Unaweza kumuacha mpenzi wako kisa haamini uwepo wa Mungu??

Una mpenzi wako, mpo katika uchumba. Kwa kipindi chote ame fake kuwa ni muumini wa dini fulani ambayo ndio unayo wewe.

Sasa siku unakuja gundua si kweli, hana dini na haamini uwepo wa Mungu.

Mambo mengine yupo safi, ni mstaarabu na mwenye nidhamu. Hajawahi kukutonesha, kukuumiza wala kukutenda. Anakupenda sana nawe wampenda. Hana tatizo na imani yako, kakupa uhuru uamini utakavyo..

Eti, waweza mwacha kisa tu haamini uwepo wa mungu, na pamoja na jitihada za kumbadilisha zimegonga mwamba?

Karibuni,
Kwanini usimuache bro ! Mbona ni rahisi tu. Asiemuamini Mola huyo ni mshiriki na vipi utamuoa mshirikina mzee ?

Mzinifu kwa mzinifu mwenzake au mshirikina na mshirikina kwa mshirikina mwenzake.
 
Ndege wafananao huruka pamoja.kama inashindikana kufikia muafaka kwenye ishu nyeti Kama hiyo Hakuna namna tunaachana tu
 
kuna maswali machache na ya muhimu unatakiwa kujiuliza kabla ujafanya maamuzi,
kama haamini uwepo wa Mungu itakuaje mkiwa ndani baada ya ndoa?
nini kitatokea kwa watoto wenu mtakao wazaa?watakua na kulelewa katika misingi ipi?
upo tahari kuona watoto wako hawana imani?
Jifikirie na kisha ufanye maamuzi sahihi,
 
kama hanizuii imani yangu....na watoto wangu...wala sina shida kabisa....simwachi.....ninampenda....nitajaribu kwa nafasi yangu kumuweka sawa,,,, na sitaacha kamwe kumshauri.......ila asiingilie uhuru wangu wa kuabudu......hata watoto wakiwa wakubwa wakaamua hayo siwazuiii.....ila wangali wadogo kama ni masjid au kanisani.....hiyo watoto ni lazima....
 
  • Thanks
Reactions: amu
Back
Top Bottom