Unaweza kujiua kwa sababu ya mpenzi wako>?

John W. Mlacha

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
3,504
1,341
msichana jirani kanywa sumu juzi ..kisa kakuta meseji ya kimapenzi ya mdada mwingine kwenye simu ya boyfriend wake ...
eti ndio solution?
 
mapenziiii.....YANA WEZA KUKUFANYA,kumkana mama ako,babaako,KUTEKELEZAA FAMILIA YAKO MKEE NA WATOTO,kuuwa au kuuliwa,MAPENZI kizunguzungu,mapenzii upepo,haya mapenzi sijuii ni jini.
 
kweli sikitiko la mahaba lashinda la msiba! niliwahi kuwaza hivyo hapo zamani lakini siyo sahihi kabisa ya nini kujiua wakati mwenzio yaendelea kura raha!
 
Kukuta meseji tu kumtoe roho!? Huo ni utoto unamsumbua.
Huwa inakera kuona mtu ana invest muda wake, mali zake na moyo wake kwa mpenziwe ambaye kwa makusudi naye anaamua kuichezea nafsi ya huyo mpenziwe kwa kuhangaika na watu wengine. Ki ukweli huwa inauma sana ila siyo kufikia level hiyo ya kujiua.
Mweee, :A S embarassed:
 
Hivi kuna kitu kizuri kama uhai/kuishi? Mi binafsi cwezi kujiua kisa mapenz au mpenz tena bora angekuwa mzazi ndo cwezi pata mwingine lkn mpenz siwezi kabisa kwan nitajua huyo hakuwa riziki yangu.
 
Nakumbuka kuna jamaa mzumbe mwaka wa 2 alitolewa nje na demu wake akaanza kulia kuwa atajiua siku ya uchaguzi akigombea urais chuo kizima kililipuka najiuaaaaaaaaaaa najiuaaaa demu alimuonea huruma wakarudiana sasa ni mke na mume miaka kadhaa
 
so pathetic... alitaka kujiua kwani wanaume wameisha? there is always something better somewhere provided you are patient enough
 
Yaani wa2 wengne kweli tunatofautiana,mi kwa kweli siwezi fanya jambo kama hili,sasa kama meseji 2 shida angewakuta chumbani wanafanya angefanyaje?yaani hata angekuwa ndo mwanaume mwenyewe duniani wala nisingewaza kujiua,huyu anatakiwa achapwe vizuri na wamama na mabibi,
 
kwanini nijiue,wakati nikifa yeye atabaki anakula raha duniani??

Hapo chacha.....lol!!! Ila kusema ukweli hii yaweza kuwa ni tatizo la kisaikolojia......may be tusimlaumu saana, kuna kitu aliamini katika hiyo hatua aloichukua! Pole yake kwakweli!
 
Sasa angekuta ya mpenzi wake kwenye sim ya mdada si ndio ingekua balaa?
How could her man prevent a third person from writing him a message?
 
msichana jirani kanywa sumu juzi ..kisa kakuta meseji ya kimapenzi ya mdada mwingine kwenye simu ya boyfriend wake ...
eti ndio solution?

Kujiua ni hulka (suicide tendency) ya watu fulani fulani ambao wao wana mtazamo tofauti na watu wengi kwenye kukabili changamoto zao. Inaweza ikawa kwa sababu ya kukata tamaa (mfano kwa watu wenye msongo wa mawazo, ugonjwa usio na tiba, au maisha magumu etc..), au wengine ni kisasi (kuwaumiza au kusend message fulani mfano mtoto anayejiua kwa kutofautiana na wazazi, au mke/mume kwa kutofautiana na mwenzi, suicide bombers etc..), au wengine ni ushujaa au kuepuka adhabu kali (mfano mtu ameua na anajua naye atauawa au kufungwa, suicide bombers etc..)

Nasema hulka kwa sababu kuna watu wengi tu ambao wanapata changamoto hizo hizo au zaidi ya hizo lakini hawajiui..sababu tu hawana hulka hiyo ya kujiua. Na mwenye hulka ya kujiua pindi ipatikanapo sababu tu ya kujiua...be sure he/she will attempt/commit suicide. Kuna session maalum za counselling kuwasaidi watu wenye suicide tendencies kwa pyschiatrists/psychologists. Muhimbili idara ya magonjwa ya akili ipo. Ila ni vigumu kumtambua mtu mwenye suicide tendency mpaka atakapo attempt kujiua, au kuna wale wengine ambao utanguliza vitisho kama...ukifanya hivi sijui ntajiua, au ikiwa vile ntajiua! Ukishaona hivyo ujue mtu huyo anahitaji msaada wa kisaikolojia...kwa sababu tayari ameshaconsider kujitoa roho kama moja ya solution ya changamoto zake...I lost a close friend ambaye alikuwa ana hizo sana, ilifika wakati akawa akitishia hivyo wazazi wake wanamuambia jiue si tutazika...na kweli, siku moja akajiua!
 
Back
Top Bottom