Unavyofikiri Tanzania itajengwa na CHADEMA peke yake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unavyofikiri Tanzania itajengwa na CHADEMA peke yake?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwanaone, Apr 30, 2011.

 1. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
  ndugu zangu nataka tujadili kwa wazi thread hii hivi ni kweli nchi yetu itajengwa na chadema pekee? naomba tuongee ukweli tuache siasa za kishabiki haziwezi kutufikisha popote sisi watanzania wa chini ndio tutakaoumia so naomba tulijadili hili kwa maslahi ya taifa letu.
   
 2. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
  ndugu zangu hii thread nilishawahi kuileta hapa jamvini lkn haikupewa haki yake. nimeirudisha tena kwani kila nikifikiria huwa nakosa jibu hivi kweli chadema chini ya mbowe au slaa wataweza kweli kutuletea maendeleo tunayoyaota bila kushirikiana na vyma vyengine vya siasa?
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Wewe unasemaje?
   
 4. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hiyo sentensi "Chadema peke yake" umeitoa wapi? Halafu post yako ya pili inafanya usieleweke unauliza nini hasa. Nchi yoyote hujengwa na wananchi wake wakiongozwa na VIONGOZI WAZALENDO WA KWELI. Natumai nimekujibu ndugu.
   
 5. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hapo kwenye red una lako jambo bora ukawa mkweli kwanza wewe? nini hasa una wasiwasi nacho weka vitu wazi zaidi tuona kama hii hoja ina misingi, kwa jinsi ilivyokaa kwa sasa ni kama una majungu furani? mwisho chadema ni chama kinaongozwa na nguvu ya watu na hao uliowataja ni kama chombo cha kukiwakilisha chama , ya kwamba kila chama lazima kiwe na viongozi ila sio ndio inakuwa ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI, hiyo sio kwa CHADEMA ni kwa chama cha magamba (CCM)
   
 6. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
  ndugu kama itakuwa hujanifahamu nilikuwa namaanisha kama ifuatavyo. may be nilikuwa sijaliweka swali langu wazi ni kwamba ni vionozi wa chadema pekee ndio wanaweza kutuletea maendeleo bila ushirikiano wa viongozi wa vyama vyingine vya siasa ?
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  hizi ni thread za kina kupeng'e na jeykey ..... hamna hoja mpya humu zaidi ya jealous
   
 8. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Marekani wanaamini katika mabadiliko wewe unatuletea unafiki wako hapa.
  Hakuna nchi duniani inayoletewa maendeleo na mtu au chama fulani, ni watu wa hiyo nchi washirikiane na viongozi wasio na hila wala wizi kujiletea maendeleo.

  We want changes in our country the only solution for ufisadi.
   
 9. mwanaone

  mwanaone JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 635
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 180
  Mimi kaka siko kwa ajili ya majungu, na jingine napenda nikuweke wazi mimi si CCM, sijawahi kuwa CCM na wala sitokuwa CCM ktk maisha yangu yote niliyobakisha hapa duniani.

  Ninavyoamini mimi ni kwamba nchi yoyote duniani hujengwa na wananchi wakiongozwa na viongozi wao wote wawe wa chama kinachotawala wakishirikiana na vyama vyote vya kisiasa.

  Lakini tatizo ninaloliona mimi ni kwamba je serikali tunayoitarajia ya CHADEMA 2015 itakuwa tayari kushirikiana vyama vya upinzani hususani CCM na CUF.

  Kwa sababu hivi sasa chadema imegoma kushirikia na vyama vyote vya upinzani kwa kuwa inasema ni vyama ambavyo sio makini vinatumiwa na CCM.

  SASA NINAVYOAMINI MIMI MAENDELEO YA KWELI YATALETWA KWA USHIRIKIANO WA VIONGOZI WETU BILA KUJALI TOFAUTI ZAO ZA KISIASA.
   
 10. Pelle mza

  Pelle mza JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2011
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 749
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Sio kweli isipokuwa baadhi ya viongozi wake angalau wamediliki kutamka neno Uzalendo wao na wananchi wazalendo tunaweza kuijenga nchi yetu
   
 11. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,084
  Trophy Points: 280
  Nchi hii itajengwa na wananchi wazalendo wa kweli wa ngazi zote, makabila yote, dini zote, kanda zote, lugha zote, jinsia zote, umri wote, wasomi kwa wasiosoma, wakulima kwa wafanyakazi, na makundi yote ya kijamii.

  Hakuna mwenye haki miliki ya Tanzania; sio CHADEMA, CCM, au chama kingine chochote; ila kwa mfumo uliopo sasa hivi, kama ilivyo vitani ambapo majemadari wanahitajika kuongoza mapambano, ndivyo kinavyohitajika au vinavyohitajika vyama vya kutuongoza kufikia ushindi na ushindi ni ustawi mwema wa taifa letu. Lakini sharti majemadari (chama/vyama hivyo) viwe na nia na malengo mamoja vinginevyo itakuwa mafarakano na malengo hayatafikiwa.

  Sasa kwa maelezo hayo, pima mwenyewe ni chama/vyama gani vinafaa kuongoza Tanzania.
   
 12. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nchi inajengwa na wananchi sio vyama , mradi tu wapatikane viongozi bora wenye vision.
   
 13. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mimi naamini hivyo!
  Ndani ya uongozi wa slaa na mbowe;
  - hatutahitaji kulima
  -tutakula manna na salwa kutoka mbinguni, yaani kwa taarifa yako itakuwa bab kubwa kuliko hata ile ya wanawaisreil.
  kila mtu atakuwa na helkopta yake na hata barabara hazitahitajika ndo maana hata sasa hivi chadema tunaponda kikwete kuendelea kupoteza hela kujenga mabarabara wakati tukijua fika sisi 2015 itakuwa mdo mwisho wa kuzitumia.
  yako mengi ila muda hautoshi ila nyie tupeni hii nchi mtaona kwa macho yenu.
  kurespondi swali lako na sema big YES, chadema pekee inatoshe hivyo vingine viiflie mbali. Naami hivyo siunajua ukiwa na imani unaweza vuka bahari kwa miguu! Asante.
   
 14. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Vyama ni last matter, sisi Watanzania ndio wajenzi wa nchi, hatufuati chama, mtu.
   
 15. A

  Abba Member

  #15
  Apr 30, 2011
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We mwanaone sijui kama uko tayari kuona.Chadema imesema wazi kwamba iko tayari kushirikiana na chama chochote makini katika mapambano yake dhidi ya chama tawala. Vile vile chadema imekuwa tayari kuwapokea wanaccm safi, wazalendo na wapiganaji wa kwa nchi hii.lakini hawa wasipojiunga na chadema sio kwamba chadema itashindwa kuleta maendeleo. Maendeleo yataletwa na vision, beliefs, uzalendo, uchapakazi na uungwaji mkono wa wananchi, ambavyo vyote vinaonekana kupatikana kwa CDM kwa sasa!

  Wewe nini hofu yako? Kwamba chama chako ulicho kipenda kinaendelea kupoteza umaarufu?kwamba cha dini yako kimepoteza muelekeo, kwamba chama chako cha ukanda hakina tena mvuto kisera? Uanyo options moja tu: waambie viongozi wako warudi na kutetea maslahi ya watanzania na wasiangalie mapambano ya tanzania mpya katika jicho la dini, ukabila na ukanda!

  There is no thing as tule wote kwenye Chadema!
   
 16. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mtoa thread kauliza swali la msingi sana. Nahakuna mchangiaji aliyetoa jibu lenye maana.
  Sera ya CDM inaelekea ni kuipinga CCM , sera ambayo naona si mbaya ila haina filosofia ya kule wanakoelekea wana CDM.
  Kwa post kama hii ndio unaona jisi CDM vipofu wanavoongoza vipofu wenzao.
  Zaidi ya ufisadi,suala linaloweza kudfanywa vizuri tu ma wanaharakati, CDM haina muono wala sera ya muelekeo kifilosofia.
  Kama ni mafisadi CDM wako tele na wanafahamika.
  Ni vyema tukaelewa kuwa kama CDM ikikamata nchi uchumi utakuwaje,siasa ya ukulima itakuwaje, wafanyakazi wattendewa vipi. Nasuala la uwekezaji umekaa vipi kulingana na rasilmali za waTanzania.
  Nina uhakika watakachokuja nacho ni kama chama tawala tu maana CDM haina jipya zaidi ya kuingia madarakani.
   
 17. fige

  fige JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wanajua sera za cdm na kila siku wanahaha kuzitekeleza kwa hiyo usiwabeze.nakama wanafanana basi na wao wapewe nchi tuone ,labda useme wao ni worse than ccm na ujenge hoja ya utetezi
   
 18. M

  Makupa JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  cdm sio chenye malengo ya kutwaa dola
   
 19. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #19
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Labda utusaidie ni sheria ipi inataka chama tawala kishirikishe vyama vingine katika utawala?? Je vyama vina uhuru kisheria wa kuunda serikali kama vimeshinda au vinalazimishwa kuungana? Na kama sheria hiyo haipo kosa la UDP, CCM, NCCR, CHADEMA, CUF na vyama vingine liko wapi? Kuna nchi vyama vinaungana ili kupata wingi unaohitajika kisheria, na kuna nchi chama kinachoshinda ndicho kinaunda serikali. Tanzania sheria inasemaje? Tunalaumu hivi vyama kihalali au ni udanganyifu wa wazi tunafanya? Na kama ni hivyo kwa nini sheria inaruhusu vyama zaidi ya viwili?! Maana tungekuwa na viwili tu ili chama A kikiwa madarakani chama B kiwe upinzani na vice vesa. Maana hizi porojo za kulazimisha vyama A,B.C,D, E nk kuungana bila kuwa na katiba ya hivyo zinashangaza.
   
 20. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  unaposema chadema pekee unamaanisha viongozi tu au pamoja na wanachama?
  Nchi itajengwa na wananchi, kama wananchi hawapo tayari kujenga nchi yao hata viongozi wafanyaje nchi haiwezi kuendelea.
  Kuna mambo mengine yanahtaji comittment za wananchi wenyewe. Mfano, uchafuzi wa mazingira, huwezi kublame viongozi iwapo wewe mwenyewe unatupa taka hovyo na unajisaidia barabarani!
   
Loading...