BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,005
BAK,
Hizi ni baadhi ya mbinu ambazo pengine tunahitaji kuzitafiti zaidi.Mimi niliwahi kusikia kuwa unashika mkono - wrist na eti nyoka huyo hatoenda popote.Niliwai kujaribu kushika mkono na wala sikupiga kelele wala nini.Nikaona nyoka huyoooooooooo anatokomea kwa speed.
Hivi kwa wale wajuzi, wanaweza kutufafanulia kuna uhusiano gani kati ya kushika sehemu ya mwili na kuzubaa kwa nyoka?
Pia niliwahi kusikia kuwa kwa mama mjamzito aliyeshikwa na uchungu, akifunga fundo kwenye nguo basi hatajifungua hadi afike hospitali.Sijui kama ina ukweli wowote.
These are some of the local knowledge that we need to document maana mara nyingi hatuko wepesi ku document vitu vyetu.
Ulichosema nakiafiki kabisa. Mababu na mabibi zetu walikuwa wanafahamu mbinu nyingi sana ambazo bahati mbaya wanakufa nazo bila kutuachia. Kuna mengine, kama hii la nyoka, ni rahisi kulifanyia utafiti ili kulithibitisha, lakini ukiwa muoga hata wa mende, basi ni kazi kubwa mno kushika titi huku unaua nyoka bila kupiga mayowe na kuruka ruka huku na kule na hivyo kushindwa kufanya utafiti kwa kina.
Bibi zangu walikuwa wanatafua jiwe tu huku wameshika ziwa na kukisigina kichwa cha nyoka taratibu. Kwa kweli ilikuwa inashangaza sana nami nilishuhudia wakifanya hivyo mara chungu nzima.