Unaweza kudumu na kuishi maisha ya furaha na mwenza wako

Ornate

Member
Jul 13, 2021
26
33
Hivi unakumbuka mara ngapi ulishawahi kumwambia maneno mazuri mwenza wako na yakamkosha hadi akafurahi? Hakuna Siri ya kwanini fulani amedumu na ana furaha katika maisha yake ya mapenzi.

Unaweza kufanya vitu mbalimbali ili kuhakikisha unakuwa na unaishi kwa furaha na kudumu katika mapenzi yako. Nilipata wasaa wa kuzungumza na mmoja kati ya wanandoa ambaye alinieleza kuwa "Nilipo olewa ndipo nilipogundua kuwa mume wangu alikuwa hajatulia kabisa,nikatafuta njia ya kumfanya atulie na mimi nipate furaha katika ndoa yangu. Nilifikiria sana lakini kuna siku wakati tumekaa usiku nikaamua kumwambia kuwa, nampenda na sitaki kuwa sababu ya mume wangu kuyachukia mapenzi ila yeye ndo awe sababu ya Mimi kuyachukia mapenzi, na nikamuuliza vipi kwa upande wake anapenda kuwa sababu ya Mimi kuyachukia mapenzi?"

Aliendelea kwa kusema "kiukweli nikaona sura yake imebadilika hivi na akawa kama ana mawazo na namshukuru Mungu kuanzia hapo alinipa heshima na sasa naifurahia ndoa yangu"

Mapenzi yanahitaji ustadi sana, jaribu kumfanya mwenzi wako kuwa mtu wako wa karibu, unapohisi umekwama katika kitu fulani au una jambo kubwa linalokutatiza, jaribu kumshirikisha ili upate ushauri kwa kufanya hivyo pia, itampa nafasi mwenza wako kujihisi na yeye ni miongoni mwa watu wake wa karibu na utaweza kumtengenezea furaha na aendelee kukuheshimu.

Tenga muda wa kukaa naye na kufurahia maisha, hata kama hauna muda wa kutosha au kazi zimekubana, jaribu kupata muda kwa kuzungumza na mwenza wako, kwa kwenda sehemu za utulivu lakini pia hata kwa kukaa nyumbani ili muweze kuongea na kubadilishana mawazo, ukaribu wako kwako kutapunguza nafasi ya mwenza wako kukusaliti.

Lakini pia, mchangamshe kwa zawadi mbalimbali kama vile maua na vingine vingi, hata kama hauna pesa za kutosha ila kidogo ulichonacho kitaongeza kitu katika mapenzi yako. Tusisubiri kutafuta mchawi katika mapenzi ila tunaweza kujitibia wenyewe
 
Ujakutana na maopportunist wao ata ufanye nn hawezi kukupenda zaid ya kulenga faida na kukuigizia tu.

NB: opportunists wapo pande zote ke &me chukua tahadhari
 
FB_IMG_1649124455930.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom