Unawahi kufika kileleni? Unachelewa kupata nguvu za kurudia tendo?


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,064
Points
2,000
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,064 2,000
Dawa ni hii
Uwanja wetu wa leo, utakuwa na kazi moja tu, kujadili tatizo la kuwahi kufika kileleni, kuchelewa kupata nguvu za kurudia tendo, chanzo na tiba yake. Dhumuni la kuandika mada hii limetokana na maoni ya wasomaji wengi.

Wasomaji hao ambao wengi ni wanaume, waliniomba niwaandikie hivyo ili kunusuru uhusiano wao. Wengine wapo kwenye ndoa, kwahiyo waliniambia kuwa ushauri wangu unaweza kuwa tiba timilifu kwao.

Hivyo basi, kutokana na kutambua umuhimu wao, ndiyo maana sijasita kuandika haya unayoyasoma.

Tatizo la kuwahi kufika kileleni, mara nyingi huendana na mambo mengine ambayo huchagiza wenzi wengi kusalitiana ama kutengana kabisa.

Wanawake wengi wanagombana na watu wao kwa sababu kama hizi, hawavutiwi kuwaona waume wao wakiwahi kufika kileleni, hivyo kushindwa kuwapa dozi inayotosheleza.

Wanasikitishwa na hali ya wenzi wao ya kukosa nguvu za kutosha wakati wa kufanya tendo la ndoa ama ugoigoi wa kuchelewa kurudiwa na nguvu za kufanya kweli.

Aidha, wanakosa amani wanapobaini kwamba wapenzi wao hawana msisimko wakati wa kufanya yale ‘mambo yetu'. Hata hivyo, tunapogeuka kisaikolojia hili si tatizo kubwa, bali linahitaji kutuliza akili.

Ninaposema kutuliza akili, nakuwa namaanisha kuwa wengi hawana magonjwa yanayohitaji dawa, isipokuwa wanasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia tu.

Vijana na baadhi ya watu wazima wengine wanaenda kwa waganga na wakati mwingine wakijikuta wanajiingiza katika matumizi ya mitishamba bila kuelewa kwamba ugonjwa wao haupo kwenye kasoro za kimaumbile, bali upo akilini.

Hapa nataka tukubaliane kwamba jambo kubwa linalowasumbua wanaume wengi wanaodai kuwa hawana nguvu ni ukosefu wa elimu ya mabadiliko ya kibinadamu na ufahamu duni wa mbinu za kuwawezesha kucheza michezo ya kimapenzi kwa ufanisi.

Mpenzi ni sanaa pana, ina mafunzo mengi na ili uimudu, unatakiwa ujifunze kila siku mabadiliko yaliyopo. Sambamba na hilo, kujua mapito, mazingira, mabadiliko ya mwili na kuyakubali ni mambo ya msingi.

Pamoja na matatizo haya kuwakera wanawake kama nilivyotangulia kusema, huwafanya wanaume kukosa amani. Mara nyingi wanaopata dosari hizi, hujihisi wana nuksi.

Hata hivyo, mshangao unaokuja hapa ni kwamba wanaume hupenda kutafuta mbinu za kutatua tatizo lao bila kuwashirikisha wenzi wao, kana kwamba wao haliwahusu.

Saikolojia inatambua kuwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ni zao la udhaifu wa mke na mume na sio la mwanaume peke yake kama watu wengi wanavyodhani.

Kwa mfano, mwanaume atapata wapi msisimko wa kimahaba kama mwanamke hatakuwa mtundu wa kubuni mbinu za kuufanya mwili uliopoa usisimke?
Atavutiwa nini mwanaume kurudia awamu ya pili, ikiwa kwenye mzunguko wa kwanza alikutana na harufu isiyofaa? Nakshi nakshi humuongezea mwanaume hamu ya kutaka tena na tena. Huo ndiyo ukweli!
Napenda niweke ukweli kweupe, mara nyingi tatizo la msisimko wa kurudia tendo, husababishwa na mwanamke mwenyewe. Kwa maana hiyo, ili litatuliwe ni lazima ziwepo juhudi za pande mbili.

Tuweke kituo kwa leo, nakuomba tukutane wakati ujao ili tuendelee na mada hii. Bila shaka, tutakapokutana ‘ishu' ijayo, utaweza kung'amua mengi kuhusu somo hili. Mimi na wewe tupo together as one.
 
Buchanan

Buchanan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,207
Points
1,500
Buchanan

Buchanan

JF-Expert Member
Joined May 19, 2009
13,207 1,500
Mkuu MM, punguza maneno mengi, nenda straight kwenye point! Ubarikiwe!
 
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
17,686
Points
2,000
Age
46
gfsonwin

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
17,686 2,000
mie nilijua leo umekuja na dawa ya mkuyati kumbe sentensi tu???

ila kuna ukweli hapo kwenye aya ya mwisho ama niseme ya pili kutoka mwisho, kwamba wanamke anatakiwa awe initiator wa second round. but kuna scenario ambazo mwanaume hataki tena mara ya pili yaakin akishashuka mara ya kwanza basiiiiiii hata mwanamke awe mtundu amfute kwa mavitambaa yaliyolowekwa kwenye yasimini bado tu mwanaume atadai subiri baadae. wengine hudiriki kutoka na kwenda kutafuta japo juice ili mpenzi apate nguvu ya mwili waendelee lkn wapi eti nimechoka sasa hapo napo mwanamke alaumiwe??

wanaume wakubali kwamba kwenye swala la mapenzi wao huwa wanaona wanawake kama hawana haki na kufurahia tendo wao huona wakisha kojoa waoo basi, mwanamke atakuwa amekojoa. kumbe si kweli. ungeanza kwanza kuwaambia wanaume waache ugoigoi labda ingesaidia.
 
Mwanawalwa

Mwanawalwa

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2012
Messages
1,015
Points
1,195
Age
19
Mwanawalwa

Mwanawalwa

JF-Expert Member
Joined May 28, 2012
1,015 1,195
studies zinaonesha round moja ni sawa na 14km asa dah jamaa lazima achoke manake mmh ila diet ya samaki kama jodari,changu,chuchunge nadhani wanasaidia kuboost energy
 
C

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Messages
12,379
Points
2,000
Age
59
C

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2011
12,379 2,000
mie nilijua leo umekuja na dawa ya mkuyati kumbe sentensi tu???

ila kuna ukweli hapo kwenye aya ya mwisho ama niseme ya pili kutoka mwisho, kwamba wanamke anatakiwa awe initiator wa second round. but kuna scenario ambazo mwanaume hataki tena mara ya pili yaakin akishashuka mara ya kwanza basiiiiiii hata mwanamke awe mtundu amfute kwa mavitambaa yaliyolowekwa kwenye yasimini bado tu mwanaume atadai subiri baadae. wengine hudiriki kutoka na kwenda kutafuta japo juice ili mpenzi apate nguvu ya mwili waendelee lkn wapi eti nimechoka sasa hapo napo mwanamke alaumiwe??

wanaume wakubali kwamba kwenye swala la mapenzi wao huwa wanaona wanawake kama hawana haki na kufurahia tendo wao huona wakisha kojoa waoo basi, mwanamke atakuwa amekojoa. kumbe si kweli. ungeanza kwanza kuwaambia wanaume waache ugoigoi labda ingesaidia.
State of mind- akili yako imekuwa tuned vipi kabla ya kuanza machezo! Pili mazoea- mwenzako mmeishi pamoja miaka , jamani matamanio yanapungua. Ni ukweli ambao unauma lakini lazima tuuseme. Mbinu za kamsha matamanio katika hali hiyo ni zipi?
 

Forum statistics

Threads 1,283,676
Members 493,764
Posts 30,796,549
Top