Unaweza kukumbwa na mikosi mpaka unaona dunia haina maana

April umeachwa na June unaachwa? Hivi ni lazima uwe na mpenzi.. Punguza kukurupuka mzee!!
 
Pole sana mkuu...kipindi hiki jitahidi kutuliza akili usifanye kitu kuimpress au kuwawin watu wako mfano boss, mpenzi majirani, ni hatari maana unaweza kujikuta unaharibu kila unachoshika....

tulia waza vizuri pia anza kujiwekea saving zako maana naona upo kwenye uangalizi job lolote laweza kutokea endapo ukifanya mistake nyingine....Mungu akusimamie
 
Wakati mwingine kwenye maisha tunaogopa kufanya kivingine lakini inasaidia sana tu,unaweza kubadilisha kazi,makazi na marafiki wote,potelea hata mikoa mingine kaanze upya,usipoteze wazazi na watoto wako tu iwapo wapo wanaishi,badilisha mpaka namba ya simu na nenda kaanze na watu wapya kabisa maeneo ya ugenini na baada ya miaka mitano itaona uko vingine kabisa kimaisha, mala zote uoga ndiyo jambo linalo tugharimu kuliko kitu kingine,inawezekana watu wako wanao kuzunguka..ndugu, marafiki, wafanyakazi wenzio, majirani, mke/wake/mume..ndiyo chanzo cha matatizo yote uliyo nayo,kua kinyonga na utafanikiwa
Noted
 
Pole sana Mkuu Maisha tunapitia binadamu wote hivyo usijali! Muamini Mwenyezi MUNGU
 
Aisee kwa upande wangu huu mwaka kama umekuwa wangu peke yangu.

Picha lilianza pale pale February tuuuu..

February 2020
1. Kuiingizia kampuni hasara ya milioni kadhaa..

March 2020
Kupunguziwa mshahara zaidi ya asilimia 40

April 2020 (a)
Kuachwa na mpenzi niliyekuwa nampenda

April 2020 (b)
Kuondokewa (kufiwa) na mtu wangu muhimu katika maisha

May 2020
Kupata kashfa dhidi ya mwanafunzi wa sekondari (Jela yaniita)

June 2020
Kukosea namba na kumtumia mtu mwingine na nisiipate (laki 8.5)

June 2020
Kuhama nyumba kwa ajili ya ufinyu na ugumu Wa kulipa Kodi.

Jana tar 25,June, 2020
Kuachwa Tena rasmi kabisaaaaa na mwanamke mwingine.

Ooooh
Dunia Kama imenielemea hivi aisee
Huu mwaka umekua na changamoto kwa watu wengi...mpaka wengine wanasema "kikubwa uhai"...lakini kwa misukosuko yako, Sio mbaya uka reset mipango na mienendo yako...itakusaidia.
 
Back
Top Bottom