishasema ndugu wakigombana shika jembe ukalime! Aisee waliona mbali sana

Sasa ukitokea wapenzi wamegombana na wakaja kuomba ushauri na wewe ukamponda mpenzi wake ni kumshauri kuwa waachane na maneno ya shombo kibao kumponda jamaa! Amini usiamini wanaweza wakaachana sawa ila siku wakipatana na kurudiana utachukiwa milele!

Yaani wewe mtoa ushauri ndio utaonekana ndio mchonganishi, unaweza kupoteza marafiki wengi kwa kujifanya wewe ni kungwi!

Utasikia fulani ndio aliniambia nikuache aisee utachukiwa milele!

Unaweza kutoa ushauri wowote kwa wapendao kama wakikuomba ufanye hivyo ila kamwe usije ukaweka neno muache ama hafai!

Utakumbana na aibu ya mwaka
 
Sidhani kama Muuza simu used anaweza hata kutoa ushauri wowote. Aneweyz, just know, unaposhauri mtu yeyote target yako inapaswa iwe kurejesha mahusiano yao -- kama problem ni mpishano kwenye mahusiano. Halafu washauriwa wanapaswa kujua kwamba the final responsibility ya maamuzi yoyote iko kwao na wala siyo kwa mshauri wao. Ndiyo mantiki ya uleee msemo wa Mstaafu JK: ^Akili za kuambiwa!^
 
Kimsingi ugomvi wowote ambao wewe sio muhusika usitie neno kwasababu huwezi kujua ya mbeleni
Haijalishi ni wapenzi ama ndugu...kaa kimya, kuwa mpenzi mtazamaji

Siku wakiamua kuelewana utaonekana adui kwa namna yoyote ile
 
Kimsingi ugomvi wowote ambao wewe sio muhusika usitie neno kwasababu huwezi kujua ya mbeleni
Haijalishi ni wapenzi ama ndugu...kaa kimya,kuwa mpenzi mtazamaji

Siku wakiamua kuelewana utaonekana adui kwa namna yoyote ile

Ni kweli kabisa mkuu
 
Kuna mshkaj wangu mmoja kipind tuko chuo aliwah kuchomwa na chupa pajan na msichana wake aliapa miungu yote hatakuja kumrudia tuliporud toka likzo tukawakuta wanapika na kupakua nashukru Mungu sikuweka neno baya kwa shem shem...

wanapika na kupakua ungetia neno ungejuta
 
Back
Top Bottom