Unaweza kufanya mapenzi na mwanamke aliye katika siku zake bila kupata mimba? Na sababu ni nini?

kvelia

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
246
44
Jamani msaada chonde chonde, pia kuna uwezekano wa mbegu za kiume kuishiwa nguvu hata kama ni mtu usiyefanya mapenzi mara kwa mara? Tiba yake ni nini? Naombeni michango jamani, hakuna haja ya kuzungumzia utasa.
 
ili mwanamke apate mimba surti ziungane mbegu za kiume na yai la mwanamke; mwanamke akiwa kwenye siku zake yai linakuwa limekufa hivyo hawezi kupata mimba. nguvu za kiume na mbegu za kiume zaweza kupungua au kuisha hata kama mtu hafanyi mapenzi mara kwa mara kutokana na magonjwa mbalimbali, uvutaji sigara nk.
 
Mbona kichwa cha habari na maneno hayo uliyoandika hapo juu hayaendi?, yaani nashindwa kuelewa!
Ila usijali wenzangu walioelewa mada yako watakuja kukusaidia
 
Ingawa si ustaarabu kufanya mapenzi na mwanamke aliye kwenye siku zake, pia kiimani ni haramu (naweza kusahihishwa) LAKINI Kufanya mapenzi na mtu akiwa kwenye siku zake hakuna uwezekano wa mtu huyo kushika mimba kwa sababu kwanza yai linakuwa limeshakufa na pili ukuta ulojijenga kusubiri kuotesha mtoto nao hubomoka na ndio husababisha kutoka damu during menses.

Mwanaume anapokaa muda mrefu bila kufanya mapenzi ana uwezekano mkubwa zaidi wa kutungisha mimba kwa sababu mbegu zake huwa nyingi za zilizokomaa vyema.

Matatizo ya mbegu yanaweza kuwa kiasi cha mbegu, yaani chache - oligospermia - au hazipo kabisa -azoospermia, lakini pia mbegu zaweza kuwa na abnormal shape au hata motilitiy na hivyo kusababisha matatizo kwenye urutubishaji wa yai.

Vyanzo vya matatizo ya mbegu viko vingi, kutaja vichache ni magonjwa ya korodani - kama uambukizo wa vimelea vya mumps, kuzidi joto kwenye korodani kwa mfano wale watu wanaofanya kazi kwenye mazingira ya joto ya muda mrefu au wale ambao mishipa ya damu kwenye korodani itavimba (Varicoceles) na kusababisha damu kuongezeka na hivyo kuongeza joto. Uvutaji wa sigara na matumizi ya dawa za kulevya pia kunaweza kuathiri quality au quantity ya sperms. Upasuaji kwenye korodani au wa hernia husababisha kuharibu njia za usafirishaji wa sperms. Yapo pia matatizo ya kuzaliwa ambayo huathiri utengezaji wa mbegu au kutokuwepo kabisa kwa mashine za kutengeneza mbegu. Saa nyingi vivimbe kwenye ubongo vyaweza kusababisha mfumo wa hormones unaosaidia utengenezaji wa mbegu kuharibika hivyo kuharibu utengenezaji wa mbegu.

Nakushari nenda hospitali upate vipimo, utatibiwa kulingana na tatizo litakaloonekana.
 
Only if ur body has gone against normal physiology of menstruation.

ni kweli, na maelezo hayo niliyapata hapa...

Naomba nitoe mifano hai kwa faida ya dada zetu na wengine:

1. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 22 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa chini:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd.

Kisha ahesabu kuanzia ile 22nd day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 8th day ya kalenda yake. Hivo 8th day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 22. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!

2. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 28 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa chini:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th.

Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 14th day. Inamaana kwamba 14th day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 28. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!

3. Kama mwanamke ana menstration cycle ya siku 35 inabidi afanye kama ifuatavo: Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa chini:

1st
, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th, 29th, 30th, 31st, 32nd, 33rd, 34th, 35th.

Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 21st day. Inamaana kwamba 21st day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 35. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!

4. Kama mwanamke ana abnormal menstration cycle ya siku 15 , BASI KUNAUWEZEKANO WA KUTOPATA MIMBA KABISA KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI:

Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama kawaida:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th.

Kisha ahesabu kuanzia ile 15th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15. Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 1st day. Inamaana kwamba, the 1st day of her bleedind ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 15. Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed, na ndiyo hiyo hiyo siku ambayo mwanamke wa kundi hili anaweza kupata mimba!

Hii inamaana kwamba, siku ambayo linaharibika lile yai la upande mmoja ndiyo siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili linapevuka tayari kwa kurutubishwa. Mwanamke wa aina hii anaweza kupata mimba tu kama atakutana na mwanaume siku ile anayoanza kubleed, kwani siku ambayo yai moja linaanza kuharibika ndio siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili linakuwa tayari kurutubishwa!

Na wanawake wa kundi hili la nne ukiwauliza vizuri watakiri kwamba hawajawahi kuona au ku-feel ule ute mweupe ambao wenzao huwa wanaupata siku ile yai linapokuwa tayari kwa kurutubishwa, kwani ute wa wanawake wa kundi hili la nne huwa unachanganyikana na damu kwa vile unatoka siku ile ile wanapoanza ku-bleed. Pia wanawake wa kundi hili huwa wanatokwa na kiasi kidogo sana cha damu; na bleed hukatika ndani ya siku moja au mbili tu!

Jambo la kushangaza ni kwamba, wanawake wengi hawana knowledge ya kutosha juu ya hili suala la siku ya mimba; hasa wale ambao wana menstration cycle inayobadilikabadilika! Wao husitukia tu wameanza ku-bleed. Ndo maana hawawezi hata ku-plan kutopata mimba! Hawana ujanja kabisa ndio sababu wengi wanatumia sindano na njia zingine nyingi za artificial ambazo mwisho wa siku huwaletea matatizo ya uzazi, kwani nyingi hu-block njia ya uzazi! Nimeona wengi wenye matatizo ya uzazi unaosababishwa na hizi artificial family planning. Wengine hulazimika kwenda hospital kuzibuliwa ili wapate mimba jambo ambalo ni hatari kwa afya zao!
 
ni kweli, na maelezo hayo niliyapata hapa...
4. Kama mwanamke ana abnormal menstration cycle ya siku 15 , BASI KUNAUWEZEKANO WA KUTOPATA MIMBA KABISA KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI:

Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama kawaida:

1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th.

Kama ikitokea mama ana cycle fupi kama hii ni kweli anaweza kuovulate wakati ana-menstruate, but as far as I know majority of people, if not all, have normal cycles ranging from 21 - 35 days with a mean at 28 days, hii ikimaanisha ovulation kwa yule mwenye cycle ya 21 days itatokea siku ya saba ya tangu aanze menses (yaani siku ya kwanza ya Luteal phase- zile siku 14 za mwisho za mzunguko wa hedhi), so kwa wale wanaopata siku zao kwa siku saba wanaweza kujikuta wanaovulate wakiwa kwenye siku yao ya mwisho ya menses and this means bado watakuwa na siku mbili ambazo ni fertile, yaani siku ya nane na tisa ambazo hawako kwenye menses na wanaweza kushika mimba.

It is abnormal yes to have cycle of less than 21 days and these people might also have problems with ovulation and therefore a problem with fertility. It is not that all women who are menstruating are ovulating. there are other cycles that are anvolutory (cycle ambazo mayai hayapevuki). Kutopevusha yai kunatokana na kukua kwa follicles bila kutokea kwa follicle itakayopevusha yai (dorminant follicle) hii inaweza kutokana na kutokuwepo kwa uwiano kati ya hormone za oestrogen na Follicle stimulating hormone ambazo uwiano wake ndio husababisha kutokea kwa dorminant follicle itakayopevusha yai.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba mahesabu ya cycle ya 15 juu ni sahihi lakini this is abnormal na huyu mtu anaweza pia kuwa na matatizo ya kuovulate kwa hiyo upataji wake mimba hata akiwa kwenye menses (anovulatory) ni ngumu.
 
Kuna wengine hupata ovulation kipindi cha bleed.. mimba inawezekana kabisa.

Nakubaliana nawe sana tu - Kapoloto anazungumza nadharia zaidi. Nina mfano wa couples ambao waliishi miaka 10 bila mtoto na kuachana. mke alipata boy friend aliyekuwa anaishi mbali hivi hivyo onana yao ilikuwa si ya mara kwa mara. Boy friend alikuja bibie akiwa siku zake na jamaa kwa vile ilibidi arudi atokako alimuomba bibie waonane kimwili hivyo hivyo akiwa bleed. Baada ya kufanya hivyo bibie kama ndoto alidaka mimba. Isingewezekana kwa mumewe wa kwanza kwa kile kinachoeleweka kuwa kuonana kimwili na mkeo akiwa katika siku zake za kubleed ni unethical.
 
Hujamuelewa kapotolo, hazungumzii nadharia, anazungumzia reality, sijakataa kwamba mtu hawezi kupata mimba wakati anableed, soma vizuri mabandiko yangu yote.

Mizunguko mifupi chini ya siku 21 ni abnormal, na mtu huyu mwenye hii abnormality anaweza ku-ovulate wakati anableed na akapata mimba ingawa implantation inaweza kuwa ngumu kwa sabababu while the woman ovulate and the egg is fertilized, the endometrium is shedding, so where will the embryo be implanted?. Though disease do not read books BUT chance of conception while menstruating is difficult. Wanaoelewa nadhani wamenielewa.
 
Hujamuelewa kapotolo, hazungumzii nadharia, anazungumzia reality, sijakataa kwamba mtu hawezi kupata mimba wakati anableed, soma vizuri mabandiko yangu yote, mizunguko mifupi chini ya siku 21 ni abnormal, na mtu huyu mwenye hii abnormality anaweza ku-ovulate wakati anableed na akapata mimba. Wanaoelewa nadhani wamenielewa.

ok. ni sawa nimekuelewa mkuu. unajua hata nasi hatukumchukulia seriously huyo mama aliposimulia baada ya kupata mimba akiwa katika hali ile.
 
Kama ikitokea mama ana cycle fupi kama hii ni kweli anaweza kuovulate wakati ana-menstruate, but as far as I know majority of people, if not all, have normal cycles ranging from 21 - 35 days with a mean at 28 days, hii ikimaanisha ovulation kwa yule mwenye cycle ya 21 days itatokea siku ya saba ya tangu aanze menses (yaani siku ya kwanza ya Luteal phase- zile siku 14 za mwisho za mzunguko wa hedhi), so kwa wale wanaopata siku zao kwa siku saba wanaweza kujikuta wanaovulate wakiwa kwenye siku yao ya mwisho ya menses and this means bado watakuwa na siku mbili ambazo ni fertile, yaani siku ya nane na tisa ambazo hawako kwenye menses na wanaweza kushika mimba.

It is abnormal yes to have cycle of less than 21 days and these people might also have problems with ovulation and therefore a problem with fertility. It is not that all women who are menstruating are ovulating. there are other cycles that are anvolutory (cycle ambazo mayai hayapevuki). Kutopevusha yai kunatokana na kukua kwa follicles bila kutokea kwa follicle itakayopevusha yai (dorminant follicle) hii inaweza kutokana na kutokuwepo kwa uwiano kati ya hormone za oestrogen na Follicle stimulating hormone ambazo uwiano wake ndio husababisha kutokea kwa dorminant follicle itakayopevusha yai.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba mahesabu ya cycle ya 15 juu ni sahihi lakini this is abnormal na huyu mtu anaweza pia kuwa na matatizo ya kuovulate kwa hiyo upataji wake mimba hata akiwa kwenye menses (anovulatory) ni ngumu.

mbona inaonekana kama vile watu hatupigii mahesabu ya persistance ya mbegu x na y.? Kwa mfano mtu wa mzunguko wa cku 15, akakutana kimwili na mwanaume cku ya 14, that means mpaka kufikia cku ya kwanza ambayo ni cku ya kuovulate mbegu x toka kwa mwanaume zitakuwa bado hai na nadhan ukuta wa mimba unaweza usibomoke.
 
mi naomba kuuliza unaanza kuhesabu ukimaliza brd siku inayofuata au unaanza kuhesabu siku hiyo utakayomaliza brd ndo inakuwa ya kwanza then mi sielewi kama ninamzunguko mrefu au mfupi coz mez wa 3 niliingia date 21 na wa 4 date 21 ila wa 5 ikabadilika nikapata date 26 inakuwaje hapo
 
huyu ameandika mada mbili tofauti, ya kwanza ni katika kichwa cha habari na ya pili katika hayo aliyoyaandika baada ya kichwa hicho...mimi si mtaalamu wa mambo haya ila nimejaribu kukuelewesha tu ili kama una msaada msaidie.
Mbona kichwa cha habari na maneno hayo uliyoandika hapo juu hayaendi?, yaani nashindwa kuelewa!
Ila usijali wenzangu walioelewa mada yako watakuja kukusaidia
 
MWenzenu mie sijui kitu, sibadili tarehe always24. sasa nisaidieni niko kweye mzunguko mrefu au mfupi?
 
Jamani msaada chonde chonde, pia kuna uwezekano wa mbegu za kiume kuishiwa nguvu hata kama ni mtu usiyefanya mapenzi mara kwa mara? Tiba yake ni nini? Naombeni michango jamani, hakuna haja ya kuzungumzia utasa.

Dr. Matunge yuko Yombo vituka, anapatikana kwenye namba 0782000091
 
mi naomba kuuliza unaanza kuhesabu ukimaliza brd siku inayofuata au unaanza kuhesabu siku hiyo utakayomaliza brd ndo inakuwa ya kwanza then mi sielewi kama ninamzunguko mrefu au mfupi coz mez wa 3 niliingia date 21 na wa 4 date 21 ila wa 5 ikabadilika nikapata date 26 inakuwaje hapo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom