Unaweza Kuamini Hii?!, Pamoja na Juhudi Zote za Rais Magufuli Kuleta Maendeleo Kwa Kusisitiza Ukweli Daima, Lakini Bado Anadanganywa Mchana Kweupe!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,440
113,448
Wanabodi,
Kuna hii video clip ni ya kipindi cha nyuma, ila mimi ndio nimeisikiliza leo, naomba na wewe isikilize halafu uniambie hayo yanayozungumzwa humu kama yanaweza kuwa ni kweli?!.

Mimi nimemsikiliza huyu Meya wa Jiji la Mwanza, Mtahiki James Bwire, hivi huyu kweli haya anayoyasema kwenye video hii ni kweli yametokea?, mimi bado siamini, huyu jamaa lazima atakuwa ni muongo huyu, anawasingizia tuu maofisa wa serikali, kuanzia Mkuu wa Mkoa, RPC na RTO.

Hivi kweli unaweza kuamini tuhuma hizo?!. Yaani pamoja na juhudi zake zote za Rais wetu mpende, Dr. John Pombe Joseph Magufuli katika kuleta maendeleo ya Taifa letu hili ambalo kwa muda mrefu lilifanywa ni shamba la bibi, hadi Rais Magufuli alipoingilia kati, kwa kuwasisitiza viongozi na wananchi tuchape kazi na kuwa wakweli daima, tena kwa jinsi rais Magufuli mwenyewe alivyo mkweli daima na alivyo mkali pale anapodanganywa, kweli unaweza ukaamini bado anaweza akatokea ofisa yoyote wa serikali hii ya Awamu ya Tano, akamdanganya rais Magufuli na kuwadanganya umma wa Watanzania tena mchana kweupe kwenye kadamnasi ya watu, kuwa maendeleo fulani yamepatikana, kumbe ni uongo!. Kweli kuna ofisa yoyote wa umma anaweza uthubutu kumdanganya rais Magufuli mchana kweupe hivi kama anavyotuhumu huyu Meya?!.
Mimi siamini!. Huyu Meya, atakuwa ni muongo huyu!.

Msaada kwa wale wavivu kuangalia video. Kwenye video hiyo inamuonyesha Meya wa jiji la Mwanza, anadai kuwa amekusanya ushahidi wa jinsi rais Magufuli anavyo danganywa na watendaji wake, akatolea mfano wa mradi fulani wa maji uliozinduliwa wakati wa Mwenge, kuwa mradi huo haujawahi kutoa maji hata tone, lakini baada ya kutafuna fedha za mradi, mradi hautoi maji, lakini ili kudanganya, viongozi wakawabebesha maji wanavijiji kwa kubebelea, na kujaza kwenye tanki manually. Mwenge ulipofika, mradi ukazinduliwa, maji yakafunguliwa, yakatoka, watu wakapiga makofi, wakashangilia, RC anajua kilichofanyika, DC anajua kilichofanyika, RSO anajua, DSO anajua, yaani rais wa JMT anadanganywa mchana kweupe huku watu wanajua lakini wame mute tuu!.

Baada ya kupokea taarifa ya ujio wa Rais Magufuli kuja Mwanza kwa ndege, Mstahiki Meya akapanga kuwalipua viongozi hao kwa rais Magufuli kuwa Anadanganywa!.

Kumbe inteligensia ya mkoa pia iko makini. Siku ya kuwasili kwa rais Magufuli jijini Mwanza, Mstahiki Meya huyo akawa wa kwanza kufika airport kumpokea rais Magufuli.

Masikini Mstahiki Meya huyo, hana hili wala lile, kabla rais Magufuli hajatua, Meya huyo alisombwa mzobe mzobe na kuwekwa lockup ya uwanja wa ndege, na baadae kuhamishiwa kituo kikuu cha mkoa na kufungiwa hadi rais Magufuli aondoke Mwanza, ili kuhakikisha rais Magufuli asijue wala asisikie jinsi anavyodanganywa na watendaji wake.

Kwa vile mimi simuamini kabisa huyu Meya kuwa anasema kweli, lakini kwasababu amezitoa tuhuma hizi public nashauri tuhuma hizi zifanyiwe kazi, ikithibitishwa ni uzushi, huyu Meya kwanza atiwe ndani na sheria ichukue mkondo wake.
Hoja za Mstahiki Meya huyu ni hizi zifuatazo
  1. Amealikwa rasmi kushiriki mapokezi ya rais. Jee mtu aliyealikwa rasmi kushiriki mapokezi ya Mhe. Rais, anaweza kukamatwa ili kumzuia asimpokee rais ili ukweli wake usijulikane?.
  2. Huyu jamaa alikamatwa kwa kuelezwa yuko chini ya ulinzi twende kituoni bila kuelezwa kosa lake.
  3. Alipofikishwa kituo cha Airport, aliwekwa chini ya ulinzi bila kuelezwa kosa wala kuulizwa chochote kwa maelezo ni amri kutoka juu!.
  4. Kumbe huu sasa ndio utaratibu mpya wa Jeshi letu la polisi linaweza kumkamata mtu na kumsweka ndani bila kumweleza kosa lake au bila ya maelezo yoyote?.
  5. Baadaye wakaja askari watatu, wakamhamishia kituo cha kati. Mtu anaweza kushikiliwa kituo kimoja cha polisi bila rekodi yoyote na kuhamishiwa kituo kingine ndiko akaandike maelezo?.
  6. Akiwa njiani kuhamishwa kutoka kituo cha polisi cha Uwanja wa ndege, kuhamishiwa kituo cha kati, ndipo akaelezwa, kuwa taarifa za kinteligensia zimeliarifu jeshi la polisi kuwa Meya huyo alipanga kufanya kitu kibaya kwenye ziara ya Mhe. Rais Magufuli.
  7. Askari hao wakamweleza kuwa wao wameelekezwa na RCO, wamkamate. Eti askari hao pia wakamweleza kuwa RCO ameelekezwa na RPC, RPC ameelekezwa na RC!, hivi huu sasa ndio utendaji wa jeshi letu la polisi, RCO akiwaeleza vijana wake wakamkate mtuhumiwa fulani kufuatia taarifa za kiinteligensia, polisi mkubwa, RCO, akitoa amri kumkata mtuhumiwa kwa ma juniors wake, pia huwaeleza kuwa hii amri imetoka kwa RPC, RPC nae kaelezwa na RC, na kwa vile RC ndio mkuu wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, wanaolewa utendaji wa serikali, mtakuwa mnaelewa taarifa hiyo ya kiiteligensia itakuwa imetokea wapi!, kweli watu wote hawa wanaweza kweli ku collude rais adanganywe mchama kweupe na kuzuia rais Magufuli asiupate ukweli?.
  8. Alipofika kituoni, ndipo akachukuliwa maelezo. Baadae RCO akaja akamruhusu kutafuta mdhamini na akadhaminiwa na kuachiwa, ila pia RCO akamweleza mambo ya ajabu sana!. Kweli RCO anaweza kumweleza mtuhumiwa wa uhalifu mambo hayo RCO aliyomweleza?.
  9. Mtahiki Meya anasema katika nchi hii, ukiwa mkweli kutetea rasilimali za taifa, dhidi ya viongozi mafisadi, utapata changamoto sana!, jee hii ni kweli?.
  10. Kosa lake ni yeye kama Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani, wamebaini ubadhirifu kwenye baadhi ya miradi, wakamweleza RC aunde tume ya uchunguzi, RC aka mute!. Hizi ndizo tuhuma zenyewe
  11. Mradi wa Maji wa Buhongwa, fidia imetolewa imelipwa lakini wananchi, hawajafidiwa!.
  12. Mradi huo hauna value for money, fedha nyingi zimetumika, lakini hakuna kilichofanyika!. Mpaka leo umetumia TZS zaidi ya milioni 800, lakini mpaka leo, hakuna hata tone moja la maji lilitoka!.
  13. Wakati wa mbio za Mwenge, wananchi wamesomba maji kutoka kijiji cha Fumagila na kuja kuyajaza tanki la Buhongwa kisha mradi ukazinduliwa.
  14. Ujenzi holela mjini, building permit inalipiwa TZS milioni 50, lakini fedha hizo hazionekani zinakwenda wapi?!.
  15. Sheria ya mipango miji inataka majengo ya mjini kati yawe zaidi ya ghorofa mbili, lakini watu wanapewa permits wananga frames tuu as long as wanalipa hiyo milioni 50!.
  16. Meya amesisitiza atasema kweli daima!, kazi yake ni kumsaidia Mhe. Rais kusukuma maendeleo, atakayemuona mbaya na amuone mbaya, anamtafuta rais Magufuli amweleze jinsi anavyodanganywa na watendaji wake.
  17. Rais Magufuli, anajituma sana, anahangaika kuleta maendeleo, hawezi kufanya kila kitu peke yake lazima asaidiwe, sasa badala ya viongozi kumsaidia rais, wao wanatafuna pesa na kumdanganya rais!.
  18. Meya anamtaka rais Magufuli kuliangalizia jiji la Mwanza, hao viongozi wanaomzunguka, wengine wanamdanganya kuonyeshea mambo ni super, mambo ni mazuri, kumbe ndio hao hao wanaomdanganya.
  19. Mstahiki Meya alipolishikia hili kidedea, madiwani wakashawishiwa wapige kura ya kutokuwa na imani na Mtahiki Meya ili aondolewe!.
  20. Unapotetea mali za wananchi, unaonekana mbaya!. Hii ni kweli?. Kwa vile hii ni ya kipindi kirefu nyuma, kwa nyinyi mlioko Mwanza, Jee mradi huo wa maji wa Buhongwa sasa unatoa maji?.
Haiwezekani kabisa juhudi kubwa zinazofanywa na rais Magufuli kutuletea maendeleo zikahujumiwa na watendaji, wakatafuna pesa, halafu wakazindua mradi fake kwa lengo la kumdanganya rais wa JMT na Watanzania wote kwa ujumla wetu.

Yaani rais Magufuli mpenda ukweli adanganywe mchana kweupe na waliomdanganya wapo tuu..
Yaya..

Nawatakia Jumapili Njema
Paskali
 
Hata yeye mwenyewe meko ni muongo, wakati wa kampeni aliahidi kuboresha maslahi ya wafanyakazi, akaahidi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa pia wakati anaongea na waandishi wa habari na wewe ukiwa miongoni mwao alisema bado Tanzania haijafikia kwa graduates wake kukosa ajira lakini mpaka sasa tatizo la ajira linaendelea kuwa kubwa (exponentially). Kwahiyo meko ndiyo kinara wa uongo kwenye serikali yake.
 
Aliyesababisha watu wawe waongo ni Magufuli mwenyewe. Hataki kuambiwa ukweli na watu wakagundua dawa yake ni kupiga mapambio yaliyojaa uongo mwanzo mwisho na yeye atachekelea na kufurahi huku akiwatupia vijembe wapinzani wake
 
Huyu Meya ni hovyo tu, shule zake za Alliance zinafutiwa mitihani kila siku kwa kuiba mitihani,na inaonekana yeye ndio mzizi wa wizi wa mitihani, kama anakuja kwenye equity ....aje na clean hands.......mwizi wa mitihani huyu. Mkoa umchunguze huyu Meya, na mtandao wake wa wizi wa mitihani,anauchafua mkoa kwa tabia hii ya wizi

Ubunge wa Nyamagana ataendelea kuuota tu.....aongeze mbolea aote vizuri
 
Huyu Meya asaidiwe, kuna tatizo kubwa Mwanza. Haiwezekani mtu atoe hoja nzito kama hizi alafu zipuuzwe.

Alafu kwa mfumo wa kiusalama ulivyo wanawezaje kupanga uongo kama huu bila mkuu wa nchi kujua? This is very serious
 
Huyu Meya ni hovyo tu, shule zake za Alliance zinafutiwa mitihani kila siku kwa kuiba mitihani,na inaonekana yeye ndio mzizi wa wizi wa mitihani, kama anakuja kwenye equity ....aje na clean hands.......mwizi wa mitihani huyu

Ubunge wa Nyamagana ataendelea kuuota tu.....aongeze mbolea aote vizuri
Kamanda bamia zimeshakomaa?nakuja Mbutu leo,sasa hivi navuka ferry...kama bamia zipo niambie ntapata kiasi gani na bei yake leo vipi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom