Unawafahamu vizuri madaktari wa muhimbili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unawafahamu vizuri madaktari wa muhimbili?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GAZETI, Jun 19, 2011.

 1. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,525
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Habarini wana JF. Bila shaka kuna watu hawawafahamu vizuri madaktari wa muhimbili. Ni watu watanashati wenye sura zenye upole na upendo. Ukikutana nao ni watu wastaarabu ambao kwa mtazamo wa haraka ni watu wenye maadili mazuri ya kazi. OLE WAKO UINGIE ANGA ZAO! Nazungumza kutokana na uzoefu nilioupata kule MOI.

  Nenda na Bima yako nenda na pesa yako ya kulipia vyeti halali, Unajua wanachokifanya? Utapangiwa tarehe kila siku mpaka utoe yale malipo yasiyo na risiti ndo utapata huduma. Nawaombeni madaktari kama mmebahatika kusoma post hii mubadilike huu ukatili mnaoufanya si nzuri mnaotuumiza ni sisi ndugu zenu Watanzania wenzenu. Hebu kuweni na huruma sura zenu zifanane na nyoyo zenu. Kwanini mnakuwa na
  SURA ZA TWIGA LAKINI NYOYO ZA NYOKA?
   
 2. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  watu tunasema tusitoe rushwa lkn hujauguliwa nakumbuka mjombaangu alipozidiwa jamaa wakasema operation labda bada ya siku nne wakati mjomba analia machozi ilibidi niongee na muuguzi mmoja kuweka mambosawa na kweli siku hiyohiyo akafANYIWA OPERATION ILIYOUDUMU KWA SAA TANO madr. mhmbili mbadilike jamani
   
 3. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2011
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Ndugu yangu wale watu ni hatari sana, yaani unashindwa kutofautisha kati ya askari na daktari, wao ni migomo mbele lakini mambo wanayotufanyia ni balaa. Halafu kwa kujitetea wanaongoza nahisi ni FREEMANSON wale.
   
 4. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ni MOI au MUHIMBILI?
   
 5. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,525
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  moi - muhimbili orthopedic institute
   
 6. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nawasiwasi hata wewe ni mmojawapo wa wale wasiowafahamu vizuri madaktari yaani hamtofautishi physiotherapists, occupational therapists, pharmacists, nurses, auxillary staffs au madaktari.

  Hata hivyo haisadii kuwalaumu wafanyakazi wa sekta moja tu, wakati jamii nzima imeoza. mbunge anadai mamilioni ya pesa kutoka kwa wachimba dhahabu ili kuzima vifo vya raia, amepata wapi huo ujasiri wa kufanya hivyo? jibu ni kwamba anauzoefu wa ikulu na anajua yote yanayotendeka huko. Uozo ni kutoka juu hadi chini, sasa madaktari wao wafanyeje wakati nao ni sehemu ya jamii? Mahitaji yao ya kila siku watayatimizaje? Wewe na mimi wote tunajua mishahara haitoshi.

  Nchi sasa ni kitendawili, ni mwendo wa kutega na kutegua tu mpaka pale watanzania wenye uwezo na uelewa watakapo pata nafasi ya kuikomboa nchi yao.
   
 7. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapana, ni al qaida
   
 8. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,525
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Hiyo Physiotherapists unaijua wewe. Siwezi kukubaliana moja kwa moja na kauli yako madaktari wengi wana hali nzuri ya kipato. Hao wanaochukua rushwa wengine ni madaktari Bingwa. Yamenikuta kufanyiwa Operesheni ilinigharimu Tsh 250,000 hiyo ni nje ya malipo halali. Ndipo daktari akajadiliana na daktari mwenzake wakakubali kufanya mwz wa 2 badala ya mwezi wa 12 ambao tulipangiwa kurudi tena hospitali na si kufanyiwa Operesheni.
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nafikiri hili ni muhimu sana ulifikishe kwenye vyombo husika hususan TAUKURU ili kulkomesha kabisa
   
 10. C

  Claxane Senior Member

  #10
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole sana kama ulichosema ndivyo.tukamatie hao madr ili wawajibishwe wewe huoni kutoa rushwa ni kosa
   
 11. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  nilitaka ufahamu kuwa kuna muhimbili national hospital(MNH) na hiyo MOI uliyoitaja.Rekebisha hiyo title ya thread inageneralise sana.
   
 12. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  hebu mweke hapa huyo dr jina lake tumchambue. unaogopa nn mtu wako si ameshatibiwa???,, wakija nje huku hawapewi ruhusa kutibu mtu wao kazi yao ni kuwashikia madaktari wa huku mikasi na madawa wkt wa operation.taaluma yao ni ya mashaka ndio maana huku hawaminiwi hata kidogo, wa nje hawezi kufanya upuuzi kama huo wao wanatibu mapema na ukipona ni sifa kwao wanaapublish pepa kuongeza credit.Ndio maana muh2 vifo vya kijinga haviishi,mm binafsi walishaniharibia mwanangu kwa kumdumga masindano ambayo sio na kumuovadozi mtoto karibia angekufa,lkn wao hawajali.
   
 13. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwa kifupi hospitali zote za Tanzania ni uozo.
  Pesa ndiyo inayoongea.

  Hata pale unapolipa pesa kibao kama aga khani usumbufu kibao hadi umuone dr kama upo serious unafia kwenye benchi.
  Hakuna wito ni ubepari mtupu. Mbeba fail anataka rushwa hadi kumfikia dr umetoa za kutosha na. wanaomba vipi chai au nipeleke fail hivi hivi tu?

  So hii nchi tunakoenda kugumu mno!
   
 14. m

  mpasta JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 383
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 60
  mshahara mdogo kila mtumishi wa serikali analalamika,,,hivyo sio justification ya kuchukua rushwa,,tene ukiwa unahusika na uhai wa mtu sio vizuri kufanya mskhara na uzima wa mgonjwa,,,,,
   
 15. C

  Claxane Senior Member

  #15
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe kapumzike tu hakuna asiyetaka kufanya kazi yenye hela nyingi.huko kwa wakoloni ulikuko unabeba mabox au unapasua mawe kwani ndugu zako wametibiwa na wanapona visa haijaisha?
   
 16. regam

  regam JF-Expert Member

  #16
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ili ishu yako ishughulikiwe na takukuru lazima utoe kitu kidogo amasivyo wanaipotezea! Upo hapo?
   
 17. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,525
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Ok inawezekana kuna makosa katika uelewa lakini Karibu asilimia 95 ya Watanzania wanajua muhimbili ni moja tu. Iwe MOI au MNH hiyo ni muhimbili tu. Wodi yoyote atakayopelekwa mtu ni muhimbili tu! Sijui huko kwingine inakuwaje lakini nimewahi kufika mara 3 huko Muhimbili kwa Case 3 tofauti, moja ikiwa inanihusu zaidi na kunilazimu kuingia mimi mwenyewe mfukoni. Na nathibitisha kushuhudia mkusanyiko wa bahasha kama zangu. Ni wauaji tu, wao kwao kifo cha mtu ni kitu kidogo sana.
   
 18. Mr. Bigman

  Mr. Bigman JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,843
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Hawa madaktari si ni wale wenye kupasua kichwa badala ya goti na kinyume chake? Tafakari na chukua hatua
   
 19. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  kuna clinical Dr. mmoja ambaye sina uhakika kama mpaka sasa anasoma masters yake au kesha graduate. Jina lake linaanzia na herufi G, aliwahi kufanya kazi hospitali ya rufaa mbeya.
  Huyu jamaa ni hatari sana, anatanguliza rushwa kwa kila jambo. Ni mtu wa majigambo na kujifanya yeye ni kila kitu kwa matatizo ya binadamu. Naandika haya kwa sababu yamewahi nikuta.
  Kwa vitisho ndo usiseme, ana confirm ugonjwa bila hata ya vipimo. Ili mradi tu ku-justify kiwango cha rushwa anayoitaka.
  Ni mlevi wa kupindukia, anakunywa mpaka anajitapikia.
  Samahani kwa kuandika haya maana yalishanikuta nilipokuwa namshughulikia ndugu yangu. Alimzushia ana cancer ya koo, hakuweza hata kumuandaa psychologically kumpa hizo hisia zake kwa sababu hakuwa ka-confirm kwa kipimo cha aina yeyote. Baada ya kula hela akaanza kukwepa appointments,
  Baadae nilihangaika sana mpaka ocean road wakasema dogo hana cha cancer wala nini. Ilikuwa bi infection ya kawaida.
  Ilibidi nimuweke sawa huyo Dr. G (mchaga), nilimuambia bila kumung'unya maneno kwamba kama taifa ndo linategemea watu wa type yake taifa litaangamia. Hata leo hii akisoma hii thread atajua ni nani aliyeandika haya. Na si majungu ila ni ukweli ili ajirekebishe na kutambua ya kuwa udaktari ni wito.
  Serikali yenyewe haina uwezo wa kumlipa daktari mpaka sasa, ingekuwaje kama wazee wetu waliokuwa madaktari wangetanguliza tamAa za fedha mbele? Hata Dr. G huenda asingekuwa daktari leo hii.
   
 20. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwa kutomtaja jina ndiyo unamwachia aendelee na uovu wake ambao bila shaka utawagharimu wengine maisha yao. Badala ya kulalamika tu, ni lazima tuwe majasiri wa kuwataja waovu bila kificho. Kwa kufanya mnachokifanya hamsaidii jamii.

  Amandla....
   
Loading...