Unaweza kuitengeneza raha na furaha Ndani ya kambi ya mateso?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,255
Akili ya binadamu kila unapoifikirisha itakupeleka mbele katika kujua na kuongeza uwezo wa akili yako katika utambuzi na kujua mengi ambayo kabla hukuwa unayajua.

Akili ya binadamu ukiacha kuifikirisha inavia na yake na leo yake vyote vinakuwa sawa.

Hakuna kinachoongezeka sana vitakuwepo vinavyopungua.

Kila ukurasa wa kitabu unaofungua unakuongezea maarifa na ujuzi.

Na katika rehema za Allah kwa binadamu ni kuwa ubongo hauelemewi kwa kuuongezea maarifa.

Ubongo hauhisi uzito wa makilo ya kurasa unazosoma.

Sana ubongo utakusukuma usome zaidi na zaidi.

Lakini ubungo huu huu una uwezo wa kukuangamiza kwa kuidanganya nafsi na nafsi ikaamini uongo ambao akili inajua si kweli lakini nafsi ikaiaminisha akili kuwa ni kweli na akili ikaukubali kuwa ule uongo ni kweli.

Jambo limekushinda lakini ukaamini umeliweza.
Binadamu anapofikia hali hii huwa katika matatizo makubwa.

Labda tujiulize binadamu anafika vipi katika hali kama hii?

Historia inaonyesha kuwa binadamu anafika katika hali hii ya kujidanganya mwenyewe pale tamaa inapomtangulia na mengine yote akayasukuma nyuma.

Kupata kukawa ndiyo kipaumbele chake.
Hapo akili inaingia upofu na upofu huu unaambukiza nafsi na nafsi inapoteza nuru ya macho yake ikawa haioni sawasawa.

Akili kipofu na nafsi kipofu ndani ya mwili wa binadamu ni hatari kubwa.

Hatari na hasara yake ni kubwa kwa jamii nzima.

Lakini katika hasara hii wapo wachache katika wengi watapata kunufaika sana tena kwa kazi ndogo isiyohitaji kuhangaika.

Kazi hii haitoi jasho lolote kazi hii inahitaji kutii, kutia hima, na kupamba bila kufikiri.

Hali kama hii inapotokea jamii yote inakuwa kwenye dhiki na inaelekea katika kuangamia.

Mifano kama hii iko mingi katika historia ya ulimwengu na tunaweza tukajifunza kujiongezea maarifa kwani ubongo hauelemewi na kujifunza.

Wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia Manazi wa Ujerumani walizifikisha akili zao kwenye upeo wa kuzidanganya nafsi zao wakaamini mambo hii leo yanastaajabisha ukiyasoma.

Mambo hayo yakawatia upofu na uziwi wakawa hawaoni wala hawasikii.

Ikawa wao sasa wanawatesa binadamu wenzao katika namna haijapatapo kutokea duniani.

Manazi wakawa wanawatia binadamu wenzao katika matanuri wakawapulizia gesi za sumu kuwaua wakiwa na nia ya kuwamaliza wasiwepo duniani.

Hapa utajiuliza iweje haya yanafanyika na Wajerumani wengine wawe kimya?

Kitu gani kilisababisha ukimya wao?

Ujerumani iligubikwa na hofu kufungua mdomo ilikuwa kujitafutia matatizo makubwa.

Watu wakajifanya hawaoni wala hawasikii.

Upofu na uziwi ukawa umemkumba kila mtu.
Lakini taarifa zikawa zinapenya ya ule uovu ambao Manazi walikuwa wanawafanyia binadamu wenzao.

Msalaba Mwekundu walifikishiwa taarifa za kutisha na ikabidi ifanye uchunguzi kuingia Poland na kwengineko ambako Manazi walikuwa na kambi wakiwafunga watu, wakawatesa na kuwaua aidha kwa yale mateso ya kupigwa, kazi ngumu chakula kidogo au kwa kuwanyunyuzia gesi ndani ya matanuri.

Akili ya Manazi lau kama walikuwa wanajua uzito upande wao wa kuruhusu wachunguzi wa Msalaba Mwekundu kukagua hizo kambi lakini wao walijiona ni wajanja kupita watu wote.

Maandalizi ya yakafanyika kwa haraka ya kuzibadili kambi ambazo Msalaba Mwekundu wataonyeshwa.

Manazi wakalenga shule za chekechea zijengwe na watoto wafungiwe mapembea ya kuchezea na vitu vingine vya michezo ionekana kuwa hakuna shida ila ni propaganda tu.

Shule za chekechea ziwe na majiko mazuri ya kupikia na vifaa vyote viwekwe pamoja na kuwa na ghala la vyakula nk. nk.

Haya yakafanyika na kila kitu kikakamilika.

Juu ya akili zao Manazi walisahau kitu kimoja.
Huwezi kumnenepesha ng’ombe siku ya mnada.

Manazi walisahau kuwa raha na furaha imehifadhika sehemu maalum katika ubongo wa binadamu na haitengenezeki kwa kujengwa kwa mapembea na vitu vya kuchezea watoto au kuwagereshea maziwa na keki.

Haya yakafanyika na ila kitu kikakamilika kabla Msalaba Mwekundu hawajafika.

Wakaguzi wa Kinazi walishtuka walipofika kwa kuona nyuso za huzuni za walimu wa chekea wote wamesimama katika sehemu zao za kazi lakini wamenyongea vichwa wameinamisha chini.

Ndani ya chekechea ile waliokuwa wamechangamka walikuwa wenyewe Manazi Wakaguzi.

Wakaguzi wakawaambia wale walimu wawe na tabasamu.

Wale walimu wa watoto wadogo walijaribu lakini tabasamu hazikuja.

Kila wakiangalia sura za wale Manazi ndani ya uniform zao za kupendeza na miili iliyonawiri kwa chakula kizuri wao hayo yote yalizidi
kuwatia simanzi kwa kuwakumbusha ndugu zao waliouliwa kwa dhulma.

Lakini kubwa zaidi Manazi juu ya ugumu wa mioyo yao waliogopeshwa na macho ya wale watoto yalivyokuwa yakiwataza kwa mchanganyiko wa hofu na kutojua kinachoendelea.

Katika historia kama hizi kuna mengi ambayo viongozi wengi katika nchi zetu za Afrika wanaweza kujifunza.

Makofi na vifijo vya wale wanaonufaika na wao visiwadanganye.

Wajilazimishe kuzungumza na akili na nafsi zao.
Huenda ukweli ukawadhihirikia.

Raha na furaha haitengenezeki kwa geresha.
 
Maalim hapa umenikumbusha historia ya Count Bernadote na madhila yaliyompata.
 
Back
Top Bottom