Unawakumbuka Kyanga Songa na Kassaloo Kyanga??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unawakumbuka Kyanga Songa na Kassaloo Kyanga???

Discussion in 'Celebrities Forum' started by KIM KARDASH, Jan 4, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Green Garden opposite JJ Bar (Kitimoto)!
   
 3. ng'wanankamba

  ng'wanankamba JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Walikuwa wanasiasa?
   
 4. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  wanasiasa za muziki..
   
 5. Futota

  Futota JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  tubandikie nyimbo zao hapa kidogo tujikumbushe enzi hizoooo za mwaka 47
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Kyanga songa na kasaloo kyanga kulwa na dotto washafairiki wote hao
   
 7. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,893
  Likes Received: 5,346
  Trophy Points: 280
  style yao ya nywele ilikuwa inanifurahisha kuliko mziki wao,..kila weekend pale riverside bar ubungo,..nilikuwa dogo and broke
   
 8. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Sijui yupi kulwa na yupi Doto!
  [​IMG]
   
 9. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Huyu wa kwanza ndio Mwanamuziki Selemani Kasaloo Kyanga ambaye alikuwa pacha wa Kyanga Songa(huyo wa chini -DOTO) walizaliwa Kongo mwaka 1957. Walikuwa ni nyota katika bendi zote walizopitia nchini zikiwamo, Matimila, Makassy, Maquis, Sambulumaa, Ngorongoro Heroes, Tancut Alimas, Sandton Sound, Kalunde Band na bendi nyingine nyingi . Kasaloo aliyetangulia kuingia nchini akifuatana na Skassy Kasambula mwaka wa 1980, aliweza kutingisha anga za muziki kuanzia pale aliposikika kwenye nyimbo zilizorekodiwa na Super Matimila. Kyanga nae akisindikizana na Issa Nundu walifuatia na sauti zao kuanza kusikika katika recording ya Orchestra Makassy na zile nyimbo Olenge,Bembeya,na pia kuimba na Masiya Radi katika nyimbo Tunagombana Bure. Kyanga alifia Kenya na Kasaloo jijini Dar es Salaam kutokana na mapafu yake kujaa maji. Alikuwa Sandton Sound Band aliyojiunga nayo akitokea Kalunde Band
   
 10. Futota

  Futota JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  maskini! wote walikufa bado vijana, inaonekana wali succumb to the complications of the new disease. jamani mwenyezi mungu atanusuru waswahili, tunakwisha na huu ugonjwa
   
 11. t

  testa JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wakiwa Tuncut Almas walijulikana kama mabush stars,hawa jamaa walikuwa wanajua kuimba mimi nilipenda walivyokuwa wasafi jukwaani
   
 12. T

  THE WHITE ELEPHANT Member

  #12
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na kucheza pia umesahau,walikua wanalishambulia sana jukwaa la fimbo lugoda tisa kumi mangalaa!
   
 13. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Kaka hawa jamaa walikuwa moto wa kuotea mbali sauti zao zilikuwa tamu kama asali,kila wimbo walioimba ulikuwa una hit,na kila bendi waliyoeenda nayo ilikuwa inakuwa juu,waimbaji sampuli ya hao ndugu waliokuwepo na waliopo ni wachache sana,naweza kuwaweka kundi moja na akina Nico Zengekela,Bichuka na pia kuna mwanamuziki Mtanzania mmoja kafia Kenya aliwahi kupiga na hao mapacha walipokuwa Tancut halafu akaenda Watunjatanjata ya akina Sheggy na mwisho akaenda Vijana kabla ya kuishia Kenya sijui alikuwa aitwa Shaweji sikumbuki .kwa hao watatu hakika walikuwa na sauti za kumtoa nyoka pangoni kiukweli
   
 14. M

  Majala Kimolo JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 344
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Swadakta kaka, mmojawapo alioa kwa akina Mpangala na alimtungia wimbo kwa jinsi alivyomjali. Amepiga muziki na akina John Kitime, Kawelee, na wengineo. Enzi hizo Iringa kumekucha. tancut Club, Jumba la maendeleo. Wakiwa tancut walichukua ubingwa wa bendi bora kitaifa.
   
 15. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Kuna mmoja alimuoa Jeni Butinini sijui ni yupi kati ya hao na sijui kama walikuwa na mtoto maana na mimi Iringa niliondoka siku nyingi sana na sijui kama huyo Jeni naye bado yupo. Ila ninachojua familia yao walikuwa wanapenda sana michezo. kuanzia mama na wanawe. nilikuwa nawajua Jeni, Bethi au mama Happy (huyu nasikia naye alisha fariki) na kaka yao Duncan Butini.

  Nakumbuka baadhi ya nyimbo zao hao mapacha kama "Mama -------- aah mama aa........... aa naona raha..... miezi tisa ya uchungu tumboni mwako yote umevumlia mama-------------- uchungu mwingi umeupata aa mama..................", na mwingine "Ninakwenda safari safari yenyewe ya masafa marefu ---------------- najua kama utabaki watasema mengi pia wabaya wetu mama watafurahi.......................safari sio kifo mama iyeye subiri nitarudi mama iyeye......................."

  Kwa kweli enzi hizo inangawa nilikuwa kinda lakini miziki ya enzi hizo kweli huwezi kuilinganisha hata robo na miziki ya vijana wa leo ambao 90% kati yao kutwa kucha kuwaza ngono. kutoboa masiko, kupaka lipstiki na angel face, kutumia karolite hujui yupi mwanaume na yupi mwanamke ukiwaangalia unaona wote wanawake maana wote wamejipamba na kujiita Sharouharo. hivi mimi sijui kama huwa wanasimamisha

  na pengine ndio maana siku hizi wanaume wenye uwezo wachache wengi bila bila viagra hawawezi kwa sababu miili imejaa kemikali, vyakula vya supamaketi n.k. samahanini msinimalize.
   
 16. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Simjui mpangala unaemzungumzia,lakini ninachojua alieoa iringa ni huyu marehemu kasaloo na mkewe ndio huyo kamzika,huyo dada anaitwa Jane Butinini ambae alimtungia wimbo mzuri uitwao butinini akiwa tuncut almas,huyu dada alikua mcheza netiball mashuhuri akichezea timu ya NBC Makao makuu kuna kipindi,alikua mrembo sana enzi zake huyo jane,na pia alikua na kaka yake akiitwa Duncun Butinini baba yao alikua polisi sasa hivi amestaafu yupo iringa,jane alikua anaishi na kasaloo hapa dar!duncun butinini yeye alifariki,enzi hizo alikua mshambuliaji hatari wa reli ya morogoro kiboko ya vigogo ikiitwa
   
 17. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ule wimbo butinini kumbe alimuimbia demu wake?niliupendaga sana ule wimbo..
   
Loading...