Unaweza kukumbwa na mikosi mpaka unaona dunia haina maana

mzee wa kasumba

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,432
2,892
Aisee kwa upande wangu huu mwaka kama umekuwa wangu peke yangu.

Picha lilianza pale pale February tuuuu..

February 2020
1. Kuiingizia kampuni hasara ya milioni kadhaa..

March 2020
Kupunguziwa mshahara zaidi ya asilimia 40

April 2020 (a)
Kuachwa na mpenzi niliyekuwa nampenda

April 2020 (b)
Kuondokewa (kufiwa) na mtu wangu muhimu katika maisha

May 2020
Kupata kashfa dhidi ya mwanafunzi wa sekondari (Jela yaniita)

June 2020
Kukosea namba na kumtumia mtu mwingine na nisiipate (laki 8.5)

June 2020
Kuhama nyumba kwa ajili ya ufinyu na ugumu Wa kulipa Kodi.

Jana tar 25,June, 2020
Kuachwa Tena rasmi kabisaaaaa na mwanamke mwingine.

Ooooh
Dunia Kama imenielemea hivi aisee
 
Pole sana mkuu ndio maisha kikubwa uzima tu mambo mengine yataenda tu, kama ujapoteza uhai hayo mengine yatakuwa sawa ni swala la muda.
 
Wakati mwingine kwenye maisha tunaogopa kufanya kivingine lakini inasaidia sana tu,unaweza kubadilisha kazi,makazi na marafiki wote,potelea hata mikoa mingine kaanze upya,usipoteze wazazi na watoto wako tu iwapo wapo wanaishi,badilisha mpaka namba ya simu na nenda kaanze na watu wapya kabisa maeneo ya ugenini na baada ya miaka mitano utaona uko vingine kabisa kimaisha, mala zote uoga ndiyo jambo linalo tugharimu kuliko kitu kingine,inawezekana watu wako wanao kuzunguka..ndugu, marafiki, wafanyakazi wenzio, majirani, mke/wake/mume..ndiyo chanzo cha matatizo yote uliyo nayo,kua kinyonga na utafanikiwa
 
Pole sana mkuu kuwa karibu na mola wako atakuongoza na kukutoa katika matitizo yako.
 
Back
Top Bottom