Unaweza kumwacha mkeo aolewe na mwanaume mwingine ukipewa pesa?

Kwa wanawake si jambo la kustaajabisha hata kidogo kumwacha mumewe baada
ya kurubuniwa kwa pesa. Swali langu linakuja kwa wanaume, Linaweza kuwa swali la
ajabu lakini kwanza nikusimulie kisa hiki:-

Fundi ujenzi mmoja(.............) alikubali kumwacha mkewe baada ya kupewa mil.18
na bosi wake na kujengewa nyumba. Ni tukio la kweli kabisa na halina shaka, alimwacha
mkewe ambaye alionekana kumvutia zaidi yule bosi na mpaka sasa yuko naye na kwa
kumbukumbu yangu huu unaweza kuwa mwaka wa 12.

Nimetafakari tu hili jambo nikataka kujua je wewe unayesoma kama ni mwanaume uko tayari
kumwacha mkeo katika mazingira kama hayo, TUFANYE TU HUYO TAJIRI KAKUAHIDI MILIONI 500.

Mke ? Kuuza mke kabisa... ila likija fungu kama 1 Billion nina muuza kwa mkopo... ila nikiwa nimezaa nae basi nitafanya 500 million, maana huyo mda wowote anarudi watoto watatuunganisha :rolleyes::rolleyes::rolleyes:
 
Mimi ukinipa laki tano nakupa mke na anakuja kwako na vyombo vya kupikia kabisa, yaani unabeba mke na vyombo vya ndani
 
Ili nahisi linawezekana kwa wengi, jiulize kwanini wengi wanaofumania wake zao hutaka kulipwa fidia tena interms of money, sasa anashindwaje kuchukua pesa ndefu, kama kwenye fumanizi kapoozwa yakaisha 😁😂😁😂
 
Wengine wanaweza kukupa mke bure na kukuongezea na hela juu, haya maisha haya na hawa viumbe hawa waache kama walivyo
 
Nataka nijionee mwenyewe. Yaani uwe na billion usiwe na furaha labda una maradhi lakini siyo suala la mahusiano no never

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
Kawaulize mtu bilionea halafu kila mwezi anabadilisha damu na baadhi ya vitu haruhusiwi kutumia....hela siyo kila kitu duniani japo ina nafasi yake
 
Back
Top Bottom