Unaweza kutumia tamko la mdomo la Rais kama ushahidi Mahakamani?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,679
149,864
Naomba kuuliza hivi tamko au agizo la mdomo la Rais unaweza kulitumia mahakamani kama ushahidi au utetezi iwapo utekelezaji wa agizo hilo utakupelekea kufikishwa mahakamani kwasababu moja au nyingine?

Je, mtu huwezi ingia hatiani kwa kuonekana hukumuelewa Rais?

Je, inatosha tu kusema kauli ya Rais ni agizo hivyo litekelezwe kama lilivyo?
 
Naomba kuuliza hivi tamko au agizo la mdomo la Raisi unaweza kulitumia mahakamani kama ushahidi au utetezi iwapo utekelezaji wa agizo hilo utakupelekea kufikishwa mahakamani kwasababu moja au nyingine?

Je,mtu huwezi ingia hatiani kwa kuonekana hukumuelewa Raisi?

Je,inatosha tu kusema kauli ya Raisi ni agizo hivyo litekelezwe kama lilivyo?
Wewe dogo bosi wako jana kasema anataka kufanya vitendo vya kigaidi. Na gaidi ukikumbana nalo ni kuua tu.
 
Kwa mini wewe unataka utumie kauli ipi ya raisi? JPM Ashatoa matamko kobao likiwemo kusitisha vibali vya ajira na kupandishwa kwa madaraja aka vyeo aka nyota aka mshahara
 
Ndiyo. Kauli ya Mkapa ilitumika kumuokoa yule balozi wa Tanzania wa Italia (Costa Mahalu kama sijakosea) aliyekuwa na kesi mahakamani. Raisi hakuthibitisha kama kweli balozi aliiba fedha za Tanzania kwa kuingia mkataba tata au lah.
Mkapa alichokisema ni kuwa yeye alimuona balozi kama ni mtu muadilifu.
Kitendo cha raisi mstaafu kusema kuwa balozi ni mtu muaminifu, mahakama isingeweza kuukataa ushahidi wa mtu mzito kama raisi mstaafu. Hivyo balozi akaachiwa huru.
Mkapa ndiye aliyekuwa karata ya mwisho kumuokoa balozi maana kesi ilikuwa imemkalia vibaya sana.
 
Nimekuelewa mkuu.Awamu hii tujiandae kuona mengi ya aina hiyo.
 
Back
Top Bottom