Unaweza kuanzisha uhusino kwenye mitandao ya kijamii?

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Wana JF.
Uhusiano wa kimapenzi ndio ambao huzaa ndoa baadae.

Lakini vijana wengi sana wamekuwa hawajui ni sehemu gani sahihi ya kumpata mweza wa kweli.

Hili limekuwa ni swali gumu ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza pasipo kupata majibu. Kutokana na utandawazi uliyopo hivi sasa, pamoja na matumizi yasio sahihi ya utandawazi yanafanywa hivi sasa.

Wengi wamejikuta wakipata wenza wasio sahihi na wapo waliopata wenza sahihi kupitia mitandao ya kijamii, hivi ni sahihi kuanzisha uhusiano na mtu uliyekutana naye katika mitandao ya kijamii?
Wadau tujadili hii
 
usahihi wake unategemea na jinsi ulivyojipanga katika kumtafuta huyo mwenza, lazima kuwe na muda wa kujuana kabla ya kutangaza ndoa
 
mh?sijui mwaya,
labda walofanikiwa kupata wenza kupitia mitandaoni waje hapa watuambie.
 
mpaka unatafuta wenza mitandaoni...lazma huto mtu ana matatizo fulani!
 
Sio sahihi. Ni njia nzuri ya kukutana na watu na unapoona kuna mtu mna interest zinazo fanana then mnapelekana kwenye njia za kawaida (dates etc) alafu ambazo ni njia pekee ya kujua kama mnamatch.
 
Hahaha hakuna matatizo ktk hilo,basi hao wanaojifanya wanamjua sana Mungu kwa kuzuga wanakwenda misikiti/makanisani ndio wana siri za ajabu ajabu ndio maana wanakimbilia ktk nyumba za ibada kuficha machafu yao. Da Shosti mtu akikutokea toka naye.
mhhhh kazi wanayo...mie nshawahiwa uzuri wenyewe
 
i think mwenza anweza patikana popote pale ,nategemeana na watu wenyewe wapo serious kwa kiasi ganai wanweza kukutana hata vichochoroni na wakawa wanamaanisha kuwa pamoja na wanaweza kukutan hat makanisan au misikitin na wasiwe serious kwenye mahusiano hayo.
Sopopote pale mahusinano yanaweza kuanzisha no matter wat............
 
kuna sehemu nyingi sana watu hukutana na kuanzisha mahusiano zamani watu walikutana disco, kanisani , kwenye sherehe mbalimbali etc lakini kwa sasa kuna mitandao ya kijamii kama facebook, etc..
kwa sasa mapenzi mengi huanzishwa kwa msukumo wa kingono zaidi kuliko uhalisia ndo maana wengi wao hawadumu au hawana fursa ya kufahamiana zaidi au kuelewana
 
Mimi nadhani uhusiano unaweza kuanza kwa wawili hao kukutana popote iwe kanisani, msikitini, mtandaoni nk. Sababu hata kama mkikutana kanisani haimaanishi ndiyo mtakuwa mmefahamiana in and out kwa siku hiyo. Muhimu ni kupeana muda wakufahamiana na kuona kama mna make good chemistry. Mitandaoni wapo watu wa aina zote ambao ni hao hao tunaopishana nao mijini, kwenye mikusanyiko, maofisini, kwenye nyumba za ibada nk. Tatizo watu wengi hasa wanaume wakishaanza kuwasiliana tu na msichana within one week wanapanga appointment zakwenda guest hapo possibility yakuangukia pua ni kubwa. Kwahiyo Chatu dume kama umempata wa mtandaoni take time to know her and see if at all she is the woman of your dream. Good lucky



Wana JF.
Uhusiano wa kimapenzi ndio ambao huzaa ndoa baadae.

Lakini vijana wengi sana wamekuwa hawajui ni sehemu gani sahihi ya kumpata mweza wa kweli.

Hili limekuwa ni swali gumu ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza pasipo kupata majibu. Kutokana na utandawazi uliyopo hivi sasa, pamoja na matumizi yasio sahihi ya utandawazi yanafanywa hivi sasa.

Wengi wamejikuta wakipata wenza wasio sahihi na wapo waliopata wenza sahihi kupitia mitandao ya kijamii, hivi ni sahihi kuanzisha uhusiano na mtu uliyekutana naye katika mitandao ya kijamii?
Wadau tujadili hii
 
Eti kwa nini usiweke sura yako ama kitu kingine,unaweka sura ya mtu inakuwaje,hasa huyo Denzel Washington.
 
Back
Top Bottom