Hello wana JF,
Nilikutana na marafiki zangu wakiwa wamejiandikisha kwenye vituo tofuati na wanavyoishi wengi wakidai kuhusu foleni na changamoto zilizokuwepo kwenye zoezi la uandikishaji. Kwa hiyo wengi wakaamua kujiandikishia kwenye vituo ambavyo waliona havina watu wengi. Nilipowauliza kama wana mpango wa kupiga kura wakasema watapiga tuu kura ya Rais kwenye kituo chochote. Mimi niliposikia wanasema watapiga kura ya Rais nikajiuliza how can this be possible wakati sio kituo chako?
Ili tuweze kujua kama kweli unaweza kupiga kura ya urais popote hata kama sio pale ulipojiandikisha unatakiwa tujijibu maswali kadhaa. Kwanza ufafanuzi niliowahi kusikisikia kwenye TV ukitolewa na Tume kuhusu siku ya uchaguzi ni upigaji kura utakua kama ilivyokua zamani kwa maana hiyo sio kwa njia ya kieletroniki. Tutapiga kura kama zamani ambapo utaenda na kitambulisho chako, wataangalia kama jina lako lipo kwenye hicho kituo halafu utapiga kura, na kama halipo basi huruhusiwi kupiga kura.
Swali la kwanza, kwa nini wanahakikisha jina lako lipo kwenye kituo? Ikumbukwe ili uweze kupiga kura lazima kuwe na zile polling paper kwa ajili yako kwenye wale wote wanaopigiwa kura, iwe ni rais, mbunge au diwani. Kwa maana hiyo, yale majina na idadi yake yanawafanya Tume waweze kujua ni polling paper ngapi wanatakiwa kuzipeleka pale kwenye kituo. Wasipojua idadi ya watu hawawezi kujua ni karatasi ngapi za kupigia kura wazipeleke pale. Kwa maelezo hayo, ina maana kama jina lako halipo pale kwenye kituo huwezi kupiga kura kwani karatasi yako haiwezi kupatikana.
Swali la pili. Itakuaje tuweze kupiga kura urais kwenye kituo chochote hatuoni ya kwamba kuna uwezekano wa kuchakachua mkubwa? Nina maana ya kwamba, kama tukiruhusiwa kupiga kura kwenye kituo chochote ambapo hata jina langu halipo wale jamaa wanaweza kuongeza kura zao kwenye sanduku na wakasema ni watu ambao hawakuwepo kwenye kituo hiki walipiga kura. Na itawafanya watu wazunguke mjini wakipiga kura za urais kwenye kila kituo na kuondoka. Kwani tunajua ni lazima kura zisizidi idadi ya watu waliopo kwenye lile daftari la kituo, ina maana kama ukiruhusu watu wengine, ile control ya namba za wapiga kura unaiiondoa na watu tutapigwa kama kawaida.
Ninachofahamu hapo awali kulikua na utaratibu wa Tume ya taifa ya uchaguzi kutoa fursa ya sisi kubadilisha kituo kile nilichojiandikishia kabla ya siku ya kupiga kura. Kuna watu wanasafiri au kuhamia sehemu nyingine, kwa kipndi kile tulikua tunabadilishiwa kituo na jina lako linapelekwa kwenye kile kituo kipwa. Sijui kwa mwaka huu itakuaje kutokana na muda tulionao kwa sasa. Cha msingi labda tume watatusaidia kujua kwa sisi tuliojiandikisha vituo vya mbali na tunapoishi tutafanyaje ili tuhamishiwe kwenye vituo vya karibu.
Wadau ndo niliona nichangie kwenye hili nililokutana nalo.