Unaweza kufanya kazi ya kuihudumia jamii (Mwalimu, Polisi, Daktari) ndani ya eneo/kijiji ulichozaliwa?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
14,776
2,000
Habari za muda huu jamiiforums.

Unawezaje kufanya kazi ya kuihudumia jamii (Mwalimu, Polisi, Daktari) ndani ya eneo/kijiji ulichozaliwa pasipo kupata lawama za ndugu, jamaa na marafiki?

Jenga picha umemaliza chuo kikuu mwaka 2008 na kisha kuajiriwa mwaka 2009 na ilipofika mwaka 2020 umepanda daraja na kwenda kuwa mkuu wa shughuli za Ualimu, Polisi (OCD) au Udaktari (DMO) ndani la Wilaya uliozaliwa.

Ninapoongelea Wilaya za mikoani usifananishe na Wilaya za majiji makuu kama Dar na Mwanza. Wilaya za Mikoa kama Mara au Kilimanjaro unaweza kuta 98% ya wakazi wake ni watu wa kabila moja tu.

Kama ni Wakurya basi hapo ni mwendo wa majina ya akina Chacha, Wambura, Mwita, Bhoke au kama ni Wachagga basi ni akina Massawe, Tesha, Muro, Mushi sio ndani ya viti vya daladala pekee hapana bali hata, katika viti virefu vya maeneo yetu yaaaaleeee (moja moto moja baridi - hahahahaaaa najua hapa mzee baba mrangi amenielewa) sokoni mpaka mashuleni.

Unawezaje kufanya kazi ndani ya eneo ulilozaliwa pasipo kupata lawama za ndugu, jamaa na marafiki zako wa muda mrefu, possibly wengine ulisoma nao? Hivi unaijua dhahama ya kuwa mkuu wa kituo cha Polisi (OCS) ndani ya eneo fulani kisha ukaona ndugu yako wa karibu anakabiliwa na kesi ya ulawiti au mauaji?

Hivi unajua inavyokera unapokuwa mwalimu mkuu wa shule fulani kisha mtoto wa binamu anakuja kuandikishwa darasa la kwanza dakika za mwisho nafasi zikiwa zimeisha? Hili neno "nafasi zimeisha au zimejaa" unalijua wewe mkuu wa shule ila taarifa zitakazoenea kijijini ni kuwa "mtoto wa mzee Mwakapala yule mkuu wa shule tuliyekuwa tunaenda naye kuwinda zamani amekataa kutusaidia".

Isiishie hapo tu, hivi unajua changamoto wanazopitia wakuu wa huduma za afya wa Wilaya (DMOs) wanaofanya kazi maeneo walikozaliwa? Wewe haujui, sasa ngoja nikwambie. Ikitokea mjomba wa DMO anaumwa kichwa au malaria tu ya kawaida, basi atafunga safari kwa baiskeli huuyoooooo mpaka mjini kwa mtoto wa dada yake kwenda kumuomba Panadol.

Tena pasipo kujua kwamba DMO yupo kiutawala zaidi na sio matibabu ya moja kwa moja, utasikia anamwambia nesi "sitaki uniguse, nataka kutibiwa na mtoto wa dada yangu".

Yaaani anataka DMO atoke ofisini kisha afunge safari mpaka hospitali kuu ya wilaya, ilhali huko atokako ameacha zahanati na vituo vya afya ambavyo vingeweza kumpa huduma stahiki kulingana na tatizo lake, ila yeye akaona kwa kuwa mtoto wa dada yake ameletwa wilayani kama boss basi yeye huyoooo kwenda kuchuma lawama.

Unakuta mtu angeweza kuepuka jinai ya ulawiti kwa kuweka kuoa mapema, ila akajua kuwa mtoto wa kaka yake ni OCD au OCS ndani ya wilaya yake, basi anaamua tu kula mzigo watoto wa shule bila noma.

Binamu anajua kuwa ndugu yake ni Mwalimu mkuu wa shule, basi apeleke watoto mapema wapate kuandikishwa darasa la kwanza, ila anasubiri mpaka tarehe ya mwisho ndio apeleke watoto shule, kisa mtoto wa mjomba yake ndio mkuu wa shule au afisa elimu wa wilaya.

It's very challenging. Juzi hapa nilisikia kuna mkuu mmoja wa Wilaya alimkamata mtoto wa ndugu yake (bila shaka ni binamu) akiwa na wenzie wametoka kuchoma mkaa. Mkuu wa wilaya (DC) baada ya kumuona ndugu yake yumo ndani ya lile kundi akashtuka sana.

Akamuuliza "yaaani kumbe hata wewe unafanyaga uhalifu huu?" Yule ndugu akajibu "ndio binamu, sasa unafikiri nisipofanya hivi, watoto watakula nini?". Alichokifanya mkuu wa Wilaya akaamua kutoa msamaha kwa wale vijana wote ila akawaonya wasirudie tena.

Sasa jenga picha kama atakuja kumkamata kwa mara ya pili ataweza kumuachia tena? Kama atamuachia, je misitu ndani ya wilaya hiyo itaendeleka kukatwa mpaka lini? Vipi endapo atamshughulikia, ndugu wa ukoo, jamaa na marafiki watamuangalia kwa jicho gani.

Kufanya kazi ya kuhudumia jamii ndani ya kijiji/eneo ulilozaliwa ni changamoto na lawama kwa ndugu. Je, yaliwahi kukukuta?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,965
2,000
Habari za muda huu jamiiforums.

Unawezaje kufanya kazi ya kuihudumia jamii (Mwalimu, Polisi, Daktari) ndani ya eneo/kijiji ulichozaliwa pasipo kupata lawama za ndugu, jamaa na marafiki?

Jenga picha umemaliza chuo kikuu mwaka 2008 kisha alipofika mwaka 2020 umepanda daraja na kwenda kuwa mkuu wa shughuli za Ualimu, Polisi (OCD) au Udaktari (DMO) ndani la Wilaya uliozaliwa?

Ninapoongelea Wilaya za mikoani usifananishe na Wilaya za majiji makuu kama Dar na Mwanza. Wilaya za Mikoa kama Mara au Kilimanjaro unaweza kuta 98% ya wakazi wake ni watu wa kabila moja tu.

Kama ni Wakurya basi hapo ni mwendo wa majina ya akina Chacha, Wambura, Mwita, Bhoke au kama ni Wachagga basi ni akina Massawe, Tesha, Muro, Mushi sio ndani ya viti vya daladala pekee hapana bali hata, katika viti virefu vya maeneo yetu yaaaaleeee (moja moto moja baridi - hahahahaaaa najua hapa mzee baba mrangi amenielewa) sokoni mpaka mashuleni.

Unawezaje kufanya kazi ndani ya eneo ulilozaliwa pasipo kupata lawama za ndugu, jamaa na marafiki zako wa muda mrefu, possibly wengine ulisoma nao? Hivi unaijua dhahama ya kuwa mkuu wa kituo cha Polisi (OCS) ndani ya eneo fulan kisha ukaona ndugu yako wa karibu anakabiliwa na kesi ya ulawiti au mauaji?

Hivi unajua inavyokera unapokuwa mwalimu mkuu wa shule fulani kisha mtoto wa binamu anakuja kuandikishwa darasa la kwanza dakika za mwisho nafasi zikiwa zimeisha? Hili neno "nafasi zimeisha au zimejaa" unalijua wewe mkuu wa shule ila taarifa zitakazoenea kijijini ni kuwa "mtoto wa mzee Mwakapala yule mkuu wa shule tuliyekuwa tunaenda naye kuwinda zamani amekataa kutusaidia".

Isiishie hapo tu, hivi unajua changamoto wanazopitia wakuu wa huduma za afya wa Wilaya (DMOs) wanaofanya kazi maeneo walikozaliwa? Wewe haujui, sasa ngoja nikwambie. Ikitokea mjomba wa DMO anaumwa kichwa au malaria tu ya kawaida, basi atafunga safari kwa baiskeli huuyoooooo mpaka mjini kwa mtoto wa dada yake kwenda kumuomba Panadol.

Tena pasipo kujua kwamba DMO yupo kiutawala zaidi na sio matibabu ya moja kwa moja, utasikia anamwambia nesi "sitaki uniguse, nataka kutibiwa na mtoto wa dada yangu".

Yaaani anataka DMO atoke ofisini kisha afunge safari mpaka hospitali kuu ya wilaya, ilhali huko atokako ameacha zahanati na vituo vya afya ambavyo vingeweza kumpa huduma stahiki kulingana na tatizo lake, ila yeye akaona kwa kuwa mtoto wa dada yake ameletwa wilayani kama boss basi yeye huyoooo kwenda kuchuma lawama.

Unakuta mtu angeweza kuepuka jinai ya ulawiti kwa kuweka kuoa mapema, ila akajua kuwa mtoto wa kaka yake ni OCD au OCS ndani ya wilaya yake, basi anaamua tu kula mzigo watoto wa shule bila noma.

Binamu anajua kuwa ndugu yake ni Mwalimu mkuu wa shule, basi apeleke watoto mapema wapate kuandikishwa darasa la kwanza, ila anasubiri mpaka tarehe ya mwisho ndio apeleke watoto shule, kisa mtoto wa mjomba yake ndio mkuu wa shule au afisa elimu wa wilaya.

It's very challenging. Juzi hapa nilisikia kuna mkuu mmoja wa Wilaya alimkamata mtoto wa ndugu yake (bila shaka ni binamu) akiwa na wenzie wametoka kuchoma mkaa. Mkuu wa wilaya (DC) baada ya kumuona ndugu yake yumo ndani ya lile kundi akashtuka sana.

Akamuuliza "yaaani kumbe hata wewe unafanyaga uhalifu huu?" Yule ndugu akajibu "ndio binamu, sasa unafikiri nisipofanya hivi, watoto watakula nini?". Alichokifanya mkuu wa Wilaya akaamua kutoa msamaha kwa wale vijana wote ila akawaonya wasirudie tena.

Sasa jenga picha kama atakuja kumkamata kwa mara ya pili ataweza kumuachia tena? Kama atamuachia, je misitu ndani ya wilaya hiyo itaendeleka kukatwa mpaka lini? Vipi endapo atamshughulikia, ndugu wa ukoo, jamaa na marafiki watamuangalia kwa jicho gani.

Kufanya kazi ya kuhudumia jamii ndani ya kijiji/eneo ulilozaliwa ni changamoto na lawama kwa ndugu. Je, yaliwahi kukukuta?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Hapo ndipo ninapoona Tz, au WaTz bado tunagaragara kwenye Umasikini na Ujinga.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom