SoC01 Unaweza kutoa mimba bila kujua mtoto unayemtoa na kumdhulumu uhai wake angekuja kuwa kama muokozi wa taifa

Stories of Change - 2021 Competition
Aug 19, 2021
6
7
Willis Austine Chimano, Bien Aime Baraza, Delvin Savara Mudigi na Polycarp Otieno ni wanamuziki kutoka nchini Kenya wanaounda kundi la Sauti Sol. Katika moja ya wimbo wao bora unaowavutia wasikilizaji wengi zaidi ni ule wa NEREA wa mwaka 2015 ambao waliwashirikisha Amos na Josh.

Ndani ya wimbo huo waliimba mistari iliyokonga nyoyo hata zikakongoka. Mwandishi wa vitabu wa zamani wa Kenya marehemu Ken Walibora aliwahi kuadika kwenye kitabu chake alichokiita ‘Kufa Kuzikana’ ”baadhi ya nyimbo ukizisikiliza maneno yake yanafikirisha, yanaelimisha, yanaonya, yanaasa na yanafurahisha kwa wakati mmoja”. Hivyo ndivyo ulivyo wimbo wa Sauti Sol Nerea.

Achana na hao ‘Wajaluo’ kutoka pale Kenya kwenye himaya ya Kenyatta kama una nauli chukua mabegi yako na ufunge safari hadi visiwa vya Madeira kule Lisbon nchini Ureno nenda katika maktaba zao ulizia kitabu cha Maria Dolores Dos Santos. Huyu ni mama mzazi wa mchezaji nyota wa mchezo wa soka dunia Crstiano Ronaldo kinachoitwa MAE CORAGEM kwa lugha ya kireno na kwa kiswahili cha kawaida maana yake ni ujasiri wa mama.

Kwenye kitabu hicho mama Maria Doroles ameandika mambo mengi kuhusiana na familia yao ikiwemo wakati alipotaka kutoa mimba ya mwanae mpenzi Cristiano Ronaldo. Mwenyewe ameandika ndani ya kitabu chake kuwa “nilitamani kutoa mimba ya Ronaldo, nilitumia njia nyingi bila mafanikio na madaktari waligoma kunisaidia kutoa mimba. Uamuzi uliofuata baada ya hapo ilikuwa ni kunywa pombe kali ili kutoa lakini sikupata mafanikio niliyoyahitaji, nilitumia kila njia ila nilishindwa, sikutaka kumzaa Ronaldo. Sikujua kama atakuja kuwa huyu anaenifanya nijivunie kuwa mama."

Kufanya kosa na kujutia kufanya kosa ni mambo ambayo yanaumiza mioyo ya watu hata mama yake Ronaldo anajutia jambo alilolitaka kulifanya kwa mwanasoka huyo nguli ulimwenguni. Na Ronaldo anajua bila za mama yake kuna siku alimrudi na kumwambia "mama angalia ulitaka kunitoa nilipokuwa mimba na sawa mimi ndiye kinara wa nyumba yetu, unanitegemea na familia yote inanitazama mimi, tazama jinsi dunia inanitazama naitwa mchezaji mkubwa duniani unadhani hii ni fahari yangu peke yangu? Inakuhusu na wewe mama yangu unapaswa kujivunia sana kuwa na mimi"

Kumbukumbu zimenikumbusha Saudi Sol na zikanipeleka mbali zaidi hadi nchini Ureno kwa mama mzazi wa Cristiano Ronaldo, pindi ninapofikiria wasichana wengi wa siku hizi wakiwa wanabeba na kuchuma dhambi kubwa isiyosameheka kirahisi mbele ya Mungu, dhambi ya kutoa mimba na kuondoa uhai wa vimbe wengi wasiokuwa na hatia.

Mara ngapi dunia inashuhudia kijana fulani anamshauri mwenza wake wa mahusiano atoe mimba aliyompachika? Ni Mara nyingi shawishi zimeendelea kutokea kwenye jamii hasa mijini na kwa uchache vijijini kwa baadhi ya watu ili wasichana watoe mimba kwa madai ya kwamba bado hajajiandaa kulea na kutoa huduma kwa mtoto ajaye. Au wasichana wenyewe wanaamua kutoa mimba ambazo walikuwa hawajazitarajia kwa sababu muda wao wakuendelea kuutumikia ujana haujakoma.

Swali la msingi la kujiuliza ni nani anajua katika mimba zinazotolewa kulikuwa na mtoto ambae baadae kwa majilio yake katika ardhi hii angekuwa mtu mkumbwa maishani na kusaidia taifa lake kama ilivyo Cristiano Ronaldo nchini kwao.

Unaweza kutoa mimba bila kujua mtoto unayemtoa na kumdhulumu uhai wake angekuja kuwa kama muokozi wa taifa kama alivyokuwa Mwalimu Nyerere kwa Tanzania na Nelson Mandela kwa Afrika Kusini au mchezaji mkubwa wa mchezo wa soka kama ilivyokuwa kwa Victor Wanyama nchini Kenya?
Kwa hivi wanawake wote wenye tabia kama hiyo ya kutoa mimba au wenye wazo la kutoa mimba jambo hili halifai, unaweza kutoa mimba kwa sasa usipate madhara yoyote lakini kadiri muda unavyozidi kusogea unaweza usipate tena mtoto kwakuwa umeishaharibu mfumo wote wa uzazi na kwa wale isiyokuwa bahati wanaweza kupoteza uhai wao kabisa kwa sababu ya utoaji mimba, mambo kama hayo yametokea mara nyingi kwenye historia za kitabibu.

Jambo lingine kubwa zaidi ni kuingia katika orodha ya wauwaji maana kuondoa uhai wa kiumbe ni jambo baya inahitaji moyo wa chuma na roho ya paka kwa hivi jambo hili halifai kwa mwanadamu anayetegemewa kuwa miongoni mwa viumbe bora sio kufanya matendo ya unyama kama kudhulumu nafasi ya kiumbe.

Kama kwamba matokeo yoyote yanatarajiwa yawe hasi au yawe chanya wakati wakufanya jambo lolote hivyo basi hata baada ya zinaa mimba au magonjwa hatarishi kwa afya ya mwanadamu hutokea, basi wahusika wa jambo hili lazima wakubali matokeo yake isiwe kuwakatili viumbe wasiokuwa na hatia kuwakatisha uhai wao.

Lakini zaidi Mungu ana mipango yake unaweza kushika mimba leo ikafika kesho usiweze kubeba tena. Hakuna tena utakachoweza kufanya baada ya hayo kutokea, ni hapo ndipo ugumba utakuwa umekaa mahala pake.
Tangu vizazi na vizazi desturi ya wanadamu kuonya juu ya mwenendo mbaya kwa binadamu wengine ilikuwepo, ni kama walivyoimba Sauti Sol na yao Nerea “usitoe mimba yangu” huwezi kujua kiumbe unachokikatili leo pengine kingekuwa nuru ya ulimwengu baadae, mfano mzuri upo chini Ureno kwa mama Maria Dolores Aveiro alipotaka kutoa mimba ya mchezaji nguli wa soka duniani Cristiano Ronaldo.

Kwa sasa ni Ronaldo huyo huyo aliyetaka kumuua ndiye amekuwa tegemeo lake ndani ya familia yao ambayo kabla ya Ronaldo fahari ilikuwa ni kitu kigeni na maisha mazuri walikuwa wakiyaona kwa watu wengine pekee.
Cristiano Ronaldo kwa sasa ametajwa kuwa mwanasoka wa kwanza kuingia katika orodha ya watu matajiri duniani akifikisha utajiri wa dola bilioni moja. Mama Maria angefanikiwa kutoa mimba ile mwaka 1985 mambo makubwa yote kumuhusu Ronaldo kwenye soka yangetokea? Jibu la swali hili ni hapana.

Duniani kote maendeleo yanatokea ongezeko la watu linapozidi ndipo maendeleo mengi yanakuja sasa kama wanawake wakiendelea kukithiri katika utoiaji wa mimba maendeleo hayatatokea na nguvu kazi ya taifa lolote ni rasilimali watu.

Sauti Sol waliiimba ili kuwaasa watu wasitoe mimba na mafunzo ya wimbo ule wa Nerea yanatakiwa yaende duniani hata milele kwa lengo la watu waendelee kuelimika na kufahamu juu ya madhara ya jambo hilo na kuweza kupoteza watu ambao wangekuja kuwa bora sana katika uhai wao kama wangeishi.
 
Back
Top Bottom