Unavyoweza kunufaika kwa kufanya tendo la ndoa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
Saikolojia na maisha
pix.gif
Kiafya
Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Wataalamu wanasema kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.

Kuongeza mwendo wa damu
Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili, hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji.

Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.

Hupunguza mafuta yenye kileo (Cholesterol)
Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha mafuta yenye kileo mwilini.

Kupunguza maumivu
Wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo hupunguza maumivu kama vile kuvimba sehemu za viungo (arthritis) maumivu ya shingo (Whiplash) na maumivu ya kichwa.

Ulinzi wa tezi ya kibofu (mwanaume)
Majimaji yanayozalishwa katika tezi ya kibofu (prostate) yakizidi husababisha kuleta matatizo mwilini. Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji hayo yenye madhara. Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa huelekea kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate.

Kupunguza mfadhaiko wa moyo
Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini. Watu wenye kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.

Huongeza uzalishaji wa homoni za kiume(testosterone) na za kike (Oestogen).
Faida nyingine inayopatika ni kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za kike likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi. Hata hivyo, baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kiume/ kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.

Kuishi muda mrefu huku ukionekana kijana
Wakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima. Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka. Kutokana na elimu hiyo DHEA ni kemikali yenye nguvu duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu, kuimarisha mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo (Cardiovascular).

Hupunguza baridi na mafua
Elimu inaonesha kuwa wanaofanya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki huongeza 30% ya uzalishaji wa chembe chembe hai za mwili ziitwazo Immunogloulin A ambazo huwa na kazi ya kuulinda mwili dhidi ya magonjwa. Hizo ni faida chache tu za kufanya tendo la ndoa.

Wakati mwingine nitawaletea hasara za kufanya tendo hilo mara kwa mara. Jambo kubwa la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa. Ndiyo maana nikasema ni maalum kwa wanandoa tu.
 
du safi sana nitadumisha nilikuwa sijui kama ni nzuri kiivyo kwani kunawapotoshaji wengi kama kina dr ndondi kwamba ukifanya kimoja unapunguza siku 3 za kuishi
 
Duh mshikaji unaamini kirahisi! Fanya utafiti na wewe
 
MKUU Magehema mimi nimenukuu kwa Wataalam sio mimi niliyoyasema wewe kama huamini jaribu kamuulize doctor anayehusika na hayo masuala kisha uje hapa kunipinga mimi upo na mimi mi Mkuu Magehema?
 
pix.gif

KAMA ilivyo ada tumekutana kwenye kona yetu ya mahaba kutaka kujuzana mawili matatu kuhusiana na mambo ya kila siku katika maisha yetu ya mapenzi...
Leo nataka nizungumzie simu ya kiganjani ambayo teknolojia hii kwa sasa imekua na kusambaa kwa haraka sana na kumilikiwa na watu wa kipato cha aina zote.

Simu imekuwa kiunganisho kikubwa katika masuala ya mapenzi pia imekuwa ikitumika kuvunja ngome za mioyo ya watu. Simu hiyo hiyo imekuwa chanzo cha mifarakano katika nyumba nyingi pale inapokuwa kiunganisho cha usaliti kati ya mtu na mtu.

Watu wengi wamejikuta wakiitumia kinyume na kusudio la simu ya kiganjani nia na madhumuni yake. Simu ni mawasiliano mepesi ambayo humrahisishia mtu kuweza kuwasiliana na mwenzake kwa urahisi. Kwa mfano mume na mke simu huwasaidia hata kupanga mambo yao wawapo mbalimbali bila mmoja kufunga safari kumfuata mwenzake.

Lakini imekuwa tofauti kabisa simu ya mkononi imekuwa ndiyo ghala la kufichia maovu ya wana ndoa, kufikia hatua ya kumuwekea mwenzako mipaka asiiguse simu yako. Hili jambo linakubalika kwa mwendawazimu tu lakini kwa mwenye akili timamu haliwezi kumuingia.

Kama unaweza kumuachia mwenzako mwili wako ausanifu atakavyo iweje simu uiwekee mipaka. Simu na mwili wako ambao unauvisha nguo ili mtu mwingine asiuone zaidi ya mwenza wako kipi chenye thamani?

Kumekuwa na mijadala mingi kuhusiana na mtu kuigusa simu ya mke au mumewe kwa vile anaweza kukuta vitu ambavyo si vizuri. Kama ni hivyo nini maana ya uaminifu katika uhusiano, upendo wa kweli una mipaka? Inaingia akilini?

Unawezaje kutumia simu ya rafiki yako kumpigia mtu kama salio lako limekwisha, lakini ya mumeo au mkeo usiiguse kwa vile mumewekeana mipaka, wasiwasi mkubwa ni kukutwa ujumbe wa mapenzi. Kweli hapo kuna ndoa au ndiyo maisha ya mazoea, upendo kitandani nje ya kitanda kila mtu na utaratibu wake?

Siku zote uaminifu katika ndoa ni pamoja na kuwa muwazi na mkweli kwa mwenzako, kama mnajua kuwa ninyi ni mwili mmoja pia ni watu mlioapa kuheshimiana na kuwa waaminifu katika uhusiano. Siamini kama utamruhusu mtu mwingine aingie moyoni mwako.

Siku zote muaminifu simu yake haimpi presha anapokuwa ameishahau hata mwenzake anapoishika, kwanini utembee na simu yako hadi bafuni bado unajifanya kichwa cha familia na kukemea tabia njema. Simu iacheni kama chombo cha mawasiliano na si kichaka cha ufuska.

Na Ally Mbetu Simu: +225 713 646500 E-mail: ambedkt@yahoo.com
 
Ahsante mkuu so siku nyengine njoo na hasara. maana kuna wengine huwa hatulali bila kupata. na wengine iki2pita cku mbili bc yatatu pushiepushie 4 au 5 ndio usingizi unakuja sasa twazalisha zaidi au
 
mmmmmh ita bidi tu chunguze kama kweli then tuki pata u hakika ita bidi tu boreshe zaidi na zaidi
 
Wakati mwingine nitawaletea hasara za kufanya tendo hilo mara kwa mara. Jambo kubwa la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa. Ndiyo maana nikasema ni maalum kwa wanandoa tu.

hasara au faida.................................jibu ni moderation and doing it for the right reasons........................
 
Kimsingi hii ni mada nyeti inayohitaji ufahamu mkubwa wa mambo. Ifahamike mapema kuwa

ninapozungumzia faida za tendo la ndoa sichochei watu wasio katika ndoa au uhusiano sahihi wafanye hivyo kwani ufanyaji wa mapenzi kiholela bila kujiamini kuna hasara kubwa. Ungana nami ili ujue faida za tendo hilo kwa afya ya mwili wako....

Kiafya

Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Wataalamu wanasema kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.

Kuongeza mwendo wa damu

Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili, hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji.

Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.

Hupunguza mafuta yenye kileo (Cholesterol)

Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha mafuta yenye kileo mwilini.

Kupunguza maumivu

Wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo hupunguza maumivu kama vile kuvimba sehemu za viungo (arthritis) maumivu ya shingo (Whiplash) na maumivu ya kichwa.

Ulinzi wa tezi ya kibofu (mwanaume)

Majimaji yanayozalishwa katika tezi ya kibofu (prostate) yakizidi husababisha kuleta matatizo mwilini. Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji hayo yenye madhara. Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa huelekea kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate.

Kupunguza mfadhaiko wa moyo

Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini. Watu wenye kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.

Huongeza uzalishaji wa homoni za kiume(testosterone) na za kike (Oestogen).

Faida nyingine inayopatika ni kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za kike likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi. Hata hivyo, baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kiume/ kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.

Kuishi muda mrefu huku ukionekana kijana

Wakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima. Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka. Kutokana na elimu hiyo DHEA ni kemikali yenye nguvu duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu, kuimarisha mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo (Cardiovascular).

Hupunguza baridi na mafua

Elimu inaonesha kuwa wanaofanya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki huongeza 30% ya uzalishaji wa chembe chembe hai za mwili ziitwazo Immunogloulin A ambazo huwa na kazi ya kuulinda mwili dhidi ya magonjwa. Hizo ni faida chache tu za kufanya tendo la ndoa.

Wakati mwingine nitawaletea hasara za kufanya tendo hilo mara kwa mara. Jambo kubwa la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom