Unaweza Kutokea Muujiza, Januari 22 Kata Zoote na Jimbo la Dimani Vikaenda Upinzani.

Kwa uchaguzi wa tume hii iliyoko chini ya kiongozi ambaye haamini katika siasa za ushindani naona kama wapinzani wameamua kupoteza muda wao na pesa. Hakuna taasisi yoyote inayofanya kazi kwa uhuru halisi zaidi ya kujipendekeza tu. Hivi najiuliza CUF kama walisusia uchaguzi wa marudio huko Znz, je huu wanashiriki kwa vigezo gani? Wakati mwingine upinzani wa namna hii ni kama kujichoresha tu.
Uliosusiwa ni uchaguzi wa BLW na huu ni wa ubunge wa JMT ambao haukususiwa
 
Salaam Wakuu.

Najaribu Kutafakari, hivi ikatokea Kata zoote zitakazofanya Uchaguzi wa Madiwani Januari 22 pamoja na Jimbo la Dimani vyote kwa Pamoja wakashinda Upinzani, Je, Makada watiifu wa CCM na Mwenyekiti wa CCM Taifa watapata picha gani kwa Taifa.

Kuna kila dalili CCM ikapoteza Kata zoote ama kuchukua chache saana na Jimbo la Dimani pia kwenda CUF.
Hii yote ni kutokana na Wananchi kukosa kile walicho kitarajia kutoka kwenye Uongozi huu wa awamu ya 5 yaani kubwa kuboresha maisha yao. Maana badala ya Maisha kuwa yawe na Unafuu, kwanza ndiyo kila Uchao yanapaa juu, Sukari Juu, Chakula kiujmla juu na hakipatikani.

Kwahiyo ndugu zangu Chama Twawala Tafadhali Jiandaeni Kupokea mlichopanda, na iwe Fair si kwa Kutegemea Vyombo vya Dola viwasaidie kuhujumu maamzi ya Wananchi.
Vizuri ukiishi kwa kujipa moyo,inakusaidia kukuepusha na maradhi ya moyo
Kwa taarifa yako ccm wana kata moja tayari
 
Acha Ujinga wewe. Muulize mwenyekiti wako kwanini amezuia Mikutano ya Wanasiasa ya hadhara, anajua yupo pale si haki yake Ila ni dhuruma tu. Yoote hiyo anajihami.
Hivi huwa wanawadhulumuje?yaani mnajua na mnatazama tu!aisee mie siwezi.
 
Kata moja Dodoma ipo kibindoni hiyo ni kabla ya uchaguzi!
Ebdelelea kuota, ukishutuka toka usingizini ndo utajua kuwa Lowasa hajawahi kuwa mpinzani!
 
Back
Top Bottom