Unaweza kutozwa kodi Tanzania na TRA kwa fedha uliyoipata kwa kufanya kazi nje ya nchi?

2017 No Name

Senior Member
Jul 26, 2017
172
133
Kwa ambao mnajua ningependa kuelimishwa. Mfano ukiwa unaishi Tanzania, ikatokea umeenda kufanya kazi nje ya nchi,kazi ya muda mfupi tu na kurudi. Mfano wewe ni bondia umeenda kupigana tu na kurudi,au ni msanii umeenda kufanya show tu na kurudi au unatoa huduma kwa njia ya mtandao wewe kama wewe na wateja wako walio nje ya nchi wanakutumia hela ila sio tz moja kwa moja bali kwenye account yako iliyo nje ya nchi mf Pay pal.

Kwa nnavyojua nchi ulikopata hiyo hela watakukata kodi ya mapato. Swali langu ni je ukirudi na hio hela tz utakatwa kodi tena? Na je ni kwa kiasi gani?

Swali langu lingine, Double taxation law ni nini na inafanyaje kazi.
 
Last edited by a moderator:
Kuna kitu kinaitwa withholding tax, tafuta kwa sheria ya hapa inafanyaje kazi... kitu kama hicho.
 
Last edited by a moderator:
Sheria ya Kodi ya Mapato inakutaka kama wewe ni raia "resident' kutozwa kodi kutokana na mapato unayopata sehemu yoyote duniani. Kama sio raia "non resident" basi utatozwa kwa mapato uliyoyapata Tanzania, Nitacheck baadae kifungu cha kodi kinachohusika. Kama ulipopata mapato kuna DTA na Tanzania hautatozwa Kodi tena
 
Last edited:
sasa kwa mfano mimi natoa paypal naingizia bank kisha natumia mpunga wangu je hapo natakiwa kulipa kodi kwani au washa kata tayari.
 
Sijui chochote kuhusu kodi lakini ulipotaja ubondia nikakumbuka kitu.

Joe Louis alikutwa na madeni mengi ya kodi hadi akafilisiwa na kodi ilijumuisha mapambano ambayo hajapigania Marekani.

Manny Pacquiao alifungiwa akaunti zake Ufilipino kwa kudaiwa kodi ambayo nyingine ilijumuisha mapambano ambayo hakupigania Ufilipino.

Hoja yake ilikua ni huko alipopigana ameshakatwa, ila hawakumsikiliza.
 
Chief naomba unieleweshe zaidi.

Let's say nimeshafungua akaunti CRDB, nini natakiwa nifanye?
waambie crdb kuwa unataka kufana manunuzi online kisha watakupa form ya kujaza utatumiwa msg kwenye simu utaingia online kwenye site yao utaji register kama huwezi basi unaenda na simu unawaomba wakusaidie
 
Asante chief.
 
Sikumbuki vifungu vya kodi lakini kwa uzoefu wangu kutokana na kufanya kazi nje ya nchi na pia kuwa na watu nje wanaofanya kazi za Tanzania wakiwa huko nje, utaratibu upo kama ifuatavyo:

1) Kama wewe ni mtanzania umeenda kufanya kazi nje, hata kama mapato yako yatalipwa kwenye akaunti yako ya bank iliyopo Tanzania, kodi utakatwa kwenye nchi unakofanya kazi. Hapa Tanzania hutakatwa chochote maana tayari umelipa kodi huko unakofanya kazi ambako kimsingi ndiko mkataba wako wa kazi ulipo.

2) Kama unafanya kazi nje lakini unaishi Tanzania na kufanyia kazi Tanzania, utalazimika kulipa kodi Tanzania, na kwa baadhi ya mataifa, utalazimika kulipa WHT kwenye nchi ambayo kazi unayoifanya ipo.

3) Kama kuna mtu ambaye siyo Mtanzania, haishi Tanzania lakini anafanya kazi kwenye kampuni iliyoandikishwa Tanzania au hana mkataba na kampuni ya Tanzania lakini akafanya kazi zilizopo Tanzania, atatakiwa kulipa WHT Tanzania. Kwa sasa ni 10%
 
Asante kwa Elimu mkuu
 
Je hela zilizo kwenye account zapaswa katwa kodi?
Mfano umepata hela kwa betting sites za nje na wakakurushia kwenye account ya tz
 
Back
Top Bottom