Unaweza muhukumu Dingi sababu ya matatizo ya mke wake?(mama wa kambo) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unaweza muhukumu Dingi sababu ya matatizo ya mke wake?(mama wa kambo)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by malamia, May 30, 2012.

 1. m

  malamia Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana JF,
  Nakuwa najiuliza mara kwa mara juu ya nini cha kufanya na kubaki in dilema, nimekuwa na mama wa kambo ambae hakuwa na upendo hata chembe mbali na manyanyaso ya kila aina kwa kupendelea mwanae tuu kama mnavyojua. sasa kwa bahati nzuri mungu amejalia kiasi flani nimetusua kimaisha japo si kivilee ila gap ni kubwa nikijilinganisha na mtoto wa huyu mama ambaye kapoteza chanel anasubiri atokee jamaa wa kuoa.
  Kutokana na manyanyaso aliyokuwa akifanya na dingi kutokuingilia kati ilimpa fursa ya kutawala nyumba mpaka kufikia hatua nikawa sikanyagi home! hivi mpaka ninavyozungumza sili nyumbani nikipita ni Hi! juu kwa juu labda nikijiridhisha kuwa msosi unaliwa na wengi na kuhakikisha watu wanapakuwa ndipo nadhubutu.
  kwa hivi sasa huyu mama anaonyesha kujirudi baada ya kuona maisha yangu kidogo safi, natembea nimekaa n.k na wakati huo huo Dingi anavyoona simpi mke wake ushirikiano ananisihi nisahau yaliyopita tugange yajayo eti niachane na mambo ya wanawake hayana maana kwani huyo mama ndo mama mlezi na sina mama mlezi mwingine hivyo nimuheshimu tu. Lakini huyu mama ana hasira kinoma ukuzingatia mwanae ambaye anampenda sana kazaa akiwa home na shule alichomoa yupo yupo tu,...hivi kweli huyu maza anaweza kuwa na nia nzuri nami au ndo anataka kuniangamiza kwani kila nikimulika nilikotoka sioni mahala ambapo alinitakia mema. Dingi nae kwa sasa ananiona mimi kama simuamini,simuelewi na simpi ushirikiano kwa sababu sina maelewano mazuri na mke wake.
  Wadau naomba maoni katika hili,
  Thx in advance-Mdau
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Fanya conflict management.

  Kumsaidia si lazima kumuamini. Fanya kama baba yako anavyosema msaidie na kumheshimu ila usimlete karibu sana na maisha yako ya sasa na familia yako.
   
 3. m

  malamia Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  asante sana Kongosho kwa ushauri, mana aibu...
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  kwanza hapo hama...... Sioni sababu ya kuendelea kuishi na huyo mama yako wa kambo ilhaki umezungukwa na wakuchukiao....

  Pili msaidie baba yako kama una uwezo......tenda wema nenda zako......
   
Loading...