Unaweza kujifunza kitu kupitia mimi

NOTE: SIKO VIZURI KTK UANDISHI, MAPUNGUFU UYAVUMILIE CHUKUA UJUMBE

Naanzia baada ya kumaliza form 4.

Nikiwa nimemaliza form 4 nilichaguliwa kujiunga na A level kwakuwa mambo ya kiuchumi yalikuwa ni magumu kifamilia nichelewa kuripoti ili niweze kuweka sawa mambo ya kifedha mara nianzapo Form Five, maana huko O level niliacha madeni ya ada nikaona na huku isiwe kama O level.

Nilifika shule A level wenzangu ndiyo wanaludi kutoka midterm, kwahiyo nichelewa nusu mhula.

Niliendelea na shule ila kiukweli mpka tunakaribia mtihani nilijiona sijajiandaa vizuri nikawa nafikiria niombe kurudia mwaka mmoja ili nijiweke sawa, ila nikiangalia nguvu ya kiuchumi haikuwa inaruhusu maana nilicho kikusanya kilikuwa kinaenda ukingoni.

Nikaona nifanye tu mtihani liwalo na liwe.
Matokeo yakatoka hayakuwa mazuri sana hayakuruhu kupata chuo kikuu cha serikali, ila ualimu yalifaa na mimi ualimu haukuwa wito wangu nikaona nifanye kitu kingine. Nikajaribu jeshi nikakosa nafasi kwenye usahili wa mwisho.

Ila kipindi chote hicho akili yangu ilikuwa inapenda kufanya biashara ila tatizo lilikuwa mtaji kwahiyo nikawa nafikiria namna ya kupata mtaji.

Note: wakati huo wote sikuwa na kazi rasmi nikawa najichanya viwandani kutafuta kazi nazilikuwa hazipatikani, unakaa getini kuanzia Asubuhi ya saa 12 pengine unaweza bahatisha kazi ya kibarua ya siku moja.

Nakumbuka wakati ule kibarua tulikuwa tunalipwa 1500/= ukipata hiyo unabajeti ule siku tatu kwakuwa huna uhakika kama kesho unaweza pata tena nafasi ukaingia kazini. Ile hali nikaona hapa sitaweza kupata hata mtaji.

Sikumoja nikaona tangazo la kazi Zanzibar na qualification ninazo nilienda siku ya usahili nikapata kazi ila mikataba yao ilikuwa ya janjajanja nikaona pia siwezi pata mtaji nikaacha kazi baada ya siku 19 tu za kazi, ingawa wafanyakazi wenzangu waliona kama napoteza bahati ila kwangu lengo lilikuwa kupata mtaji.
Nikaludi Dar nikaendelea na kusaka kazi itakayo weza nipa mtaji.

Siku moja nikaona watu wanasotea kazi ya car parking mjini nikajichanganya nami kuomba kazi ila napo nafasi zilikuwa ishu kupata. Nilibahatika kupata day waka ( maaana yake leo upo kazini ila kesho hujui kama utaingia kazini maana hawakuifanya kuwa rasmi) ila nilibahatika kufanya kwa miezi 9 nilifanikiwa ku save kama laki 6.

Ila hayo mazingira ya ku save laki sita niliishi kigumu sana nilikuwa nakula jioni na asubuhi ni andazi moja na mchuzi wanauita selwa k/koo na mchana ni kahawa na kashata pia nilikuwa na bajeti ya maji2 ya sh 100, maji ya Azam ya kiroba kabla hayajazuiliwa.

Niliacha kazi ya parking nikiwa na laki 6 wenzangu wakasema kwanini unaacha kazi, wakinishauli hiyo hela sasa ninunue uwanja nifikirie kujenga.

Malengo yangu yalikuwa kuanza biashara, kweli nilifanikiwa kuanza biashara ingawa changamoto zilikuwa nyingi nilikomaa nazo hivyo hivyo ili niweze kukuza mtaji ingawa ilikuwa kazi ngumu kwakuwa naanza biashara tayari nina wadogo wananiangalia wanasoma kwenye familia wewe unaonekana ndiyo afadhali hata kwa upeo.

Duka likawa halikui kwakuwa majukumu ni Mengi na mtaji kidogo, nikajaribu kwenda kukopa ila nikawa sina sifa ya kukopesheka.

Nikafikiri kubuni biashara inayo tumia mtaji mdogo na inauhakika wa faida
baada ya kufanya hayo maamuzi nili anzisha biashara ya GENGE LA MATUNDA nilikuwa makini ktk kuchagua na heshima kwa wateja na kwa wakati ule wauzaji hatukuwa wengi, nilikuwa na uhakika wa ku save 30,000/= mpaka 40,000/= per day as net profit.

Kupitia genge nilikua kimtaji na duka lika imalika, nikaanza kukopesheka nikakuza biashara mpka sasa duka lipo, nimeongeza maduka mawili ya simu, na chakata mahindi nauza unga na nimefanikiwa kiasi chake kuingia kwenye soko la unga.

Mwanzo na hapo mwishoni nimefupisha kwakuwa kuandika kila kitu itakuwa ni kitabu na wasomaji wata choka.

FUNDISHO

1: Kukosa chuo hakukunifanya kuwa mnyonge na kuamua kifikilia plan B

2: Pia kuchelewa kufanikiwa isikupe shida kikubwa kutulia ktk lengo lako siku ukifanikiwa watashangaa.

3: Kuto kimbia majukumu (usiwe mbinafsi) itakufanya kunguza mzigo wa Wategemezi (wasaidie wadogo zako ili siku za mbeleni msaidiane majukumu ya familia nzima kuliko kuwa wewe peke yako kuwa nguzo ya familia)

4: Tusiwazalau hawa wafanya biashara ndogondogo najifunza mengi kutoka kwao kikubwa wewe ni kuifanya kisasa na kwa ukubwa mfano: Diamond Karanga, Azam Ukwaju. Ni biashara zilizokuepo miaka mingi ila wao wamezifanya kisasa na kwa ukubwa.

5: Tufikirie nje box ikibidi Mf: baada ya kushindwa kukuza mtaji nili fikiria Genge ingawa sikuwa najua chochote kuhusu hiyo biashara.

CHANGAMOTO

1: Kuchekwa kuwa kwanini ufanye biashara ya Genge !, note: ilikuwa mwaka 2003 na alikuwa akiheshimiwa mfanyakazi.

2: Wazazi pia waliona kama nimechanyikiwa kwakua sipendi kuwa mwalimu na waliona baadhi ya vijana tulio soma nao wanakazi na wao walitegemea mtoto wao baada ya shule waone ninakazi.

3: Kipindi nafanya kazi ya car parking unakutana na wenzako wako chuo mfano, pale IFM wewe uko nje unakatishia tiketi magari na wenzako unawaona wanasoma na wengine wamekuja na magari ya wazazi wao ina umiza ila inataka moyo.

YAPO MENGI ILA SIWEZI KUANDIKA YOTE. KAMA KUNA CHA KUJIFUNZA BASI CHUKUA.

Asante.
Kongole kwako mkuu
 
Back
Top Bottom