eucalyptos
JF-Expert Member
- Jan 23, 2010
- 391
- 139
mkuu umeshtukia ee?msiumize vichwa na watu wenye low self esteem.ni kawaida sana kusikia madaktari wa muhimbili wauaji,manurse wa mwananyamala wanaua watoto,hospitali ya amana ni machinjion n.kingawa ukijaribu kuuliza uthibitisho wa madai haya utasikia vijistori vya kutunga!Kinachoshangaza huwezi kusikia madaktari au manurse wakisifiwa hasa pale afya ya mtanzania inapoboreka mfano vifo vya mama na mtoto vikipungua sana sana utasikia sifa inaenda kwa mkuu wa mkoa au kwa chama tawala.Fundi mchundo haelewi kwamba serikali inalazimisha madaktari bingwa waende mikoani sasa anategemea madakta hawa wakatoe emperical treatment kama Clinical officers?!wanahitaji vitu kama C.T SCANNERS n.k kama tunaweza kununua mashangingi zaidi ya 200 kwa wabunge iweje tushindwe kununua hizo scanners kwa mikoa 28?
Hiyo ni kuwambia ngoma kwako. Si siku nyingi sana Mwaka huu kuna muhudumu wa afya (nurse/mid wife) wa pale TMJ alifanya "kazi yake kwa mujibu wa kiapo" kwa kumtolea damu mama aliyekuwa akijifungua akiwa hana damu. Aliokoa uhai wa mama huyu pamoja na mtoto. Japo muhudumu huyu alikuwa mwenyewe alifanya hayo yote.
JE HUKUSIKIA MAJIBU YA WANANCHI, WAMILIKI WA HOSPITALI, FAMILIA YA MGONJWA, VYOMBO VYA HABARI ETC KWA MUHUDUMU HUYU?
Tuache propaganda kwenye mambo yanayoonekana wazi.